JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,968
Nilimuwekea utaratibu mpenzi wangu wa kuchukua mahitaji yake katika maduka ya rafiki zangu kadri anavyohitaji halafu nikipata pesa naenda kulipa,
Akijisikia vipodozi ataenda kwa Roja na kuchukua, akiona nguo zinapungua basi atakimbilia kwa Beka napo akiugua ataenda kutibiwa kwa Rich na dawa kuchukua kwa Sarafina.
Tukaja kuingia mgogoro katika penzi letu, nikachukua juhudi kulimaliza halikuisha tukaachana, wakati tunaachana tayari alishatengeneza deni la kama laki 6, nilitamani kumwambia akalipe na deni lake lakini nikaona si sahihi kwa kuwa alitumia fursa akiwa katika himaya yangu,
Nimejikongoja kulipa hilo deni na hatimaye wiki ilopita nimefanikiwa kulimaliza, ndiyo nimelimaliza lakini kwa uchungu mkubwa.