Nimepata Barua ya uhamisho ndani ya miaka 2 kazini

Nimepata Barua ya uhamisho ndani ya miaka 2 kazini

Mkuu ninakoenda si kuzuri kila ninaemuambia ananikatisha tamaa, kikubwa hakuna amani,

wanajeshi wa JWTZ muda wote na RPG na kihistoria mji huo miaka kadhaa nyuma ilishambuliwa na watu wenye itikadi kali za kidini, wamewapa jina la alshababi. Waliua, kuharibu mali na kuteka watu hadi leo hawajulikani walipo.
Kibiti pazuri nenda tu!!
 
Acha kejeli wewe hapo story ingekuw fupi atoe barua jf na ushauri kuusu uhamisho , wote tusipo kuwa walimu nan atakuwa mwalimu bila mchango wa mwalimu ungefik ulipo
Li ticha lisha panic, saidia liticha lenzako linajikaanga lenyewe muda sio mrefu tutaskia wameshalila kichwa.
 
Shukrani kwa mawazo yako,
Msimamo wangu ni kwamba sikatai uhamisho,
hadi kufikia J3 naenda kuripoti kisha narudi kituoni hapo ndo sibanduki bila pesa.
Mkuu viongozi aliowateua Rais Samia wanamdharau sana. Malimbikizo ya madeni ya uhamisho ni mengi mno na anayeamua kutofanya hivyo ni wakurugenzi. Inasikitisha mno
 
Toa hiyo barua mdogo wangu hiyo kazi uliomishwa unaweza ukaikosa hakuna ulichoficha hapo na umesema umepelekwa mji wenye mapigano Sjui nini sikiliza Ushauri wa wenzio
Huyu atakuwa kapelekwa KITAYA huko mpakani karibu na Msumbiji..
But hajui tu, maelezo yake yanasaidia kabisa mtu kufahamu ni mwalimu wa shule gani/Halmashauri gani na anapelekwa wapi.. Offcoz Hilo jina la Mkurugenzi aliloliacha ndio Kisanga
 
Huyu jamaa amefanyiwa uhamisho wa Ndani ya Halmashauri, kutoka Shule Moja kwenda nyingine Ndani ya Halmashauri. Ninachojua huo uhamisho utagharamiwa na DED mwenyewe kupitia OC za Idara ya Elimu(P/S) anayofanyia kazi mdau.

Nimewahi kuzunguka huko nilipokuwa nafanya biashara ya kununua Korosho, kwahiyo probably jamaa atakuwa amehamishwa kupelekwa maeneo ya Kitaya au Kilimahewa. Ingawa Nina Uhakika itakuwa Kitaya ndiyo ilikumbwa na machafuko ya kushambuliwa na Magaidi. Ingawa Ulinzi umeimarishwa saivi kuanzia Kitaya-Kilimahewa-Mnongodi-hadi Kitama I &II.

Kila la kheri Mkuu, Pesa yako ya Uhamisho utalipwa ingawa kwa kuchelewa kutegemeana na OC inavyokuja.

Mwanaume hachagui kazi, tuendelee kupambana.
 
Huyu atakuwa kapelekwa KITAYA huko mpakani karibu na Msumbiji..
But hajui tu, maelezo yake yanasaidia kabisa mtu kufahamu ni mwalimu wa shule gani/Halmashauri gani na anapelekwa wapi.. Offcoz Hilo jina la Mkurugenzi aliloliacha ndio Kisanga
Kitaya mbona kuko poa Tu...

Maisha safi japo mtandao hamna kuna Ttcl tu.
 
Komaa waifute,sio muda utakuta screen shot za hiyo barua yako kwenye magroup ya hapo halmashauri kwenu
Huyu ticha pimbi kashajichanganya,

Watu wanamshauri yy anajifanya mjuaji, ngoja watembee nae

Kale kamradi kake ka pool table karibu na bar ndio kanampa jeuri ya kutaka kukataa uhamisho,

Sasa subiri wakutoe mazima ili ukasimamie kamradi kako vizuri[emoji3061]
 
Back
Top Bottom