Jicholamwewe
JF-Expert Member
- Jan 2, 2021
- 307
- 348
Waheshimiwa, habari ya kazi na pole kwa majukumu.
Waheshimiwa, mwaka jana 2023, nilibahatika kupata ufadhili wa kwenda masomoni nje ya nchi hivyo nililazimika kutafuta passport. May 2023, nilifika ofisi za uhamiaji Kurasini na viambatanisho vyangu vyote kufanya ombi la passport. Nilifanikiwa kukamilisha ombi langu na kulipia gharama zote.
Waheshimiwa, toka May 2023, hadi sasa sijapata passport. Nilipojaribu kufatilia niliambiwa siwezi kupata passport kwa sababu mimi sio Mtanzania.
Waheshimiwa, mimi nimezaliwa, kukua na kusoma ndani ya mipaka ya Tanzania kama viambatanisho vyangu vinavyoonyesha. Wazazi pamoja na babu zangu ni watanzania.
Waheshimiwa, nimefanya jitihada zote pamoja na kuleta wazazi kutoka kijijini na kwenda nao uhamiaji bila mafanikio. Nimeingia gharama kubwa sana kufuatilia hili swala ukizingatia mimi ni kijana niliyemaliza chuo na bado sijabahatika kupata kazi. Kadhalika kuna uwezekano nikapoteza ufadhili niliobahatika kuupata kama sitapata passport kwa wakati; ndoto na maisha yangu kiujumla yataharibika kwani elimu ndio tegemeo langu kujikwamua kiuchumi.
Waheshimiwa nimekuwa ni MTU wa mawazo sana pamoja na misongo. Naombeni msaada wenu kutokomeza ukosefu wa haki katika nchi hii.
Ni mimi kijana mwenzenu Mwenyezi Mungu awabariki mnapoendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa.