Peleka polisi man. Niliokota wallet ina IDs kibao za mtu mmoja, nikaona ya ofisini kwake DIT. Hapo nimeokota Chang'ombe kule.
Kwakua nilikua na trip ya posta iyo siku, nikajifanya mwema nikaenda nacho DIT walinzi nikawavuka bila kuwaambia ila nilivoenda mapokezi nikawaambia. Nikawekwa sehemu akaja HR nikawa naongea nae.
Aisee kumbe jamaa alivamiwa jana yake alivokua anarudi kutoka kazini. Kaibiwa ibiwa ye yupo hospital.
Sema HR alikua muelewa, ila nikaacha taarifa zangu. Owner alikuja akanitafuta akiwa na polisi aone kama atanitambua ni moja ya watu niliomuattack, alivoniona tu akasema hapana uyu mrefu sana walikua wafupi. Nikasema dah. Wema huu.