Nimeona magari ya mpaka $700 Befoward, je kweli ni bei yake?

Wasudi

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
226
223
Habari wana jamvi, naulizia wanajamvi nimeingia mtandaoni pale be foward nimeona magari hadi dola 700 na chini ya hapo kweli ndio bei zake na vipi inaweza kukugharimu ngapi hadi zikanyage ardhi ya magu?
 
Ndio hiyo ni bei ya manunuzi - FOB, na kimsingi zipo hadi gari za dola 200,

Ila ghalama ya manunuzi na kuifikisha bandari ya salama TZ - Yaani CIF huwa ni kubwa

Ungeweka link ungepata mchanganuo kamili.

Pia ni vyema hiyo gari husika ukaangalia ghalama zake za TRA hapa: USED MOTOR VEHICLE VALUATION CALCULATOR

Hivyo tatizo liko kwenye gharama za TRA na CIF
 
Ahsante mkuu umenifungua sana je kwa uzoefu wako kwa bei hii nikiwa na million 7 inakuwa yangu?
 
Haiwezekani kusema inatosha au haitoshi bila kujua aina ya gari.

Andika ref number ya hiyo gari hapa - Angalia kwenye picha utaona kama hii.
upload_2017-4-19_19-26-24.png

Ndipo utapata hesabu sahihi.
 
Ndio hiyo ni bei ya manunuzi - FOB, na kimsingi zipo hadi gari za dola 200,

Ila ghalama ya manunuzi na kuifikisha bandari ya salama TZ - Yaani CIF huwa ni kubwa

Ungeweka link ungepata mchanganuo kamili.

Pia ni vyema hiyo gari husika ukaangalia ghalama zake za TRA hapa: USED MOTOR VEHICLE VALUATION CALCULATOR

Hivyo tatizo liko kwenye gharama za TRA na CIF
Mkuu nipe ufafanuz madhut wa hiz incoterm mbili FOB na CIF yaani Free on board na Cost insurance Freight jinsi zinavyo husika na ununuaji wa vitu overseas. Thou nimesha zisoma chuo kwenye Module ya international logistics na comercial aspects still i need emulation and real applications of such incoterms
Nawasilisha.............!
 
Kwa ufupi, FOB ni bei ya bidhaa (gari in this case) tu, bila gharama za kulisafirisha, ukaguzi, na bima. CIF inajumuisha vyote hivyo. Unakuta gari FOB ni dola 200, freight dola 800, inspection dola 250, insurance dola 100, ukijumlisha vyote ndio unapata CIF ambayo ndio unatakiwa kuzingatia.
 
Kuwa makini sana. Mengi ya bei hizo huwa yameoza kabisa(literally!).

Kama ukiamua kununua hakikisha limefanyiwa ukaguzi na ku pass kule Japan (kuna gharama huwa inaongezeka kidogo ya huo ukaguzi). Usipofanya hivyo TBS watalikataa hapa Tz au ukajikuta unatoa pesa zaidi (kuhonga!) ili kulipitisha.
 
Afadhali umesema,

Maana nimeogopa kusema mie.

Ni kweli kabisa ulichosema!
 
Back
Top Bottom