Nimeona jina leo la mkopo na chuo sijaenda

tzhumoally

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
412
156
Wakuu naomba mnisaidie, mimi nimechaguliwa bachelor ya statistics UDOM lakini nilishindwa kwenda kwa sababu nilikosa mkopo batch zote zilizotoka.

Sasa leo naingia katika account yangu nimeona nimepata mkopo,nsasa naomba ushauri nifanyeje sasa hivi, nikienda UDOM watakubali nighairishe ili nije nianze mwakani?

Msaada kwa mwenye uelewa.
 
Tafta mtu aliyeko udom mwambie afanye juu chini apate number za dean of students the wasiliana naye mweleze kila kitu kilivo utapata ufafanuzi mzuri
 
Tafta mtu aliyeko udom mwambie afanye juu chini apate number za dean of students the wasiliana naye mweleze kila kitu kilivo utapata ufafanuzi mzuri
Nilitaka niende kesho physically..lakin naogopa kuja kupoteza nauli yangu wakanitimua
 
Kuendelea na chuo sidhani kama inawezekana maana umechelewa sana kujisajili, kujiridhisha nenda chuoni kaombe utaratibu wa wao kukusaidia kuahirisha mwaka.
 
Wakuu ahsanteni sana kwa mawazo yenu..jamaa wamekubali nifanye registration
 
Nenda karipoti chuo haraka sana, miezi 2 uliyochelewa sio tija kama uko seriuos na shule yako usipoteze muda tena fanya hima ufikie lengo lako na hakikisha bodi ya mikopo unawasiliana nao
 
Nenda karipoti chuo haraka sana, miezi 2 uliyochelewa sio tija kama uko seriuos na shule yako usipoteze muda tena fanya hima ufikie lengo lako na hakikisha bodi ya mikopo unawasiliana nao
Sawa mkuu nitafanya hivyo,nilipofika kwa mhasibu ameangalia katika system amesema hela hazijarudi just nilipie necessary fees jumatatu nianze kusoma..shukran sana
 
Sawa mkuu nitafanya hivyo,nilipofika kwa mhasibu ameangalia katika system amesema hela hazijarudi just nilipie necessary fees jumatatu nianze kusoma..shukran sana
Nakutakia masomo mema, jiwekee malengo yanayotekelezeka, usikubali kurudishwa nyuma, ratiba na kuiitii ndio ukombozi wako uliobaki. Mtegemee Mungu zaidi.
 
Wakuu naomba mnisaidie,mimi nimechaguliwa bachelor ya statistics UDOM lakin nilishindwa kwenda kwa sababu nilikosa mkopo batch zote zilizotoka.

Sasa leo naingia katika account yng nimeona nimepata mkopo,sasa naomba ushauri nifanyeje sahivi,nikienda UDOM watakubali nighairishe ili nije nianze mwakani?

Msaada kwa mwenye uelewa.
Nenda loan bord kasitushe mkopo
 
Back
Top Bottom