Nimenunua Bia yenye uchafu. Nikalalamike wapi?

Nimenunua Bia yenye uchafu. Nikalalamike wapi?

Habari za jioni wakuu,

Jamani naihitaji msaada hapa nimeagiza bia ila nilivoicheki kwa chini kuna kifuniko kipo ndani mule na bia sijaifungia naombeni ushauri nikalalamike wapi wadau?
NI RAHISI

Andika barua kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRA wa Mkoa uliopo, kwasababu wanakukata kodi kwenye Bia yenye uchafu.

Nakala kwa:

- Katibu Tawala Mkoa uliopo (RAS)

- Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya uliopo (DED)

- Mkuu wa wilaya uliopo (DC)

- Katibu tawala wilaya (DAS)

- Afisa lalamiko Wilaya

- Afisa Mtendaji wa kata ilipo baa, sharti awe na Mwenyekiti wa Mtaa au kijiji ilipo baa

- Mmiliki wa Bar, ambapo ulipata Bia hiyo hapo.

ZINGATIO:

- Piga picha label ya Bia hiyo na ukascan pamoja na bar code ionekane.

- Hakikisha unaambatana na mashahidi zaidi ya mmoja wenye akili timamu waliiona hicho kisoda katika Bia (wasiwe wamelewa)

- Hakikisha huna uhusiano wa kindugu au kirafiki na Shahidi yeyote utakayempeleka

- Hakikisha unaambatana na Polisi pamoja na mashahidi hai utakapokwenda kuscan hiyo label, kulaminate, kutoa copy na kuwapelekea viongozi husika ili walifanyie kazi, kuepuka polisi kuhongwa na kuvujisha hiyo siri

Hili halivumiliki hata kidogo kwakweli.
 
Habari za jioni wakuu,

Jamani naihitaji msaada hapa nimeagiza bia ila nilivoicheki kwa chini kuna kifuniko kipo ndani mule na bia sijaifungia naombeni ushauri nikalalamike wapi wadau?
Mzee kwani umenunua ukiwa kwenye basi wakati unasafiri?
 
Donoughue and Stevenson case

Donoghue v Stevenson [1932] UKHL 100 was a landmark court decision in Scots delict law and English tort law by the House of Lords. It laid the foundation of the modern law of negligence, establishing general principles of the duty of care.
 
Wenzio tulishakuta kondom iliyotumika wakati bia iko nusu, nusu nyingine tumboni, wewe unalamika kizibo?; Hebu kitoe hicho kizibo, kinyonye kisiondoke na utamu Kisha kifyekelee mbali
 
Habari za jioni wakuu,

Jamani naihitaji msaada hapa nimeagiza bia ila nilivoicheki kwa chini kuna kifuniko kipo ndani mule na bia sijaifungia naombeni ushauri nikalalamike wapi wadau?
Uwe makini unaagiza bia wakati wa msiba?
 
Kafungur kesi mahakamani negligence case, law of tort
 
Kwa nchi za wenzetu (sio sisi akina zoa zoa), hilo ni bonge la kashfa ambayo hakuna kampuni ambayo ingependa kashfa hiyo itoke nje kwa sababu itaathiri sana mauzo kwa kuonekana kuna tatizo kubwa la hygiene! Sasa ili kufunika hiyo kashfa, watataka m-settle nje ya mahakama, na hapo unaweza kutoka na mkwanja mnene na wa kutisha! Lakini hata kwa Kibongo bongo, pia wanaweza kukulipa mkwanja wa haja kwa sababu ili kuto-risk kufungiwa na mamlaka hadi watakapohakikisha wana mfumo mzuri wa uzalishaji
 
Back
Top Bottom