Nimemsaidia; sasa ananitongoza

Nimemsaidia; sasa ananitongoza

Ilikuwa majira ya saa nne usiku wakati narejea nyumbani, siku hiyo sikutumia usafiri binafsi nilikuwa sijaenda mbali, lakini kutokana na kukolea story za hapa na pale nilijikuta narejea home muda huo saa nne usiku. Kutoka barabara kuu hadi nyumbani ni lazima ukatize miti na vichaka kadhaa na nyumba chache kabla kufikia mtaa ninaoishi.

Nikiwa katikati ya miti na vichaka nilisikia mbele yangu yowe la mwanamke akiomba msaada. Nilikaza miguu kuwahi lakini kwa tahadhari, nilikuta vijana wawili wamemdhibiti huku wakijitahidi kumnyang'anya mkoba wake. Kwa kuwa kimazoezi siyo mvivu nilifanikiwa kuwakabili wale vijana na walikimbia wakiwa tayari na maumivu miilini mwao. Yule mwanamke/ Binti alinishukuru na aliniambia walifanikiwa kumpora hereni na mkufu wake tu. Mkoba ulibaki salama na aliniambia alikuwa ametoka ubalozi siku hiyo kuchukua visa yake kwani anasafiri kesho yake mchana, hivyo sambamba na hati ya kusafiria alikuwa na nyaraka muhimu za ofisi ambazo angesafiri nazo.

Kwa kuwa yeye ni mgeni mtaani kwetu nilimsindikiza hadi karibu na kwake kisha mie nikashika zangu njia kwenda nyumbani. Nakumbuka tulibadilishana namba za mawasiliano.

Alikwenda safari, sikujua amerejea lini lakini hivi sasa ni wiki ya tatu tangu aanze kuwasiliana nami. Of course nimekutana naye (siyo kimwili) mara kwa mara maeneo ya kujidai. Kitu cha kushangaza ni kuwa amekuwa akinitokea ktk simu kwa waziwazi akisema tangu siku ile niliyomuokoa ametokea kunipenda na angependa niwe naye faragha na chochote atanipa. Ukweli nimeshangazwa na ujasiri wake wa kunitokea. nimemuambia kuhusu status yangu ya ndoa na watoto lakini amesema kuwa japo yote hayo lakini anapenda just to hang out with me for sometime.

Kiukweli nimesawajika maana nikikumbuka ule mchepuko wangu ambao umeniachia kumbukumbu mbaya maishani sipati jibu. Pili ni kweli binti analipa idara zote (ingawa sijui afya status yake), na nikiangalia ni kuwa siku ile ya balaa aliacha gari gereji na pia anajiweza kiuchumi hatohitaji kuhongwa bali atahitaji mtu ampepee tu! Ni kweli nimuonapo my other head inakwenda crazy lakini my real top head inagoma kabisa kutoa ushirikiano.

Nimeleta hapa nikiomba ushauri namna ya kumkwepa kwani ni jirani yangu na ananivuruga kweli kimawazo. Mke wangu sitomuambia kwai hatoniamini na itaniletea tatizo jingine.

Naomba ushauri wakuu

Baki na mke wako uchi ni uchi tuu hata ukiwa wa mtoto. Acha tamaa zako na baki na mke wako. Unaweza kuwa nae as friends na siyo kufanya ngono. Sasa ukishafanya ngono then what.?
 
We vepeee!! hebu Ramba vitu mura ukishindwa wapasie wengine wenye njaa mura,
Ni hayo tu kwa REO mura ,ngoja niwahi kwa mama robhi naona ananidip sana.
 
heri yako wewe story zako za kusadikika zina sound poa..kuliko mwenzio MSHANA JR kazi kutisha watu mara leo midoly ina roho..mara kutoka nje ya mwili aaaaaaaarrrrrgh
 
Ilikuwa majira ya saa nne usiku wakati narejea nyumbani, siku hiyo sikutumia usafiri binafsi nilikuwa sijaenda mbali, lakini kutokana na kukolea story za hapa na pale nilijikuta narejea home muda huo saa nne usiku. Kutoka barabara kuu hadi nyumbani ni lazima ukatize miti na vichaka kadhaa na nyumba chache kabla kufikia mtaa ninaoishi.

Nikiwa katikati ya miti na vichaka nilisikia mbele yangu yowe la mwanamke akiomba msaada. Nilikaza miguu kuwahi lakini kwa tahadhari, nilikuta vijana wawili wamemdhibiti huku wakijitahidi kumnyang'anya mkoba wake. Kwa kuwa kimazoezi siyo mvivu nilifanikiwa kuwakabili wale vijana na walikimbia wakiwa tayari na maumivu miilini mwao. Yule mwanamke/ Binti alinishukuru na aliniambia walifanikiwa kumpora hereni na mkufu wake tu. Mkoba ulibaki salama na aliniambia alikuwa ametoka ubalozi siku hiyo kuchukua visa yake kwani anasafiri kesho yake mchana, hivyo sambamba na hati ya kusafiria alikuwa na nyaraka muhimu za ofisi ambazo angesafiri nazo.

Kwa kuwa yeye ni mgeni mtaani kwetu nilimsindikiza hadi karibu na kwake kisha mie nikashika zangu njia kwenda nyumbani. Nakumbuka tulibadilishana namba za mawasiliano.

Alikwenda safari, sikujua amerejea lini lakini hivi sasa ni wiki ya tatu tangu aanze kuwasiliana nami. Of course nimekutana naye (siyo kimwili) mara kwa mara maeneo ya kujidai. Kitu cha kushangaza ni kuwa amekuwa akinitokea ktk simu kwa waziwazi akisema tangu siku ile niliyomuokoa ametokea kunipenda na angependa niwe naye faragha na chochote atanipa. Ukweli nimeshangazwa na ujasiri wake wa kunitokea. nimemuambia kuhusu status yangu ya ndoa na watoto lakini amesema kuwa japo yote hayo lakini anapenda just to hang out with me for sometime.

Kiukweli nimesawajika maana nikikumbuka ule mchepuko wangu ambao umeniachia kumbukumbu mbaya maishani sipati jibu. Pili ni kweli binti analipa idara zote (ingawa sijui afya status yake), na nikiangalia ni kuwa siku ile ya balaa aliacha gari gereji na pia anajiweza kiuchumi hatohitaji kuhongwa bali atahitaji mtu ampepee tu! Ni kweli nimuonapo my other head inakwenda crazy lakini my real top head inagoma kabisa kutoa ushirikiano.

Nimeleta hapa nikiomba ushauri namna ya kumkwepa kwani ni jirani yangu na ananivuruga kweli kimawazo. Mke wangu sitomuambia kwai hatoniamini na itaniletea tatizo jingine.

Naomba ushauri wakuu

Ni pm no ya huyo dada aisee
 
Amri ya sita "USIZINI' mungu kakupa miguu macho akili mikono nk dhambi zingine zikimbie ogopa
 
Mwongo mkubwa we! Unaleta umbeya kupoteza muda wa members kwenda kumchambua Jambazi sugu na wale wanaolamba peremende.
 
Mkuu....mpime afaya yenu, kisha muandae muda mwanana uka mpepee...
maisha yenyewe haya mafupi....kwani ukizubaa waweza kuta mmoja wa wale jamaa
waliompiga ngeta (kabali ya mbao) anakula mzigo.

Hahahaa!
 
mkuu kwa kuwa moyo wako unasita,ni bora uache,regardless huyo dada yupo vipi,ukishakula itakusumbua saerna,na utajuta na kusema ulishasita tangu.,better option achana naye
 
Ni saa nne ya usiku, ametoka kuchukua visa na ana safari kesho yake...okay. Sasa ameshindwa hata kuchukua boda boda au bajaji imfikishe anapoenda mpaka apite vichakani huku kabeba nyaraka muhimu?

Haha we kweli Mⓢⓐⓝⓘⓘ.
 
Soma kati ya mistari.....
aliacha gari gereji huwezi kujua alipata breakdown au nini, pengine alikuwa na mishe za kuaga muda ukampiga mkono...

muda huo huko kwetu hakuna boda, unapiga Lexus tu mpaka hme kama huna wheels
 
Back
Top Bottom