Nimemwachia mali zote, naanza upya

Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
9,008
16,134
Stori isiwe ndefu.

Mke wangu mtumishi na mimi mtumishi. Anatiwa ujinga na wenzake kila siku, tuna viwanja viwili na kimoja tumejenga. Leo nimempelekea hati za viwanja vyote na akae navyo.

Na nimemwambia nakuachia mali zote usiliwe KIZEMBE liwa ukiwa na hamu. Naondoka wasikilize hao marafiki zako. Simu nazopigiwa sio za dunia hii.

Nimeamua kumuachia mali zote, nianze upya. Wanawake Mungu anawaona. Sasa naombwa vikao kusululisha wakati ananionea kijinsia hakutafuta ndugu. Nimekaa miezi hanipi mzigo kwa ustaarabu sikutaka kumuingilia kinguvu.

Leo namuachia kila kitu nilichopambania ameita familia kutatua na kujadili nirudi kwenye ndoa ambayo hajaihudumu zaidi ya mwaka. Mimi Mkristo Mkatoliki ila huu ujinga sitaki

Nimempa kila kitu nianze upya.
 
Pole sana mkuu. Subiri feminist waje kukuambia hizo ni changamoto ndogo tu katika ndoa na kwamba ili uonyeshe uanaume wako ulitakiwa upambane nae msuluhishe muendelee kujenga familia.

Mimi natoka kidogo ntakuja kuchangia baadae
.
.
.
Nimerudi. Wanawake sijui nani kawaroga siku hizi. Nahisi hawa mashosti wa saluni, ofisini na vikoba wanawaharibu sana.

Juzi nilikuwa nimeenda mgahawa flani hivi karibu na hapa kitaa. Pembeni kuna kasaluni ka kike mbele wamekaa wale masela wanaowapaka rangi madem pamoja na kuwasugua sugua miguu (kwa wakazi wa dar mtakua mnanielewa) aisee story walizokua wanapiga ni aibu tupu. Kuna mdada namjua kabisa ameolewa anawahadithia mambo yake ya chumbani na mumewe mashosti zake ambao asilimia kubwa pale ni masingo maza na wameshapoteza muelekeo wa kua na waume wa kuwaoa. Wengine wanamshauri "heee mie mwanaume hanipelekeshi hivyo shosti! Yani nimechoka zangu na kazi eti anilazimishe nimfulie manguo yake! Kah mlioolewa mna kazi! Si amtafute tu beki tatu!" Wakaanza kujichekesha kinafki.. Mwengine anadakia, "shosti yani ww pambana na watoto wako huyo bwana pasua kichwa wa nini na una kazi yako mamii! Tafuta mchepu akupunguzie stress! Siku hizi haki sawa akikuletea za kuleta unampeleka dawati la jinsia.. Kwisha habari yake!!!"

Daaah! Nikajisemea kwa hali hii mabachela tuna kazi sana kumpata mwanamke anaejitambua na kutambua majukumu ya ndoa..

Nakumbuka dingi yangu mdogo alikuwa na mke na watoto wawili, mjengo na usafiri wa kutembelea na biashara iliyosimama. Lakini alikimbia mji wake na kutokomea mikoani kuanza upya. Ndugu walikuwa wanaponda sana kile kitendo kiasi kila mtu alikua anamchukia kwa yale maamuzi. Wahenga waliosema kuwa uyaone hawakukosea. Sasa ndio nimekuwa nimeanza kumuelewa dingilai!
 
Mnh! Hizi ndoa ni changamoto, ukiwa na moyo wa plastik hakika unaweza ukawa kichaa.

Muhimu haujamuumiza mtu anza upya, kama ulifika ulipofka hakika unaweza fika na zaidi. Pambana, ukiamua amua kweli na si kutania.

Mara nyingi kitanda usichokilalia huwezi jua kunguni wake, sasa basi maamuzi uliyofanya ni sahihi maana wewe ndiye muhuska mkuu. Muhimu usivunje amani ya nchi......
 
Kwa hiyo Uanaume ni kukimbia tatizo?

Mnawaokotaga wapi?
We Mzee ... Mwanamke anakuita mjinga,mpumbavu mbele za watu .. umemjengea , umempa Biashara ,umemsomesha... na alikuwa mhudumu tu wa ofisi ... Umemuwezesha pote huko ... Ya Nini ... Bahati mbaya nimesomesha maendeleo ya jamii na yupo ustawi anajifanya anajua haki za wanawake
..nimemwambia haya yote hayo Hapo .chukua .... Hataki anataka turudiane wakati Mimi sitaki hizo dharau.





.
 
Doh, pole Sana aisee. Wanawake ifikie mahali tubadilike kdg. Hii haki sawa hii itatuponza...

Kusikiliza mashoga watoe ushauri wa ndoa yangu, hapana kwa kweli. Khaaaa!!!!
Yaani... Alikuwa demu wangu wa kwanza kabisa ..nilimpenda na nampenda sana ..anajua hilo... Ndio nikasema to make story short .. nafaulu form four 2003 .. yeye anafeli .... miaka 9 mbele namkuta nilipoajiriwa ... Nikamsaidia kuajiriwa kama mhudumu na nikamsaidia kusoma maana nilimpenda sana.. daaah .... Na nikafunga naye ndoa 2016...... hamjui tu maumivu... nimeomba uhamisho niondoke kabisa hili eneo....
 
We Mzee ... Mwanamke anakuita mjinga,mpumbavu mbele za watu .. umemjengea , umempa Biashara ,umemsomesha... na alikuwa mhudumu tu wa ofisi ... Umemuwezesha pote huko ... Ya Nini ... Bahati mbaya nimesomesha maendeleo ya jamii na yupo ustawi anajifanya anajua haki za wanawake
..nimemwambia haya yote hayo Hapo .chukua .... Hataki anataka turudiane wakati Mimi sitaki hizo dharau.





.
Kumbe tatizo ulitengeneza mwenyewe bana.
 
Yaani... Alikuwa demu wangu wa kwanza kabisa ..nilimpenda na nampenda sana ..anajua hilo... Ndio nikasema to make story short .. nafaulu form four 2003 .. yeye anafeli .... miaka 9 mbele namkuta nilipoajiliwa ... Nikamsaidia kuajiliwa kama mhudumu na nikamsaidia kusoma maana nilimpenda sana.. daaah .... Na nikafunga naye ndoa 2016...... hamjui tu maumivu ...nimeomba uhamisho niondoke kabisa hili eneo....
I can feel you brother pole sana, Japo tatizo umelitengeneza pale ulipompeleka akasome maswala ya haki sawa. Tafuta toto ingine anza upya mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom