1. Nimeonja pendo lako,
nimejua u mwema
Nitakushukuru
nitawainua wote wakusifu
wewe
Nitawaongoza wote waimbe
kwa furaha
Nitakushukuru
nitawainua wote wakusifu
wewe
Ukarimu wako ee Bwana,
na huruma yako wewe
Msamaha wako ee Bwana,
na upole wako wewe
Umenitendea wema
usiopimika
Nitakushukuru
nitawainua wote wakusifu
wewe.
2. Kina mama simameni, piga
vigelegele -
Kina baba nyanyukeni,
mkapige makofi -
3. Watu wote nesanesa,
chezeni kwa furaha -
Inua mikono juu,
mshangilieni Bwana -
4. Watawa washangilie,
makasisi waimbe -
Walei warukeruke, waseme
aleluya -
5. Vitambaa mikononi,
vipeperushwe juu -
Na vichwa viyumbeyumbe,
kwa mwendo wa kuringa -
6. Nitakushukuru mimi, na
nyumba yangu yote -
Nitayatangaza haya, maisha
yangu yote -