Nimepata kazi sina nauli, nauza vitu vya ndani

Status
Not open for further replies.

john_thesmart

Member
Jan 20, 2022
81
277
Habari ndugu zangu, baada ya kupitia changamoto kadhaa kwenye mambo ya kazi nashukuru Mungu nimepata kazi mahali fulani na nategemea kuanza kesho.

Tatizo linakuja ni kuwa akiba kidogo niliyokuwaa nayo imeisha kwenye matumizi na kutafuta kazi.

Nimefikiria nikaongee nao hapo kazini lakini ni ofisi kubwa na watu wamenishauri nisianze kazi na kuomba omba hela hapo kazini kwani haileti picha nzuri. Kuna mtu aliniahidi nisubiri ila hadi leo hii ndio ananiambia ameshindwa kupata.

Mwenye chochote anikopeshe au anunue vitu vifuatavyo ninavyouza (nitabaki na kitanda tu) mwisho wa mwezi naamini mambo yataanza kukaa sawa.

-Meza ya jikoni (ya kuingia mtungi mdogo)
-Stand ya kuwekea viatu
-Adapter ya laptop(dell) pin ndogo, mpya
-heater ya kuchemshia maji etc.

Ndio, vyote ni vitu vidogovidogo, nahitaji nauli ya kuweza kufika kazini hizi week mbili tu.

Maelezo zaidi PM, nashindwa kuweka namba hapa maana maboss wanaweza wakakatiza huku na labda ikaniletea tabu kidogo.

Hii simu ningeuza ila ni mbovu mbovu hata kuweka picha ya vitu hapa imekataa.

Nipo Dar asanteni

=========
UPDATES

NAOMBA NIKIRI KUWEZESHWA NAULI YOTE NA MWANA JF lilykaybee SIONI KAMA ITAKUWA BUSARA KUENDELEA KUOMBA MCHANGO AU KUUZA CHOCHOTE.

Asanteni na wote mlioonyesha moyo, Mungu awabariki sana.
Dada Evelyn Salt ulisema watu wataishia kucheka tu but apparently sio wote,kuna wachache wenye moyo wa huruma. I hope kazi itaenda vizuri na nashukuru sana kwa wishes zenu.
 
Umbali wa kazini mpaka nyumbani nauli yake ngapi? Rafiki au mwana familia hakuna wa kukupa mkopo wa 30,000 mpaka 50,000?? Jaribu kuongea na HR na kumwambia uhalisia na kuomba mkopo wa nauli mpaka mwisho wa mwezi wakate kwenye mshahara wako. Kama unaishi nyumba ya kupanga baba/mama mwenye nyumba muombe mkopo hadi ukipata mshahara wako.
 
Mkuu hapo kwenye ndugu sio kiivyo kabisa, ninayemtegemea ndio huyo ananisaidia mara nyingi na alisema nisubiri ila amekwama kabisa.
 
Umbali wa kazini mpaka nyumbani nauli yake ngapi? Rafiki au mwana familia hakuna wa kukupa mkopo wa 30,000 mpaka 50,000?? Jaribu kuongea na HR na kumwambia uhalisia na kuomba mkopo wa nauli mpaka mwisho wa mwezi wakate kwenye mshahara wako. Kama unaishi nyumba ya kupanga baba/mama mwenye nyumba muombe mkopo hadi ukipata mshahara wako.
Tatizo la kazini ni kwamba ofisi gani wanakubali kutoa mkopo mtu hujakaa hata mwezi? Ingekuwa ni biashara ya mtu sawa ningeongea na boss
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom