Niliacha kazi kumsaidia aliyewahi kunisaidia na hata hatukuwahi kufahamiana kabla

Oxpower

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,143
2,999
Naamini wote mko salama, twende kwenye mada moja kwa moja.

Katika maisha haya unaweza msaidia mtu kitu kidogo bila kukuathiri wewe kwa lolote, lakini bila kujua unaweza kuwa umemsaidia pakubwa sana, twende kwenye mada sasa.

2010 nikiwa kidato cha 6 mkoani Iringa shule X, nyumbani ni Mbeya, ilitokea nimefanya kosa fulani nikarudishwa nyumbani kwa siku 21 huku nikisindikizwa na barua mbili; moja ya mzazi na nyingine ifike kwa Mkuu wa Wilaya na ipigwe muhuri wake siku narudi.

Shida haikuwa kurudishwa nyumbani, ila je, hapo nyumbani nitaingia mlango gani Mzee wangu ilikuwa fanya ujinga wote ila sio mambo ya shule. Nikikumbuka O-Level niliachwa stand mkoa wa mbali kisa suspension.

Nikapiga hesabu nikaona hapana mzee ataniua, akili ikanijia niende kwa mama mkubwa Moshi (huku Moshi tuliwahi kuishi tuna makazi hivyo napafahamu vizuri). Tatizo likaja kwenye fedha, sikuwa na fedha ya kufika Moshi ila nikaona niende huko huko maana Mbeya mzee ataniua.

Basi mapema tu nikadaka zangu Sumry ya Dar mpaka Chalinze, kufika Chalinze pale nikafika sina hata 100 na njiani sijala kitu, maana niliomba kwa 15000 Iringa to Chalinze na ndio pesa nilikua nayo.

Nimeshuka pale njaa inauma vibaya sana, kiu imenikaba sielewi kitu, nikaona nisije kufa hapa. Nilikuwa na koti moja hivi kwa enzi zile lilikua kali sana, nilinunua elfu 20 Mbeya; sasa vuta picha koti la elfu 20 mbeya mwaka 2010.

Nikanza kutafuta mteja pale, watu hata hawana mpango nalo yani,i katokea tu jamaa akasema ana 5000 nimpe, nikambembeleza aniongeze hata buku, kweli akakubali nikawa na 6000 sasa.

Nikachukua chakula cha 1500 na maji 500 nikabaki na 4000, sasa nikawa nawaza hii pesa mimi itakuaje inifikishe moshi na sina simu? Basi mida kama ya saa 10 hivi naona gari ya Mbeya-Arusha, ile imefika tu mimi nikazama ndani, nikaenda mwisho kabisa wa gari.

Gari ikanza safari, basi muda kidogo tu jamaa wakagua tiketi hawa hapa, dogo lete nauli mimi natoa 4000 jamaa akawaka sana, twende mbele ushuke.

Gari ikatembea huku tunabishana, ikafika muda sina namna, nikamuomba kama ananishusha basi anishushe kijiji chenye watu na anipe 4000 yangu maana sina hela nyingine.

Muda wote huo kuna konda alikuwa anasema huyo dogo anazingua, analeta uhuni kazini alete hela, ila sura yake haikuwa siriazi kama huyu mchukua nauli na huyu inaonesha alipandia njiani mana badae alishuka.

Basi nikaona nimfate huyo kaka, nikamwambia kaka nifikisheni Moshi, nikifika pale nipelekeni polisi mama yangu ni maarufu wale polisi watakuwa na namba zake tu au nitawapeleka nyumbani mtapata hela yenu.

Yule kaka akaona nipo serious, basi akampanga dereva huko mimi nikakaa mbele pale staff. Jama akawa ananipiga maswali ya hapa na pale basi tukawa poa nae tu, akaninunulia msosi, yaani kila muda ananiuliza nataka nini, yaani akawa ananipa attention kubwa sana.

Kiukweli nilifurahia kukaa pale, hata nilipopata siti sikwenda nikamwambia tunakaa wote hapa. Mungu mwema tukafika Moshi mida ya saa 6 usiku, kwa mama ni katani chini ya Moshi Tech. Basi jamaa akafosi nikashuke magereza pale, habari za hela akaniambia niachane nazo ila nikirudi skul nisifanye ufala tena. Kweli nikafika home safi, kilichoendelea ni story nyingine.

2014 baada ya kumaliza chuo, ajira hakuna na katika kujiongeza nikajikuta nipo kwenye magari kampuni X kutoka Mbeya to Dar kama konda ila kitengo changu ilikua hasa kugawa vyoda, biskuit na maji pia kuwakagua wakatisha tiketi na kuhakikisha hesabu ziko sawa, kifupi ndio nilikua boss humo ndani na ajira yangu ilitoka kwa mmiliki wa magari maana tulikua majirani na ananijua vizuri; kifupi nilikua chawa wake.

2015 miezi ya mwanzoni ile, acha gari zianze kuchinja watu sijui kafara za wanasiasa zile, kidogo tu Majinja imechinja watu wote changarawe Mafinga, mara Mohamed Trans Singida huko kachinja, na ajali nyingi nyingi, basi ile hali ikaleta mtafaruku na mama nyumbani akitaka niache.

Sasa nawaza niache wakati nimefungua carwash na kuna vitu kibao sijakamilisha nategemea hizo kazi ndio nipate pesa pia kuomba tenda. Mgogoro ukawa mkubwa na mimi nimekaza siachi kazi kama ni ajali zipo tu, basi mimi na bimkubwa tukawa hatupo kiivyo.

Katika harakati hizo ndipo nilikutana na konda alienisaidia kutoka Chalinze mpaka Moshi bure na msosi juu, ila nilimkuta amechoka sana ndio kwanza ana mwezi mmoja tokea aanze kuwa sarange (mpiga debe).

Story yake ilikua ndefu na ya kusikitisha ila kifupi aliachana na mambo ya magari, alipata kazi nyingine ila muda huo hakuwa na kazi na mke wake mjamzito kamrudisha kwao na yeye yupo ubungo hapo amekuwa mdago dago (dago ni watu wanalala nje).

Kiukweli niliumia sana, nikaona isiwe tabu, kwakua niko na mgogoro na bimkubwa, pia jamaa yangu anashida basi nikaona niache kazi kumpisha jamaa.

Nilienda kwa boss nikampanga vyema akapangika na nikampanga mzee aseme yule ni kijana wake pia, ilikuwa rahisi kwa mzee kwakuwa story hiyo nilimsimulia kabla kwahiyo alipomsikia tena basi akakubali kwakuwa ile safari ya mimi kwenda Moshi mzee nae ilimuingiza kwa mgogoro na mama kimtindo.

Basi jamaa akalamba ajira, kumbuka ile safari kupeleka gari Dar ni 30000, mkipiga piga na huko road tumizigo na abiria wa mchongo basi hukosi 80000 kwa siku, siku mbovu ni 50000. Yule jamaa akanza kazi, badae maisha yakatupeleka kasi tukawa tumepoteana na ile kampuni badae iliyumba kimtindo nae akaenda kwingine kisha hatukuonana tena.

2023 mwezi huu wa 3, uso kwa uso na huyu jamaa ndani ya mji wa Masasi. Mimi sikumtambua kwakuwa sasa hivi ana mwili kimtindo, cha ajabu tukajikuta tumekumbatiana hadi machozi, nilikua na safari zangu ikabidi nigairi nimsubiri. Sasa hivi ameshakuwa dereva wa malory ya nje wenyewe wanaita transit.

NB: Tukipata nafasi ya kusaidia tumsaidie mtu yeyote bila kujali, maisha haya ni fumbo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namini wote mko salama,twende kwenye mada moja kwa moja


Katika maisha haya unaweza msaidia mtu kitu kidogo bila kukuathiri wewe kwa lolote,lakini bila kujua unaweza kuwa umemsaidia pakubwa sana.twende kwenye mada sasa

2010 nikiwa kidato cha 6 mkoani iringa shule X.nyumbani ni Mbeya ,ilitokea nimefanya kosa fulani nikarudishwa nyumbani
Muhimu sana kusaidiana, na ndiyo dini yenyewe
 
Daah nimejikuta nakuwa emotional ghafla na machozi yananilenga, hongera Sana Kwa moyo mzuri na huruma.

Ndio maana tunaambiwa tutende Wema siku zote kwani hatujui ni wapi na Nani atatusaidia
Kweli mkuu,hivi na ile 4000 ningefanya nn ifae,na yeye katika hali ile alifikia kulala nje mana hakuweza kulipa kodi tena,kweli wema ni akiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom