nimempenda kanisani

nimempenda kanisani

Joined
Feb 15, 2013
Posts
9
Reaction score
2
mimi ni kijana wa miaka 20 nimempenda msichana mmoja kanisani, na naamini nimempenda kutokana hata nikiwa nyumbani huwa sura yake inanijia, tatizo sijui nitamwanzaje kanisani pale na muda wote saa ya kutoka nikimsubiri huwaga na mama yake nahisi hawaachani, mnanishauri nifanye nini maana sijui jina lake wala sina namba yake
 
jikaze dogo. talk nae japo jiandae kula bakora za kutosha ukikamatwa.
 
Jipange lakini kabla ya yote tumia macho ili agundue feelings zako kwanza
 
sasa kama una miaka 20 yy ana umri gani! inaonyesha huyo msichana bdo mdogo ndio maana anatembea na mama yake.
 
Hivi kanisani huwa mnaenda kusali au kutafuta wachumba, sikujua kama kanisani mnaweza kutongozana:biggrin:
 
mimi ni kijana wa miaka 20 nimempenda msichana mmoja kanisani, na naamini nimempenda kutokana hata nikiwa nyumbani huwa sura yake inanijia, tatizo sijui nitamwanzaje kanisani pale na muda wote saa ya kutoka nikimsubiri huwaga na mama yake nahisi hawaachani, mnanishauri nifanye nini maana sijui jina lake wala sina namba yake

Kupenda siyo kitu kibaya, inategemea na kuwa umempenda kwa malengo gani. Kwa maelezo yako na umri wako, inaonyesha wazi kuwa unamtaka kingono. Nakushauri achana na hayo mawazo, tumia Kanisa kusikiliza neno la Mungu na kulitii maana huko kila siku wanapiga kelele watu waache ngono au wavumilie mpaka umri wa kuoa ufike ili wafuate taratibu zinazokubalika. Sijui mwanangu huwa hausikilizagi mahubiri au unakuwaga bize kuangalia vimwana wakati wa kwenda kutoa sadaka na wakati wa kutoka?
 
Duh, hope amekuelewa coz wakat wa sadaka nao una mambo?Shetani ndo anapo jaribu kuwainua wajeruhia wake! Dogo, mwache binti wa watu afurahie joto la mama ...
 
dah! hivi matokeo ya form six ni lini tena jamani??

huyo ni miongoni mwa tinejaz wanaobalehe vibaya asikusumbue kichwa.alichonikera ni ile kwenda sehemu ya ibada akiwaza ushetani wake.at his age angetakiwa awe mtu anapambana kujijenga yeye na hiyo jamii yake anayofikiria kuianzisha.hajui hata kutofautisha kupenda na kutamani...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom