Nimemiss shule ya msingi jamani

Hivi wale wa mazingaombwe shuleni sijui bado wapo...dah kuna siku niliingia nikalipa 100 ...basi akafanya mazingaombwe zikatoka ela nikaokota..kutoka nje nikaenda kwenye juisi ya ndoo kupimiwa glas..nikainywa...kuzama mfukoni ela imeyeyuka...daaa ikabidi nimpe saund mwenye juisi kwamba ntakuletea kesho..kwa kuwa anakujaga hapo marakwa mara akanielewa..ile ni miradi ya walimu tu.
 
Daah kitambo Profesa Singira,pia power Mabura,power Iranda....
 
kama leo nimepita karibu na shule nimetamani kweli uanafunzi,kama miaka ingekuwa inarudi nyuma!
 
Nimeona kuna mwanafunzi muislam kavaa ushungi aiseee
 

Hahaaaa... mkuu umenikumbusha mbali sana,zamani ilikua katikati ya vipindi inagongwa kengele mnatoka kwenda kutambulishwa mwanamazingaombwe...anapiga intro kidogo then mnarudi class hadi siku ya show kwa mwenye hela... sie wengine tunaishia nje tukidubiria fungulia dog
 
Nimeona kuna mwanafunzi muislam kavaa ushungi aiseee


Daah! Nakumbuka nikiwa Form Nyoya sio s/msingi
sasa wanafunzi wengi wakike walikuwa wanatinga Hijabu(ushungi) sasa kuna ticha mmoja sijui alijisikia nini siku hiyo
si akamfunua mmoja akakuta wigi wapili kasuka Rasta tulikuwa paled walinuliwa wooote walikula stick kisha hakuna kuvaa ushungi!!
 
Enzi za mashindano ya ngoma sarakasi kwaya ngojera na vichekesho
What a beautiful flashback
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…