Nimenunua soda chafu.wapi nianzie kuishtaki kampuni?

tizo1

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
856
145
Jamani leo nimenunua soda ndani yake nimekuta mabaki ya mshumaa.wapi nianzie kuishaki coca cola tanzania?msaada nimechukha sana kwani nilinunua klet nying na soda 1 ndo nimekuta ina uchafu
 
Jamani leo nimenunua soda ndani yake nimekuta mabaki ya mshumaa.wapi nianzie kuishaki coca cola tanzania?msaada nimechukha sana kwani nilinunua klet nying na soda 1 ndo nimekuta ina uchafu

ili upate fidia ya kisheria (redress) sharti kwanza uthibitishe kwamba umeathirika kwa tukio hilo. Kama umeona tu kipande cha mshumaa, so what. Ingekuwa tofauti kama ungemeza huo uchafu (bila kujua) na matokeo yake ukapata madhara fulani. Lakini hivyo ilivyo, the most u can get ni kubadilishiwa hiyo soda na oral apology kutoka coca cola!
 
Na uzembe wako je?, unanaunua kitu kichafu, unasepa nacho home, unarudi kudai fidia baadae?!.
 
Jamani leo nimenunua soda ndani yake nimekuta mabaki ya mshumaa.wapi nianzie kuishaki coca cola tanzania?msaada nimechukha sana kwani nilinunua klet nying na soda 1 ndo nimekuta ina uchafu
mkuu labda glass uliotumia ndio ilikuwa chafu
 
Du pole sana bado watu mnakunywa soda? wakati matunda Tanzania yako mengi na yanaozeana kila kona.
 
Kitu kama hicho nlishakuta kama mara mbili,nyeupe kama kipande kidogo cha ugali!since then,sitaki tena soda.
 
Kama umedhamiria kushitaki mtafute wakili yeyote aliye jirani mtake akupe
ushauri kwanza kuhusu nafasi zako za kufanikiwa kesi akikuambia kuwa ushahidi
unatosha ingia vitani...ila haitakuwa vita rahisi maana unapambana na deep pocket
 
Ulikunywa au ulishtukia kabla ya kunywa?. Ingia kwenye mtandao, soma kesi inayofanana na hiyo ya Donoghue v Stevenson.
 
Mze unataka umalizie shida zako hapo? Ni zali la mentali nini? Chuna bana kwani wewe hukosei?
 
Mimi ninayo na sijaifungua, nangojea tu
siku moja najua nitakwaa bingo tu mkuu,
nikimpata hata mtikila namuuzia yeye aende
nayo mbele.
 
  • Thanks
Reactions: RR
ili upate fidia ya kisheria (redress) sharti kwanza uthibitishe kwamba umeathirika kwa tukio hilo. Kama umeona tu kipande cha mshumaa, so what. Ingekuwa tofauti kama ungemeza huo uchafu (bila kujua) na matokeo yake ukapata madhara fulani. Lakini hivyo ilivyo, the most u can get ni kubadilishiwa hiyo soda na oral apology kutoka coca cola!

Angalia kesi ya Donoghue v Stevenson - itakupa mwanga kidogo, from there you can build your case, I guess
 
Ni ngumu kuprove kama umeshaifungua, hapo utakutwa na contributory negligence.
Soda iliyo kwenye chupa nyeupe isiyo opaque ni rahisi kuona uchafu, unaweza usipate kitu labda ingekuwa bia, hata hivyo unabidi uthibitishe umeathirika kwa namna moja au ingine kama kiafya otherwise uwe na soda nyingi chafu uwapeleke TFDA! Ila ndo ufahamu ni ngumu wewe kupata kitu hapo.
Kuna jamaa hapo juu kaongea kitu safi sana.
Otherwise tafuta a good counsel in Tort actions akushauri. Usijepoteza muda wako bure na soda yako, we wambie wakupe ingine we kunywa zako bana kata kiu.
Makampuni ya vinywaji nayo yanasheria inayowalinda mkuu, its tough mpaka uprove damage on your part.
 
Hata hivyo siku hizo chupa zenye mishumaa ndani cocacola wanazikataa. Mie nina duka la vinywaji nafahamu hilo.
 
Mimi ninayo na sijaifungua, nangojea tu
siku moja najua nitakwaa bingo tu mkuu,
nikimpata hata mtikila namuuzia yeye aende
nayo mbele.

Mamdenyi peleka wakubadilishie soda ukate kiu, kumbe umeshaona uchafu unakaa nayo ya nini?
Yani ndo maana kinywaji kisicho kwenye chupa ya opaque ni ngumu kupeleka a suit then upate damages, pia itabidi uprove kama umepata madhara kitu ambacho kitakushinda.
We wapelekee mmalizane kuna sheria inawatetea pia ndugu.
negligence suits zipo very complicated kwa mtu wa kawaida kuelewa, hapo hakuna mapene we peleka wakubadilishie, unless unamsubiria mtikila wakati hata yeye huwa anaenda kupeleka kesi zisizohusisha kupata malipo fulani yeye tunamuheshimu kwa kupenda haki. Kesi zake ni za muhimu sana katika mabadiliko ya sheria ila hapa kwa mambo ya industrial negligence tunatumia sheria za common law and principles of equity za uingereza kwa hiyo ni ngumu kubadili msimamo ulivyo.
Kata kiu mkuu.
 
Back
Top Bottom