Nimenunua home theater LHD657 Model, lakini cha ajabu ina Sauti ya kawaida sana

Ni kampuni ya LG. Kuna maandishi yanasomeka lhd657 january 2023. Nimeifunga ndani kwangu cha ajabu inazidiwa mkito na hizi sabufa za kichina spiano

Nimeinunua 700k. Pesa yangu inaniuma sana kwa hiki nilichokutana nacho

Nimeagiza mwanza sijafata mwenyewe. Je, hii sio fake kweli wakuu?
Unaponunua hizi Home T

Ukitaka kununua hizi Home Theatre au Sound Bar zingatia WATTS..kwa LG nunua angalau kuanzia WATTS 1000W..hiyo yako itakua ni 330W so hakuna kitu...pia Sea Piano ni Subwoofer moja imetulia sana tatizo tu brand yao ila ni mziki wake uko poa sana
 
Kwa upande wa sound hadi sasa Sony ndio naona anafanya vizuri sana....
Hakuna kitu hapo nilikuwaga nayo kwa mwaka mmoja tu nikauza kwa hasara.

LHD 756 LG Home theater ni baba lao kwa ladha, nikifunguliaga volume 16 tu huwa naburudika sana, kuna siku niliijaribu volume 28 hadi Watu kadhaa walikuja kuuliza kuna sherehe waje kubanjuka?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kama ulitaka mziki, nenda na music system sio home theatre, home theatre is for surround sound kama dt dobbie nk ambazo utaskia souti ya movies vzr kwanye hizo channel 5 za sauti, hakuna mziki una channel 5, mziki ni sterio ya channel 2 tu.

Ukitaka mziki, chukua music system hii, andaa milioni zako kadhaa
Unaitwaje unapatokanaje bei yake ipoje hapa na huko nje?
 
Kuna kitu watu mnachanganya! Home Theater haijaundwa kwaajili ya heavy sound! Hiyo ni kwa kiswahili chepesi ni (Kitoa sauti) tu. Home theater haiwezi kushindana na Subwoofer kwasababu muundo wa coil zake speaker zake ni tofauti kabisa. Ingawa zote zinaathiriwa na Watts zake. Kama unataka mziki wa maana hakikisha Unanunua Hi-Fi System au Subwoofer yenye kuanzia watts 600. Home theater hata ikiwa na Watts 1000 hawezi kushindana na Subwoofer ya watts 400 au Hi-Fi ya watts 500.

Zingatia. Hi-Fi -> Woofer -> Home Theater
 
mkuu mpaka natoa hiyo hela nilitaka kitu kizuri kisicho na bla bla
Kaka hujapigwa angalia WATTS zake bila shaka ni 330W ndo uwezo wake..so kachukue kubwa yake yenye 1000W halafu rudi hapa na thread ya ushuhuda hapa
 
Nina uhakika na ninachoandika..niliwahi kununua LG 330W sikuielewa kabisa..niliuza nikanunua LG 1000W naenjoy mziki wa maana..na pia zinapendeza sana ukiziweka sebuleni..sipendagi kuandika kitu nisichokijua kama wewe unabisha upumbavu huku unatumia sabufa ya ALITOP
 
LG sitaki kuwasikia kabisa. Nilinunua LG radio mzigo. Lakini baada ya miezi 9 kiliharibika kifaa kinahusika na umeme. Kile kifaa kwenda LG gharama ya hicho kifaa ni sawa na radio mpya. Mpaka leo nimebaki na kopo. Nimebakiwa na speaker tu
Hukuzingatia stabilizer, mi sikutaka kukosea kabisa maana connection ya umeme, mzik, friji na TV vinatokana na soketi 1, niligharamika kununua stabilizer mapema sana

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kuna kitu watu mnachanganya! Home Theater haijaundwa kwaajili ya heavy sound! Hiyo ni kwa kiswahili chepesi ni (Kitoa sauti) tu. Home theater haiwezi kushindana na Subwoofer kwasababu muundo wa coil zake speaker zake ni tofauti kabisa. Ingawa zote zinaathiriwa na Watts zake. Kama unataka mziki wa maana hakikisha Unanunua Hi-Fi System au Subwoofer yenye kuanzia watts 600. Home theater hata ikiwa na Watts 1000 hawezi kushindana na Subwoofer ya watts 400 au Hi-Fi ya watts 500.

Zingatia. Hi-Fi -> Woofer -> Home Theater
Weka hata picha tubarikiwe
 
Uwingi wa spika sio ukubwa wa sauti na wala ukubwa wa watts wa redio sio ukubwa wa sauti.
Sauti ambayo inarekodiwa na wanamuziki ni stereo kwa maana ina njia mbili mithili ya masikio yetu yalivyo.Radio ambazo ni home theater sio kwa ajili ya kusikilizia muziki ila ni kwa ajili ya kutazamia muvi mana kwenye muvi kila spika moja hupewa sauti maalumu kwa mfano kuna spika zinatoa sauti ya mazungumzo tu, kuna ambazo zinatoa sauti ya effect za kwenye muvi, kuna ambazo zinatoa sauti ya saund track na mambo mengine mengi na ndio maana ukizitumia kwenye mziki sauti haziwi kubwa sana kwa sababu spika ambazo zinafanya kazi huwa ni tatu tu( 2.1)spika moja ya kulia, moja ya kushoto na subwoofer.
Kitu kingine ni kwamba nguvu ya spika haipimwi kwa watt.Watt inaonyesha kiwango cha umeme ambao redio itatumia kwa muda fulani.Kiwango cha sauti kinapimwa na SPL yaani Sound pressure level.
Kadri Spl inavyokuwa kubwa ndo sauti nayo inakuwa kubwa. Kwahiyo redio kubwa ambayo ina watt kubwa na spl ndogo inazidiwa mdundo na radio ndogo ambayo inawatt ndogo ila spl kubwa.Kama shida yako ni sauti basi zingatia spl ila kama shida yako ni kujua redio inakula umeme kiasi gani basi zingatia watt.
LAMINATED COMMENT.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom