TANZIA Nimempoteza baba yangu mzazi

Nimempoteza baba yangu mzazi

Sijui hata nisemeje

Baba ndo.alikua kila kitu kwangu

Roho inaniuma baba kafa kanipambania mwanae nisome leo baba kafa ikiwa hata hajala mkono wangu nikiwa still napambana kupata kazi

Nimebaki yatima mimi
Pole sana mkuu. Bado una nafasi ya kumfanya afurahie matunda yako.

Ni furaha kwa Kila mzazi kuona watoto wake wakifanikiwa. Kama jitihada zake ilikuwa ni kukufanya ufikie sehemu nzuri kimaisha, basi muenzi kwa kuhakikisha unatimiza ndoto zake.

Fight for your better tomorrow, and your father will rest easy and happily.
 
Nimempoteza baba yangu mzazi

Sijui hata nisemeje

Baba ndo.alikua kila kitu kwangu

Roho inaniuma baba kafa kanipambania mwanae nisome leo baba kafa ikiwa hata hajala mkono wangu nikiwa still napambana kupata kazi

Nimebaki yatima mimi
Kuna emoji ya kucheka. Hebu itoe. Nimeifikia nikatamani kucheka nikakumbuka kisa ni cha huzuni.

Baba yako hakukupambania ili aje kula jasho lako wala unachokiita mkono wako. Ilikuwa ni wajibu wake kama mzazi aliyekuleta duniani.

Na wewe usiwakuze na kuwapambania wanao ili waje wakusaidie. Itabaki ni hiari yao tu.

Muombee apumzike anapostahili. Hata wewe utakufa siku moja.
 
Nimempoteza baba yangu mzazi

Sijui hata nisemeje

Baba ndo.alikua kila kitu kwangu

Roho inaniuma baba kafa kanipambania mwanae nisome leo baba kafa ikiwa hata hajala mkono wangu nikiwa still napambana kupata kazi

Nimebaki yatima mimi
Pole mkuu ila tunaambiwa tushukulu kwa kila jambo sijajua imani yako iko upande gani ila unaweza ukawa unamsomea dua na kumtolea sadaka marakwa mara swahabu zikamfikia huko alipo na huko ndo kukawa muhimu sana kwake ndo kula kwenyewe ndo maana tumeambiwa tuache watoto walio wema kwaiyo mkuu kuwa upande watoto aliye mwema pole sana
 
Pole sana ndugu yangu. Mshukuru Mungu kwa muda aliokupa wa kuwa naye huyo baba. Wengine baba zetu walitwaliwa mapema hata hatukupata muda wa kuwafahamu wala kuwakumbuka. Na tulikua hivyo hivyo bila role models wala nini. Na makovu yake yangalipo!

Pass it forward sasa. Mema yote aliyokufundisha. Kayaeneze hayo. Kawe binadamu mwema na bora kwa kadri inavyowezekana. Na siku utakapopata mke na watoto wako basi kajibidishe sana kuwa mume mwema na baba wa kupigiwa mfano. Ndiyo njia bora zaidi ya kumuenzi baba yako maana yeye kazi yake keshaimaliza na safari yake hapa duniani imekoma.

Asante na pole sana. Mungu Akutie nguvu na Upendo wake usio na kikomo ukawafariji nyote 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Nimempoteza baba yangu mzazi

Sijui hata nisemeje

Baba ndo.alikua kila kitu kwangu

Roho inaniuma baba kafa kanipambania mwanae nisome leo baba kafa ikiwa hata hajala mkono wangu nikiwa still napambana kupata kazi

Nimebaki yatima mimi
Pole sana kwa kumpoteza mzazi wako. Tumwombee mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake pema peponi.
Wewe kubali kazi ya Mungu lakini uendelee kumuenzi mzazi wako hata kama hayupo nawe tena. Kila ulifanyalo, jiulize kama lingemfurahisha iwapo angekuwa hai; utapata baraka zaidi.
 
Nimempoteza baba yangu mzazi

Sijui hata nisemeje

Baba ndo.alikua kila kitu kwangu

Roho inaniuma baba kafa kanipambania mwanae nisome leo baba kafa ikiwa hata hajala mkono wangu nikiwa still napambana kupata kazi

Nimebaki yatima mimi
Pole sana kupoteza,

Ila usisahau kuwa Yesu ndiye Kila kitu, hata baada ya kupoteza baba Bado maisha yataendelea, Yeye ndiye baba wa Yatima.

Tafuta Mchungaji mwaminifu mwenye BUSARA ya Mungu, Mwombe awe baba Yako wa kiroho,

Utapata faraja ya Mungu kupitia mtumishi wake.

Ubarikiwe 🙏
 
Back
Top Bottom