Nimeona shughuli kidongo chekundu' ni mambo ya id el hajj?

Jahom

JF-Expert Member
Aug 26, 2008
351
32
Inawezekana leo ni Eid El hajj kwa wengine? Nimeona Kanzu nyeupe na Baragashia zake nyingi sana na hijab kwa pembeni. Mi najua ni kesho, kulikoni? Mniwie radhi kama sitaeleweka kwa maana nzuri.
 
Ni kweli wanazuoni waandamizi wanasema shughuli (Eid) ni leo na kwamba BAKWATA wamechemsha
 
Wanazuoni Waandamizi hawamo ndani ya Bakwata? NI vema wakaunda Summit nyingine itayokuwa inatoa msimamo penye utata na kuruhusu kufanya marekebisho ya matukio ya namna hii ambayo yalianza kabla ya kugundulika kwa kalenda tunayotumia sasa, iwe ya Kimisri au ya Kiarabu(????) na kujenga uhakika zaidi. Vinginevyo hata kwenda Mbinguni itategemea kuandama kwa mwezi.
 
Bakwata wanasema eid kesho ila kuna watu wamekomaa wanasema leo sasa bakwata imekuwa chama cha siasa?i guess ndo wasimamizi wakuu wa misingi ya dini how come wanatofautiana na wengine au kuna miezi miwili?
 
Bila shaka BAKWATA wanamsubiri mkuu wa nchi Dr JK kurudi nchini kutoka Jamaica.
na ahudhurie baraza la eid kesho huko Dar.

Tuombe nae asipigwe vibao.
 
Eid ni leo na wenye kusali wameshasali...hao bakwata sijui wako dunia gani? boring
 
Dogo mbona unataka kulianzisha!! tehe tehe.
Nimewidhidroo .......... Ila sijaelewa vitu vifuatavyo... NAOMBA ANAYEFAHAMU ANIELEWESHE

1. Kwa nini baadhi ya sherehe za kiislamu (kama si zote) zinategemea kuandama kwa mwezi...????
2. Nilitegemea nchi zilizo mbali sana na nyingine kijiografia ndo zipishane katika kusheherekea sikukuu hizo......... Nashangaa kwa nini ndani ya nchi moja kunatofauti ya siku nzima...????
3. Huku kutofautiana kupo tanzania tu anza dunia nzima...????
 
NAOMBA ANAYEFAHAMU ANIELEWESHE

1. Kwa nini baadhi ya sherehe za kiislamu (kama si zote) zinategemea kuandama kwa mwezi...????
2. Nilitegemea nchi zilizo mbali sana na nyingine kijiografia ndo zipishane katika kusheherekea sikukuu hizo......... Nashangaa kwa nini ndani ya nchi moja kunatofauti ya siku nzima...????
3. Huku kutofautiana kupo tanzania tu anza dunia nzima...????[/
QUOTE]

Sherehe zote za kiislamu zinategemea kuandama ka mwezi. Hiyo inatokana na kalenda ya kiislam inachua reference yyake kutokana na mzunguko wa mwezi.

Kutokana na somo la geografia tunaeleza kuwa Dunia inalizunguka jua. Na Mwezi unaizunguka dunia. Sasa utaona kabla ya hii technologia mpya ya kisasa watu wa zamani walitumia njia hii ya mzunguko wa Mwezi katika kuweka kumbukumbu zao. Sasa utaona sherehe zote za kiislamu zimewekwa kufatana na mwandamo wa mwezi.

2. Waislam wanatofautiana katika mwandamo wa mwezi kutokana na tafsiri halisi ya mapokeo ya hadithi mbalimbali zilizotokana na wale waliofanya jitihada katika kuzitafsiri hizo hadithi.
Mfano wa mfungo wa mwezi wa ramadhani. Hadithi imesema mfunge pale mtakapo uona mwezi. lakini hadithi hii haikueka mipaka kuwa popote ukionekana tufunge au sehemu fulani wakiona tufunge.
Sasa waliofanya jitihada katika kuelewa hili wamebainisha wazi na matokea yake kuna MWEZI A KIMATAIFA na MWEZI WA ZONE. anaofata mwezi wa kimataifa watafunga pale sehemu yoyote ukionekana mwezi wanafunga. Na wale wa mwezi wa zone watafunga pale ambapo nchi wanazoshirikiana nao kuona mwezi ukionekana wanafunga.

Kifupi hiyo ni tofauti ya ueleo wa hadithi lakini zote ni sawa.

Huko kutofautiana kupo Dunia nzima. lakini nchi nyingi sana zina mamlaka maalum za kutangaza mwandamo wa mwezi .

nafikiri nimejitahidi kukujibu.

Dr Hamza
 
Back
Top Bottom