Nimenunua home theater LHD657 Model, lakini cha ajabu ina Sauti ya kawaida sana

Ni kampuni ya LG. Kuna maandishi yanasomeka lhd657 january 2023. Nimeifunga ndani kwangu cha ajabu inazidiwa mkito na hizi sabufa za kichina spiano

Nimeinunua 700k. Pesa yangu inaniuma sana kwa hiki nilichokutana nacho

Nimeagiza mwanza sijafata mwenyewe. Je, hii sio fake kweli wakuu?
wengi huwa wanakosea hasa kwa kununua HT kwa ajili ya kupata sound kubwa ya mziki.

Home HT zimetengenezwa maalum kwa ajili ya kucheki movie's kwa maana ukiipata og na kipindi kama hichi cha mvua unapata ladha kama vile upo lwenye movie kwa mfano ni kama vile unaskiliza music au movie kupitia earphone og

ila kama utataka kupata kupata sauti kubwa ongeza zile tower speaker
 
Lazima ni settings tu,zina namna yake.Me yangu ni ndogo but ni balaa. Ila awali nilikosea settings sikuielewa.Nilipata fundi akaunganisha vizuri speakers level na sound effect ikaanza kukita mchujo na sauti ya maana
 
Hukuzingatia stabilizer, mi sikutaka kukosea kabisa maana connection ya umeme, mzik, friji na TV vinatokana na soketi 1, niligharamika kununua stabilizer mapema sana

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Tatizo halikuwa umeme. Muda mwingi nilikuwa sijaitumia hiyo radio. Siku nataka kuiwasha nikaichomeka vizuri tu kwenye umeme vifaa vingine kama tv vimeunganishwa vyote kwenye stabilizer. Lakini radio ikagoma kuwaka. Mimi niko mkoani. Nikaisafirisha hadi dar kwa hao LG. Kitu cha Kwanza kufungua tu 30 pale. Kukagua sijui what what 20 pale. Kifaa ndio nikaambiwa laki 3+ na kitu. Wakati radio ni laki 5+
 
Ni kampuni ya LG. Kuna maandishi yanasomeka lhd657 january 2023. Nimeifunga ndani kwangu cha ajabu inazidiwa mkito na hizi sabufa za kichina spiano

Nimeinunua 700k. Pesa yangu inaniuma sana kwa hiki nilichokutana nacho

Nimeagiza mwanza sijafata mwenyewe. Je, hii sio fake kweli wakuu?
Huo ndo mziki sasa achana na makelele ya seapiano na aborder
 
Naona JBL wana speaker nzuri ila kama unapenda masauti makali nunua hata zile towers mbili kubwa za aborder hutakaa usikilizie hadi mwisho
 
Uwingi wa spika sio ukubwa wa sauti na wala ukubwa wa watts wa redio sio ukubwa wa sauti.
Sauti ambayo inarekodiwa na wanamuziki ni stereo kwa maana ina njia mbili mithili ya masikio yetu yalivyo.Radio ambazo ni home theater sio kwa ajili ya kusikilizia muziki ila ni kwa ajili ya kutazamia muvi mana kwenye muvi kila spika moja hupewa sauti maalumu kwa mfano kuna spika zinatoa sauti ya mazungumzo tu, kuna ambazo zinatoa sauti ya effect za kwenye muvi, kuna ambazo zinatoa sauti ya saund track na mambo mengine mengi na ndio maana ukizitumia kwenye mziki sauti haziwi kubwa sana kwa sababu spika ambazo zinafanya kazi huwa ni tatu tu( 2.1)spika moja ya kulia, moja ya kushoto na subwoofer.
Kitu kingine ni kwamba nguvu ya spika haipimwi kwa watt.Watt inaonyesha kiwango cha umeme ambao redio itatumia kwa muda fulani.Kiwango cha sauti kinapimwa na SPL yaani Sound pressure level.
Kadri Spl inavyokuwa kubwa ndo sauti nayo inakuwa kubwa. Kwahiyo redio kubwa ambayo ina watt kubwa na spl ndogo inazidiwa mdundo na radio ndogo ambayo inawatt ndogo ila spl kubwa.Kama shida yako ni sauti basi zingatia spl ila kama shida yako ni kujua redio inakula umeme kiasi gani basi zingatia watt.
Hiyo spl unaipata wapi?
 
Hizi radio nyingi huwa ni issue ya setting, cheza na remote vizuri, cheki bass, check noise, mwisho cheki connection za waya kama zipo sawa.
Kuna rafiki yangu mmoja alinunua subwofer la aina ya Seapiano, akiwasha inaongea kama sauti ya simu ya kitochi, nikakutanaye naye yupo kwenye bajaji ameibeba nairudisha.

Nikamwambia rudisha radio nyumbani, kisha nikamwambia aunganishe kama alivyounganisha mwanzo. Kwanza kule nyuma zile speaker alikosea kuunganisha, nikaweka sawa. pia ukiangalia kwenye remote especial ya Seapiano sijui kwa LG, kuna sehemu ya bass imeandikwa - na +, bonyeza + mpaka mwisho. Nenda sehemu ya noise weka on, kuna sehemu nyingine tena ina alama za - na + ponyeza plus usikilize mdundo utakao toka.

Hizi radio zimekuwa designed unaweza kata kabisa bass ikawa stereo tupo na hiyo hiyo ukaweka busy na usiamini kama hiyo ni radio ile ile.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom