Nimemuelewa Rais Magufuli, sasa namuunga mkono

Kujitangaza. Kila tendo au neno la Rais au wa chini yake linatangazwa. Kama si luningani,redioni basi litachomoza gazetini au hata mtandaoni. Uongozi matangazo!..........VIPI KUHUSU KUTANGAZWA KWA MATANGAZO YA BUNGE?
 
Rais John Pombe Magufuli na serikali yake wamewashika watanzania. Wameamua kufanya jambo moja kubwa kisiasa:kujitangaza. Kila tendo au neno la Rais au wa chini yake linatangazwa. Kama si luningani,redioni basi litachomoza gazetini au hata mtandaoni. Uongozi matangazo!

Kujitangazatangaza huku kunawafanya waamini kuwa serikali inafanya kazi na Ilani inatekelezwa. Wananchi wanaoneshwa,kutangaziwa au kuandikiwa maagizo,maelekezo,teuzi na hata maigizo yasiyo na ujuzi. Ilimradi wananchi wasiache kusikia,kusoma au kuona.

Kauli hazitoi nauli. Vyeo havileti maendeleo. Lakini,kusemasema na kutajwatajwa kuna uzito wake wa vito kisiasa. Viwanda vitajengwa na kuoneshwa. Tanzania ya viwanda yaja!Vyombo vya habari,ni muda wenu kuajiri wengi kwakuwa kila kiongozi atataka filamu yake ionekane na kutamba. Naunga mkono ubunifu na usanifu huu maarufu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Zanzibar)

Na bado Bunge halitoonyeshwa kamwe.Kila siku itakuwa mbwembwe na viroja mara leo kamtimua katibu kata kesho afisa kilo wa wilaya mtondogoo Tanzania itauza umeme nchi jirani.

Kila siku porojo hakuna lolote zaidi ya promo za kitoto eti umeme umeshushwa bei 1% huku IPTL ikiendelea kulipwa mabilioni ya kodi zetu.Kama kweli kazi ni kutumbua majipu ni kwanini walioliingiza taifa katika mikataba ya kinyonyaji hawashitakiwi ????????.
 
Rais John Pombe Magufuli na serikali yake wamewashika watanzania. Wameamua kufanya jambo moja kubwa kisiasa:kujitangaza. Kila tendo au neno la Rais au wa chini yake linatangazwa. Kama si luningani,redioni basi litachomoza gazetini au hata mtandaoni. Uongozi matangazo!

Kujitangazatangaza huku kunawafanya waamini kuwa serikali inafanya kazi na Ilani inatekelezwa. Wananchi wanaoneshwa,kutangaziwa au kuandikiwa maagizo,maelekezo,teuzi na hata maigizo yasiyo na ujuzi. Ilimradi wananchi wasiache kusikia,kusoma au kuona.

Kauli hazitoi nauli. Vyeo havileti maendeleo. Lakini,kusemasema na kutajwatajwa kuna uzito wake wa vito kisiasa. Viwanda vitajengwa na kuoneshwa. Tanzania ya viwanda yaja!Vyombo vya habari,ni muda wenu kuajiri wengi kwakuwa kila kiongozi atataka filamu yake ionekane na kutamba. Naunga mkono ubunifu na usanifu huu maarufu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Zanzibar)

hahaaa hapa kazi kweli

muda wa kazi raisi yupo na mkewe wanapata muda wan kupiga simu kwa tv

makonda wakamate wote wanaocheza pool table asubuhi badala ya kuwa na wakezao au kupiga simu clouds

hahahaahhhaaaa mwaka mtamu huuu
 
Kujitangaza. Kila tendo au neno la Rais au wa chini yake linatangazwa. Kama si luningani,redioni basi litachomoza gazetini au hata mtandaoni. Uongozi matangazo!..........VIPI KUHUSU KUTANGAZWA KWA MATANGAZO YA BUNGE?
Bunge si serikali

Mzee Tupatupa
 
sijaona chochote kilichofanywa na serikali hii zaidi ya porojo na matangazo kwenye media ni full maigizo na watz ni vipofu wa fikra na wao muda wote wako kwenye media kuangalia leo kuna tangazo gan
Watanzania ni watu wenye akili finyu sana!!!
 
hapo ndo ushange sasa, maana pamoja na kujinasabukwenye media kuwa ukusanyaji wa mapato umeongezeka maradufu, bado hospitali hazina dawa, hakuna vitanda, shulen madawati na vyumba vya madarasa havitoshi pamoja na matatizo mengine rukuki, sasa hiz hela zinazokusanywa sjui nani anakula
Nilikua ileje majuzi, niliyoyaona huko hayasimuliki.... Ndo najiuliza hizo kasi anazosifiwa ni ktk nini hasa?

Kila kitu bei juu gharama za mawasiliano hazishikiki chakula hatari tupu sasa sijui hiyo kasi ni IPI wengine mtuambie....
 
unakaa kwenye computer unafunga macho alafu then unafungua ukute ghorofa imetokea hapo mbele yako ghafla ndio utasema magufuli kafanya kitun( no miracle in development but the dev. is processes moving from one stage to another), wewe mwenyewe umefanya nini tangu magufuli achaguliwe,
Hebu wewe utusaidie basi kutuambia hiyo kasi sijui spidi ni ktk nini hasa?
 
Rais John Pombe Magufuli na serikali yake wamewashika watanzania. Wameamua kufanya jambo moja kubwa kisiasa:kujitangaza. Kila tendo au neno la Rais au wa chini yake linatangazwa. Kama si luningani,redioni basi litachomoza gazetini au hata mtandaoni. Uongozi matangazo!

Kujitangazatangaza huku kunawafanya waamini kuwa serikali inafanya kazi na Ilani inatekelezwa. Wananchi wanaoneshwa,kutangaziwa au kuandikiwa maagizo,maelekezo,teuzi na hata maigizo yasiyo na ujuzi. Ilimradi wananchi wasiache kusikia,kusoma au kuona.

Kauli hazitoi nauli. Vyeo havileti maendeleo. Lakini,kusemasema na kutajwatajwa kuna uzito wake wa vito kisiasa. Viwanda vitajengwa na kuoneshwa. Tanzania ya viwanda yaja!Vyombo vya habari,ni muda wenu kuajiri wengi kwakuwa kila kiongozi atataka filamu yake ionekane na kutamba. Naunga mkono ubunifu na usanifu huu maarufu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Zanzibar)

Mjomba hujampongeza pia kwa kusema hata peleka maendeleo kwa Yale majimbo ya Wapinzani kwani huwezi kupeleka chakula kwa Mtoto wa Kambo wakati wa kwake ananjaa.Kwa hiyo tulio kwenye majimbo ya Upinzani tumemuelewa.Maendeleo yetu tutajikusanya na tutafika.Ila Kikubwa tumemuelewa Mjomba.
 
zanzibar ipi ya ufipa?

Ila ni kweli kwamba serekali hii matangazo mengi kuliko ubora wa kazi yenyewe. Simaanishi kwamba hakuna kinachofanyika lakini sifa zimezidi ubora wa kile kinachotangazwa. Ngoja tuone kinachoendelea kama wenyewe mnavyopenda kusema ni bado mapema watu wanapowabana kwenye angle ya maendeleo ya kweli. Sasa hivi kutumbua majibu imekuwa kama kibao kizuri chenye mirindimo mizuri hata kama hujui kinachoimbwa wala hakina faida kwenye maisha yako. Hao watumbuliwa majibu nasikia bado wanachukua mishahara yao tena wengine wana part time kiasi kwamba wanakula double salary. Je ni ya kweli haya Stroke?
 
Kiongozi yeyote akisimama kidete hata kwenye familia katika misingi yamaadili na utu kwa ujumla,maendeleo lazima yaonekane na ndio vyombo vingi vya habar vinamulika sababu yaliyokemewa yamepatiwa ufumbuz, nani kwa manufaa ya wote japokua wachache vichwa maji kama wana ukawa watapuuza kwa intrest zao za uroho, uchu wa madaraka na kuogopa kupokwa wafuasi wao
 
Bunge si serikali

Mzee Tupatupa

Tatizo ninaloliona ni kukosekana kwa uwiano katika kutangaza shughuli za serikali.Kwa upande mmoja serikali inatangazwa sana ila muhimili mwingine wa dola (bunge) umefinywa kujitangaza.
Pili katika bunge kuna viongozi wengi wa serikali mule.Ni uwanja mzuri kwa serikali kuendelea kujinadi ukizingatia umahiri wa mawaziri na serikali ya awamu ya tano.
 
Serikali ya Magufuli haina dira; haina falsafa ya maendeleo. Magufuli hana maono kwa nchi hii; hana mrengo wa kiitikadi anaoegemea. Anasema elimu bure wakati hata falsafa ya elimu yetu haijulikani. Anasema "Tanzania ya viwanda" wakati hata hajui aanzie wapi! Anasema anatumbua majibu kumbe ni sarakasi tupu za kisiasa. Katika mazingira kama haya serikali na chama chake wanalazimika wawekeze katika propaganda ili angalau wananchi wazidi kuamini kuwa "kuna serikali inayowahudumia". Lakini njia ya mwongo ni fupi...
 
Kidogo nijisemee 'ubaya kweli unamwisho' mpaka niliposoma message yenyewe.
 
Mi nafikiri kuna kitu kina haunt hii serkali. Awamu ya 5 inatafuta legitimacy na kukubalika kwa wananchi kupitia media!
 
Mjomba hujampongeza pia kwa kusema hata peleka maendeleo kwa Yale majimbo ya Wapinzani kwani huwezi kupeleka chakula kwa Mtoto wa Kambo wakati wa kwake ananjaa.Kwa hiyo tulio kwenye majimbo ya Upinzani tumemuelewa.Maendeleo yetu tutajikusanya na tutafika.Ila Kikubwa tumemuelewa Mjomba.
Aanze na Dodoma kama kweli anawapenda wanae
 
unakaa kwenye computer unafunga macho alafu then unafungua ukute ghorofa imetokea hapo mbele yako ghafla ndio utasema magufuli kafanya kitun( no miracle in development but the dev. is processes moving from one stage to another), wewe mwenyewe umefanya nini tangu magufuli achaguliwe,

Amefanya nini? Kwani alishakuja kwako kukuomba msaada wa kuendesha familia yake?Au unafikiri wote ni kula kulala kama wewe?
 
Na Rais baada ya kuona Clouds wamepunguza speed akaona aruke nao hewani kipindi cha 360.
Wakati wengine wanaambiwa wawahi kazini yeye yuko na mama chumbani wanaongea na mtangazaji wa studio.
Na bado senema ndio zinaanza, kama Isidingo vile
Umenena mkuu chukua like hiyo
 
Back
Top Bottom