Nimemsaidia; sasa ananitongoza

Nimemsaidia; sasa ananitongoza

Ilikuwa majira ya saa nne usiku wakati narejea nyumbani, siku hiyo sikutumia usafiri binafsi nilikuwa sijaenda mbali, lakini kutokana na kukolea story za hapa na pale nilijikuta narejea home muda huo saa nne usiku. Kutoka barabara kuu hadi nyumbani ni lazima ukatize miti na vichaka kadhaa na nyumba chache kabla kufikia mtaa ninaoishi.

Nikiwa katikati ya miti na vichaka nilisikia mbele yangu yowe la mwanamke akiomba msaada. Nilikaza miguu kuwahi lakini kwa tahadhari, nilikuta vijana wawili wamemdhibiti huku wakijitahidi kumnyang'anya mkoba wake. Kwa kuwa kimazoezi siyo mvivu nilifanikiwa kuwakabili wale vijana na walikimbia wakiwa tayari na maumivu miilini mwao. Yule mwanamke/ Binti alinishukuru na aliniambia walifanikiwa kumpora hereni na mkufu wake tu. Mkoba ulibaki salama na aliniambia alikuwa ametoka ubalozi siku hiyo kuchukua visa yake kwani anasafiri kesho yake mchana, hivyo sambamba na hati ya kusafiria alikuwa na nyaraka muhimu za ofisi ambazo angesafiri nazo.

Kwa kuwa yeye ni mgeni mtaani kwetu nilimsindikiza hadi karibu na kwake kisha mie nikashika zangu njia kwenda nyumbani. Nakumbuka tulibadilishana namba za mawasiliano.

Alikwenda safari, sikujua amerejea lini lakini hivi sasa ni wiki ya tatu tangu aanze kuwasiliana nami. Of course nimekutana naye (siyo kimwili) mara kwa mara maeneo ya kujidai. Kitu cha kushangaza ni kuwa amekuwa akinitokea ktk simu kwa waziwazi akisema tangu siku ile niliyomuokoa ametokea kunipenda na angependa niwe naye faragha na chochote atanipa. Ukweli nimeshangazwa na ujasiri wake wa kunitokea. nimemuambia kuhusu status yangu ya ndoa na watoto lakini amesema kuwa japo yote hayo lakini anapenda just to hang out with me for sometime.

Kiukweli nimesawajika maana nikikumbuka ule mchepuko wangu ambao umeniachia kumbukumbu mbaya maishani sipati jibu. Pili ni kweli binti analipa idara zote (ingawa sijui afya status yake), na nikiangalia ni kuwa siku ile ya balaa aliacha gari gereji na pia anajiweza kiuchumi hatohitaji kuhongwa bali atahitaji mtu ampepee tu! Ni kweli nimuonapo my other head inakwenda crazy lakini my real top head inagoma kabisa kutoa ushirikiano.

Nimeleta hapa nikiomba ushauri namna ya kumkwepa kwani ni jirani yangu na ananivuruga kweli kimawazo. Mke wangu sitomuambia kwai hatoniamini na itaniletea tatizo jingine.

Naomba ushauri wakuu

Mambo mengine ndugu yangu ni utoto kweli sasa unaulizq nini wakati unaweza we mwenyewe tu kuamua umtandike nao mkia au laaa
 
Mkuu Msanii hiki kidole cha 21 kwa wanaume wengi kinatupelekesha sana. Sikiliza ushauri wa kichwa cha juu ma achana na kidole cha 21 man!!!
 
Last edited by a moderator:
Naona unajitihada binafsi za kuharibu ndoa yako..... mara mchepuko sasa huyu.....
Mkeo akisepa rudi utapewa tu ushauri
 
Mwambie wazi kuwa umeoa na hutaki kufanya uzinzi. Pia Mungu hapendi.
 
Tatizo liko wapi sasa, kitendea kazi si unacho na ulipewa bure au hujui matumizi yake?
 
Sasa ananitokea
Pls mkanye maana nijuavyo mwanamke akitaka lake daaah huwa hapatoshi...

Huyo si wangu...maana wa kwangu hata nje ya mtwara hajawahi kutoka...nzuri zaidi hata passport hana😎
 
Fanya kile akili yako imekutuma.
Muulize mkeo kama unaona huwezi kufanya maamuzi sahihi.
 
ukitembea nae dhambi umefanya uzinzi, ukimuacha bure unaonekana joka la kibisa..
maamuzi ni yako na story za kutunga
 
Ilikuwa majira ya saa nne usiku wakati narejea nyumbani, siku hiyo sikutumia usafiri binafsi nilikuwa sijaenda mbali, lakini kutokana na kukolea story za hapa na pale nilijikuta narejea home muda huo saa nne usiku. Kutoka barabara kuu hadi nyumbani ni lazima ukatize miti na vichaka kadhaa na nyumba chache kabla kufikia mtaa ninaoishi.

Nikiwa katikati ya miti na vichaka nilisikia mbele yangu yowe la mwanamke akiomba msaada. Nilikaza miguu kuwahi lakini kwa tahadhari, nilikuta vijana wawili wamemdhibiti huku wakijitahidi kumnyang'anya mkoba wake. Kwa kuwa kimazoezi siyo mvivu nilifanikiwa kuwakabili wale vijana na walikimbia wakiwa tayari na maumivu miilini mwao. Yule mwanamke/ Binti alinishukuru na aliniambia walifanikiwa kumpora hereni na mkufu wake tu. Mkoba ulibaki salama na aliniambia alikuwa ametoka ubalozi siku hiyo kuchukua visa yake kwani anasafiri kesho yake mchana, hivyo sambamba na hati ya kusafiria alikuwa na nyaraka muhimu za ofisi ambazo angesafiri nazo.

Kwa kuwa yeye ni mgeni mtaani kwetu nilimsindikiza hadi karibu na kwake kisha mie nikashika zangu njia kwenda nyumbani. Nakumbuka tulibadilishana namba za mawasiliano.

Alikwenda safari, sikujua amerejea lini lakini hivi sasa ni wiki ya tatu tangu aanze kuwasiliana nami. Of course nimekutana naye (siyo kimwili) mara kwa mara maeneo ya kujidai. Kitu cha kushangaza ni kuwa amekuwa akinitokea ktk simu kwa waziwazi akisema tangu siku ile niliyomuokoa ametokea kunipenda na angependa niwe naye faragha na chochote atanipa. Ukweli nimeshangazwa na ujasiri wake wa kunitokea. nimemuambia kuhusu status yangu ya ndoa na watoto lakini amesema kuwa japo yote hayo lakini anapenda just to hang out with me for sometime.

Kiukweli nimesawajika maana nikikumbuka ule mchepuko wangu ambao umeniachia kumbukumbu mbaya maishani sipati jibu. Pili ni kweli binti analipa idara zote (ingawa sijui afya status yake), na nikiangalia ni kuwa siku ile ya balaa aliacha gari gereji na pia anajiweza kiuchumi hatohitaji kuhongwa bali atahitaji mtu ampepee tu! Ni kweli nimuonapo my other head inakwenda crazy lakini my real top head inagoma kabisa kutoa ushirikiano.

Nimeleta hapa nikiomba ushauri namna ya kumkwepa kwani ni jirani yangu na ananivuruga kweli kimawazo. Mke wangu sitomuambia kwai hatoniamini na itaniletea tatizo jingine.

Naomba ushauri wakuu

Mamaa.....uwiii...hang out wth her carefully...kisela tu brouh..ka akuelew..deal nae tu...mwanamke akupendae halaf wamringia n dhambi...mwambie asidisturb ndoa yako tu...
 
Hizi movie za akina van damme zinamengi, hii sasa hata tittle yake sijui inaitwaje
 
Back
Top Bottom