Nimemuomba aje tuishi, tufunge ndoa hataki

jean phillipe beyun

Senior Member
May 18, 2015
142
167
Wadau nawasalim,

Kuna mshikaji wangu tulikua tunakaa gheto moja 2005_2007 tuliishi kama ndugu kwa kweli, bahati mbaya 2008 akatangulia mbele za haki.

2010 kuna mdogo wake wa kike aliewahi kututembelea siku za nyuma wakati kaka yake yupo hai akanipigia simu kuwa anaomba kuja mjini afikie kwangu aje kujaribu maisha town, kwa kuwa kuna mdogo wangu wa kike niliekua naishi nae hapo nikaona haina shida aje tu wawe kampani moja.

Akaja, akajiunga na kozi ya hotel mgmt, wakawa hawaishi kugombana na mdogo wangu, yule binti akatoka kwangu na kwenda kuishi kwa ndugu mmoja wa ukoo, lakini ikawa kila mara anafika kazini kwangu kuomba hela za kujikimu, baadae akajiunga kwa certificate of business administration, alinisumbua sana wakati wa kozi hii, maana ada hana ikawa ni kuunga unga tu, nilimsaidia sana, hadi akamaliza

Sasa amejiunga tena chuo kwa ajili ya diploma in business admin academic year iliyoanza November nadhan, akalipa pesa kidogo tu akawaambia December atapeleka zingine, sasa amekuja kwangu juzi, huwa ananiita kaka, akasema ""kaka nisaidie fedha kiasi nikatatue shida za shule, sina hela ya hostel, fees, transport, na nimezuiwa kuingia class.

Nikamwambia, ""mama"" nimeshakusaidia sana huko nyuma, sijanufaika na chochote, sasa basi huna haja ya kuhangaika kiasi hicho, fanya hivi beba mizigo yako yote uje tuishi, tufunge ndoa tuishi kama mke na mme, nitagharamia elimu yako hata hadi degree ukitaka, Chuo unaweza kusoma huku ukiwa umeolewa, na bahati nzuri nimeshamaliza nyumba nimehamia tayari, njoo ujinafasi.

Cha kusikitisha akaanza kujiuma uma, ooh nina mtu wangu, yakaenda yakarudi, na ushenzi mwingine mwingi unaofanana na huo,
Miaka yote niliyokua nakusaidia maisha kama mdogo wangu huyo mpenzi alikua wapi, ingawa nilikua namsaidia kama mdogo wa marehemu rafiki yangu lakini sasa gharama zimeshakua kubwa, pia nami kama mwanadam niliekamilika nimeona nimsaidie kwa muoa hata roho ya ndugu.yake itapumzika kwa amani, anaanza ngonjera.

Mm hadi sasa nimekua na complications nyingi kwenye mapenzi sasa nikaona bora nimchukue huyu binti, siwezi kumlipia hizo gharama kabla ya kumuoa maana nawajua wasichana vizuri atakuja kunigeuka akamaliza chuo, ila nikimuweka ndani, nikapiga na mimba moja mbili hatakua na ujanja tena wa kunigeuka.

Achague moja asome kwa mateso hivyo hivyo kwa kuomba omba, au aje watu wale mpunga asome kwa starehe huku akipunga upepo wa ununio beach nilikohamia.

Au wadau mlikua mnasemaje?
 
Sisi twaona kwa kutumia macho.

we unaonaje kwani ?
 
Unatumia udhaifu na shida za mtu ila kujinufaisha? Hakika utalaaniwa maana hujui wewe watoto wako yatawakuta yepi! Nani anayeijua kesho yake? Kama unamsaidia msaidie tu kama lah basi muache. Hio biashara unayotaka kuifanya ni hatari
 
uyo bint ametumia busara sana...angeweza kukubali ndoa na akafanya yake na akimaliza degree asepe zake...ndoa kitu gani bhana!!!

in short hakupendi na unaonekana kweli upo complicated kwebmny relation zako na hauko romantic ..MTU mpaka unajenga na kuhamia huna ata mchumba?loll hufai ata bure. .
niache mtoto wa watu km unamsaidia sawa. hutak muache
 
Kma kweli unataka kumuowa nenda ongea nae vizuri kwanza akisha kukubali kuwa mpenzi wako nenda nyumbani kwao kajitambulishe then umchukue kwa haki,maana isije ikawa tamaa ya mwili tu ukishamgeuza upendavyo umuache mtoto wa watu,Kumbuka rafiki yako so tenda haki mdumishe undugu.Asante
 
Unaenda kumuoa mtu si kwa sababu ya kumpenda bali shida zake.
Ila unaonekana una uwezo mdogo wa kutongoza.!
 
Dah! Umempa bonge la Opportunity alafu anazingua. Mtafutie video ya semina ya Mwakasege pale kwenye viwanja vya chuo kikuu aliposema wanawake ambao wanahitaji kuolewa waje hapa mbele. Nasikia nusu ya mkusanyiko ulienda pale...
 
Inauma wewe unatoa fedha wengine wanakula kiulainiiiii. Hapana na wakati mwingine amege fedha unayompa ampe kidume mbegu kijinafasi kwa raha zake! Tusidanyanyane kila mtu ni mwekezaji. Akitoa senti yake anaamini atanufaika vipi siku za mbele
 
Hujakosea mkuu, hujambaka wala hata hvyo umeshamgharamia sana. kama amekukataa basi akasomeshwe na atakaekua mme wake. wewe muambie tu huna hela. na kwa kozi alizosoma zinamtosha kutafuta kazi na kujitegemea
 
Sio poa kama una msaidia msaidie lakini usiombe show maana huyo hujampenda ila kigezo ni shida zake.kkwahy toa msaada kama una uwezo kama huna mwambie ukweli.
 
Back
Top Bottom