Je, ni kweli Mahindi yameshuka bei?

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
Kutokana na Taarifa ya hapo chini kutoka Azam Tv:

KUSHUKA KWA BEI YA MAHINDI, NINI SABABU NA KIFANYIKE?: Hoja ya kuporomoka kwa bei ya mahindi nchini imetinga kwa mara nyingine bungeni baada ya Mbunge wa Mbozi, George Mwanisongole kutaka Bunge liahirishe shughuli zake ili lijadili suala hilo huku wakulima wa zao hilo nao wakipaza sauti zao juu hali ilivyo katika biashara hiyo ya mahindi.

Wakati malalamiko hayo yakijiri Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameendelea kusisitiza kwa wakulima kuwa hakuna zuio la uuzwaji wa mahindi nje ya nchi kwa mfanyabiashara mwenye vibali vyote na hadi jana vimetolewa vibali vya zaidi ya tani 20,000 za mahindi na unga wa mahindi tani 15,000 huku bei elekezi ya mahindi ikiwa ni shilingi 800 kwa kilo maeneo ya mjini huku kwa maeneo ya pembezoni ni shilingi 600.

Je ni kweli mahindi yameshuka bei?
Mbona huku niliko naona bei bado iko juu na ni neema kwa wakulima

Vipi huko uliko mahindi ni bei gani?
 
Daah yameshuka mkuu yaani kilo sh 500 kwa hapa nilipo ni hasara tupu wakati mwezi wa tano ilikuwa 850
 
Na yanaenda kupanda geita tunalima mara mbili mahindi saiv tunalima tunauza bei 80000 lakini kufukia mwezi ujao walanguzi watakuwa wamekwisha maliza kazi yao ya kulangua
 
Back
Top Bottom