Nimemkumbuka Mwalimu wangu aliyeungua moto kwa kulipukiwa na petrol ndani

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,746
Hii habari nilikuja kuipata siku niliporudi kijijini baada ya kumaliza shule kama miaka 2 hivi tangu niondoke kijijini.

Alikuwa ni mwalimu wa kike aliyejiingiza kwenye biashara ya kuuza kashata hapo shuleni na baadaye petrol kipindi nasoma.

Kwajinsi nilivosimuliwa ilikuwa muda wa jioni baada ya muda wa masomo kuisha aliporudi kwenye zile nyumba zao wanazoishi, kuna mtoto alienda na kuhitaji petrol sasa wakati anapima haijulikani hasa ilikuwaje, ila alilipukiwa na petrol usoni na kumuunguza uso vibaya mno.

Alipelekwa hospitali lakini mdogo wangu ananisimulia kwamba shule nzima walienda hospitali kwa mguu ni zaidi ya kilometa 30 kufika hospitali, mdogo wangu ananiambia huyo mwalimu aliungua usoni vibaya pia alikuwa analia sana.

Sijajua kama aliweza kurudi tena kazini maana hukurudigi tena shuleni alipokuwa anatufundisha.

Maishani kuna wakati tunatamani turudishe muda nyuma kidogo ili tusifanye tena makosa ila ndo hivo haiwezekani tena.
 
Back
Top Bottom