Nimemkamata mwizi wa Taa (balbu) usiku wa leo

Mngetakiwa mvunje mguu au mkono au mkaten na mapanga alafu hao walinz nao mngewachanganya kwa kipigo lao moja tu inakuwaje mnaibiwa nawao wako tu alafu ET mkawakabiz mwiz mwiz hakabiziw anatandikwa vizur
 
Hayo yote tumeyakumbuka badae et
 
Your Id reminds me of "SITREP...over"
Back to your comment ,Vijana wa siku hizi wameweka "pesa" mbele kabla ya chochote hata akufumanie na mkewe utasikia
"UNA KIASI GANI TUMALIZANE?"
Ha ha ha! Kwa uzoefu wangu kitu ambacho nahisi walinzi walifanya
Walimsachi na kuchukua kila kitu alichoiba/
Walimpiga faini (ela ya betri) na kama alitoa kiasi kikubwa walimwacha.

Pia huyo jamaa huenda nae ni sungusungu.
 
Kwa hiyo kaambulia vichwa viwili na mkamwachia jaba lililojaa taa akatokomea kusikojulikana............
 
Kuna mwizi nilimdaka hakuamini ...maaana alikuja kuiba kuku kwenye banda langu sasa mbwa wa jirani walilia sana machale yakanicheza nikatoka kimya kimya jamaa anahangaika kukamata kuku mm nilimpa kichapo kimya kimya sema alichoropoka ila kile kipisi cha nondo kilimpa nundu za kutosha.
 
Inashangaza na inaskitisha...

Ilikua ni majira ya usiku saa saba na ushee usinigzi uligoma kabisa nilikuwa naumwa, tumbo lilikuwa linasokota nikatoka nje kuskilizia maumivu, sasa nikiwa nmekaa kwenye maua yaliyostawi niliona kwa jirani yangu taa za nyumba yake zimeanza kuzima moja baada ya nyingine.

Baadae hapo hapo kwa jirani kulikuwa na taa kubwa ameiweka nyuma ya nyumba nikamuona mtu akielekea kuifuata hiyo taa alipofika eneo ilipo huku mimi nausoma mchezo, taa ilikuwa juu zaidi taa ilizima ghafla jamaa alikua ameshikilia ndoo ndogo ambapo akitoa taa anatumbukiza kwenye hiyo ndoo na fimbo ndefu yenye kimduwala juu

Fimbo imefungiwa chupa la maji lililokatwa likawa na shimo hakuna taa inayoruka ina maana taa inasonteshewa fimbo inakandamizwa na kuchekecha kidogo basii taa inakua imetoka inabakia kwenye li chupa

Basi alitoka hapo nikamuona anaelekea kwangu moja kwa moja nyuma ya nyumba nikafuata taratibu amekalia kuangalia taa nikatokea nyuma yake nikamkaba nikamwambia TULIA UTAKUFA akawa mpole akaanza kujitetea, kwanza karibia mtaa mzima ukua giza utafikiri hatuna luku.

Nikachukua tukaongozana kwa jirani nikamuita jirani akaamka akauliza kuna nini usiku huu? Nkamuuliza hauna luku mbona giza, akasema mbona taa za ndani zinawaka labda zitakua zimeungua, nikawambia huyu hapa mwizi wa taa zako.

Jamaa alipigwa vichwa viwili akaulizwa huwa unapeleka wapi alijibu fasta huwa napeleka machimboni nauza bei ndogo, anasema ikijaa ndoo ndogo ninayozunguka nayo mitaani naenda kumimina kwenye ndoo kubwa (diaba) nililolipaki sehemu, aisee tulimpiga tukaongozana akatupeleka lilipo lindoo likubwa, taa zilikua nyingi kwakweli.

Tukaamua tumpeleke police tukiwa njiani kuelekea huko njiani tukawekwa chini ya ulinzi na walinzi wa mitaani tukaelezea mwanzo mwisho wakatuelewa maana kidhibiti alikua nacho mwizi, tulirudi kulala walinzi tukawakabidhi mtu huyo ndio walimpeleka polisi.

Yuda Exalioth
Natumia Jamiiforums
Karibuni Geita.
"inasonteshewa" hahaha
Karibu sumbawanga bro.
 
Kuna mwizi nilimdaka hakuamini ...maaana alikuja kuiba kuku kwenye banda langu sasa mbwa wa jirani walilia sana machale yakanicheza nikatoka kimya kimya jamaa anahangaika kukamata kuku mm nilimpa kichapo kimya kimya sema alichoropoka ila kile kipisi cha nondo kilimpa nundu za kutosha.
Alienda kujitibu huko hahaha
 
Kwa hiyo kaambulia vichwa viwili na mkamwachia jaba lililojaa taa akatokomea kusikojulikana............
Sio vichwa viwili vingi sana sema jirani yangu ni mzoefu kwa vichwa aisee,, tulichoka kupiga tukawaachia polisi jamii
 
Back
Top Bottom