Nimenyimwa hati ya kusafiria kisa mi ni wa Kigoma

shida ni nini? au mfanano wa majina. unakuta mtanzania anaitwa NIYONZIMA, hapo kwa watu wa uhamiaji lazima watake jicho la pili. though sioni shida, hata uraia nchi mbili kwangu nisingekuwa na shida.
Kiukweli bro inanimate Sana,Yani kusema kweli Kigoma Ni kama tulisha laaniwa
 
Mughabo Kama maombi hayakusaidii jiongeze toa rushwa. Bongo kila kitu kinawezekana hata mhuri original wa Ikulu unapata ukirefusha mkono.
 
Shida ilianzia hapo kwenye"Mimi ni muha original" kama hujui waha Wana kiulizo kwenye ofisi za uhamiaji na hiyo kutokana na jinsi warundi wanavyo ingia kigoma usiku na mchana, na kibaya zaidi wote mnaongea lugha moja tofauti baadhi ya matamshi tuu, na hao ndugu zenu warundi wakisha kaa kigoma miezi miwili tuu wanaanza kujiita waha, hao waha wakienda hata kufatilia namba za nida Wana nyooshwa kisawa sawa
Kwa hyo maoni yako ni yapi,Nipe mbinu basi wanirudishie pesa zangu
 
Mughabo Kama maombi hayakusaidii jiongeze toa rushwa. Bongo kila kitu kinawezekana hata mhuri original wa Ikulu unapata ukirefusha mkono.
Yeah ni kweli ila sasa km nimetoa zaid ya 3K huoni bado tu nimejiongeza, Anyway'Ulakoze
 
Habari zenu wadau.
Ninayo masikitiko makubwa sana kuona nimenyimwa hati ya kusafiria) Passport)Kisa mimi ni mzaliwa WA Kigoma!!
Picha ilianza hivi:Mimi Ni kijana mwenye umuri WA miaka 37,Babu na mababu zangu wote mzaa baba na mama wote ni wazaliwa wa wilaya moja wapo ktk mkoa wa kigoma,Kwa kifupi mimi ni muha original,mnamo mwaka 1990 wazazi wangu walihamia mkoa wa kagera wilaya ya Ngara,Na huko ndiko niliko patia Elimu yangu ya shule ya msingi na Secondary pia,

Km tunavyo jua ili upate passport kuna vigezo unatakiwa kuwa navyo,
Mimi nilipata mwaliko WA kwenda Norway kwa ajili ya Kuhibiri injili,Hivyo nikatumiwa barua ya mwaliko,kwenye mwaliko huo gharama zangu ilikus ni kupata passport tu na mambo mengine madogo madogo,

Wenyeji wangu walikuwa wapo tayari kulipia gharama zote za usafiri NK.

Baada ya hapo nilianza kuchukua hatua za kupata hyo nyaraka muhim,Kwa bahati nzuri kila kilicho hitajika nilikuwa nacho,
Nilijaza form online ile ya kuomba pass kisha nikaipeleka ofis za uhamiaji,

Pale zilikaguliwa zikaonekana zote zipo sahihi,Nikapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole kisha nikaondoka,
Baada ya Mwezi mmoja niliitwa tena ofisi za uhamiaji "Eti nihojiwe maana imeonekana kwamba huenda Mimi sio mtanzania,Nilifika pale nikajaza taarifa zote wanazo hitaji,
Cha ajabu Leo ni miezi 5 imepita sipewi haki yangu,
Na gharama zote nimetumia zaid ya Lack 2 ,Swali langu nifanyeje ili wanirudishie gharama zangu?
Jiongeze!

Huyo AFISA ungepenyeza rupia tu mkuu!

Amekuomba Rushwa KIAKILI hujamwelewa!

Ndivyo walivyo!!
 
Back
Top Bottom