Nimelazimika kukubaliana na Kagame katika hili!

Nimelazimika kukubaliana na Kagame katika hili!

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Jana rais aliyezushiwa kifo Paul Kagame alijitokeza hadharani kuongea taifa lake. Kagame hakuongelea hata kidogo uzushi wa kifo chake bali wale aliowaita wasaliti wa taifa lake.

Amesema yoyote anayesalita taifa lake atakiona cha moto! Amedai kuna watu wameshiba wakasahau walikotoka. Amesisitiza hata wale ambao hawajifikiwa wasijione salama maana ni suala la muda tu!

Kagame ameyasema hayo, huku ikiwa ni juzi tu kanali Kalegeya akiwa ameuawa hotelini Afrika kusini.

Kagame hana mchezo na WASALITI!!!!!
 
Mkuu sijakuelewa hapo una halalisha nini?PK is your role modal?hivi unajua maana halisi ya neno usaliti au uhaini?-Nenda korea ndo utapata maana yake
Katika enzi hizi za zama za democracy and diplomacy all over the world ,Maisha anayoyaishi dictator PK,Museven mwisho wa maisha yao huhitaji Shekhe Yahya kukutafsiria
Pk ni suspect na source no 1 wa mauaji yote yaliyowahi kutokea Rwanda kuanzia ya kimbali(genocide) hadi yanayoendelea ndani ,nje Congo(M23) na hata maadui wake ambao wanamsema vibaya hadharani(usiombe itokee tanz Rais anaitwa dhaifu hadharani the mnakutana kama kawaida mnagonga mvinyo)
 
Akwendee kulee nae huyoo awatishe nyau wa nyumban kwakeeeee
 
Bahati mbaya sana kwa watu wengi ni rahisi sana kuona mapungufu ya m2 mmoja na kudhani kuwa amekuwa mkatili sana kuliko mtu yeyote duniani,mifano ipo hai nchi za uarabuni, walimtoa Saddam Husein kwa vigezo hivyo hivyo,nchi ilikuwa imetulia, leo angalia ni watu wangapi wanauawa kila siku?, Gaddaf, Misri n.k. Upo wakati mtawala lazima awatafute na kuwafikia wale wote wapinga demokrasia popote walipo na kuwashughulikia
 
Unajua rwanda iko katika healing process kutoka katika genocide,kuna watu wanao feel gilt na kuna wengine wanaotaka kulipiza kisasi,pk na serikali yake wana work hard ili pasitokee tena genocide nchini rwanda,sasa kuna watu wanaoangalia matumbo yao binafsi wanaotaka kukwaza hiyo process ndio maana wanyarwanda wakiongozwa na rais wao mpendwa hawata kubali kurudi enzi za genocide,wanyarwanda wanajua wazi kua kuna watu wasio watakia amani just kwasababu hawapendi watusi tu.
 
Mmegeuza genocide kuwa mtaji!

Sometimes nawashangaa watu wanaosema genocide ni mtaji,je ungefurahi watusi kulipiza kisasi kwa wahutu?nafikiri watusi hawakushindwa kuwafyeka wahutu wote kutokana na waliyo yafanya,lakini hawa kufuata njia hiyo sasa kuna watu wanao taka second genocide itokee,na pk hataki hilo litokee,ni pk pekee aliyeweza kuzuia revange,sasa kuna watu wanatamani aondoke ili machafuko kama yaliyotokea 1994 dhidi ya watusi yarudie kutokea,tunaomba mungu atuepushe na hilo janga.
 
Jana rais aliyezushiwa kifo Paul Kagame alijitokeza hadharani kuongea taifa lake. Kagame hakuongelea hata kidogo uzushi wa kifo chake bali wale aliowaita wasaliti wa taifa lake.

Amesema yoyote anayesalita taifa lake atakiona cha moto! Amedai kuna watu wameshiba wakasahau walikotoka. Amesisitiza hata wale ambao hawajifikiwa wasijione salama maana ni suala la muda tu!

Kagame ameyasema hayo, huku ikiwa ni juzi tu kanali Kalegeya akiwa ameuawa hotelini Afrika kusini.

Kagame hana mchezo na WASALITI!!!!!
With time, utakubaliana na PK katika mambo mengi sana. To me personally, ukiondoa mambo yake ya mavita na political prisoners, PK namkubali sana. Hachekei uozo wala rushwa. Viva PK
 
Kwa sasa si rahisi ku'revenge' wakati macho ya dunia yako Rwanda. Lakini unaweza kutueleza nani aliyefanya ile 'genocide' ya Wahutu kule Kongo ya Mashariki wakati wa vita vya Banyamulenge kumwondoa Mobutu Seseseko?
 
Kichwani linabaki swali iwapo pk amefanya 'genocide' kuwa mtaji wa kubaki madarakani na kuonewa huruma na ulimwengu au la. Lakini lililo wazi, anayo hari ya kweli ya kuijenga nchi yake kiuchumi kwa nguvu zote. Anayeonekana kutaka kupunguza spidi ya pk au kumsimamisha katika mwelekeo huo, hakuna msamaha! 'It is another extreme in comparison to our leaders here but we Tanzanians have something to learn and gain from this!'
 
Kagame lazima atachukiwa tu kwa sababu hela ya anayopata iwe halali au haramu anajengea nchi badala ya kustarehe kama walivyokua wanategemea hao wenzake kina kalegeya. Tofauti na nchi nyingine kama Congo viongozi wanafanya matanuzi ya kufa mtu (kama hujawahi fika kinshasa usibishe!) hadi wanalisahau jeshi mpaka linakua weak mno na kuvamiwa na vikundi vidogo vidogo. Makosa yale yale ya Mobutu wanayarudia na isingekua kusaidiwa Congo kuna siku ingepigwa na M23 mpaka Lugumbashi sio Goma tu kwa uzembe. (Usiombee na Tanzania tufikie uzembe huo ingawa sidhani, tunalijali sana jeshi.)

Watu kama kina kanali Kalegeya ni wasaliti kweli kwasababu hao walikua watu wa karibu wa Kagame kwa hiyo kama Mauaji walifanya wote! Lakini wana m_demonize Kagame as if wao hawakuua. Ukiishi kwa Upanga utakufa kwa Upanga. Kagame naye zamu yake itafika but until then acha awaonyeshe mfano hawa wanasiasa jinsi kujenga nchi na kudeal na wala rushwa na treasoners.

Demokrasia na Siasa nyingi kwa nchi changa sometimes ni Majanga tu.
 
I owe you a drink, bossman!
 
Back
Top Bottom