Achana na hizo insecurities mzee zitaharibu mahusiano yako.
Yani wewe ununue zawadi na bado uumize kichwa kama kazipenda au lah,
Hupaswi kujiuliza maswali kama hayo Mkuu, ataona hujiamini kabisa na mwanaume asiyejiamini hapendwi na Mwanamke yyte confidence ni namba moja anachovutiwa nacho mwanamke kutoka kwa mwanaume.
Haijalishi, kama hajaipenda hiyo zawadi wewe haikuhusu.
Kama umempa zawadi na hajazipenda wewe haikuhusu piga kimya acha kuanza kumlamba lamba ..
Acha ku-seek validation mkuu.. ameshakwambia "nimepata zawadi thanks" . Sasa kwani i uwe na wasiwasi mkuu, maana yake hujiamnini ...?
Ishu yako sio big deal lakini unaifanya hivyo kwa kujijaza uwoga na wasi wasi usio na msingi, umetingishwa kidogo unaanza kuweweseka mkuu
Mwanamke anyekupenda kutoka moyoni hata ukimnunulia ubuyu kama zawadi umepitia ofcn kwake mfano na kumpa atafurahi sana kwani kwa upendo alio nao kwako utamfanya aweze kushukuru hata kwa vitu vidogo...
So acha kusikiliza ushauri sijuo wa zawadi za funguo za gari, iPhones etc. Upendo wa kweli haununuliwi unatokana na hisia alizonazo mtu juu yako... wangapi wamewagharamia hadi kuwasomesha wachumba na wakaachwaKwenye mataa...
Chakufanya Kwa kuwa ameamua kukaa kimya na wewe piga kimya.. maana ulishajaribu kumuuliza nini kimemsibu.
Atakapoona kimya atajirudi na kukutafuta lakini kwasasa endelea kuakazana na biashara zako mkuu...