VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Rais John Pombe Magufuli na serikali yake wamewashika watanzania. Wameamua kufanya jambo moja kubwa kisiasa:kujitangaza. Kila tendo au neno la Rais au wa chini yake linatangazwa. Kama si luningani,redioni basi litachomoza gazetini au hata mtandaoni. Uongozi matangazo!
Kujitangazatangaza huku kunawafanya waamini kuwa serikali inafanya kazi na Ilani inatekelezwa. Wananchi wanaoneshwa,kutangaziwa au kuandikiwa maagizo,maelekezo,teuzi na hata maigizo yasiyo na ujuzi. Ilimradi wananchi wasiache kusikia,kusoma au kuona.
Kauli hazitoi nauli. Vyeo havileti maendeleo. Lakini,kusemasema na kutajwatajwa kuna uzito wake wa vito kisiasa. Viwanda vitajengwa na kuoneshwa. Tanzania ya viwanda yaja!Vyombo vya habari,ni muda wenu kuajiri wengi kwakuwa kila kiongozi atataka filamu yake ionekane na kutamba. Naunga mkono ubunifu na usanifu huu maarufu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Zanzibar)