Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 42,099
- 12,919
Juzi baada ya saa za kazi, nikiwa naondoka ofisini nilikuta akina dada wa hapa ofisini getini wakinunua machungwa. Nikamuomba dada mmoja kwa kumwambia naomba "Tukatiane" chungwa aliloshika mkononi. Ajabu watu waliosikia waliangua kicheko. Sasa imekuwa kero kila mtu anayeniona ktk korido za ofisi hasa wasichana salamu zao huwa "Tukatiane", hata nikiwa mbali mijitu inapaza sauti "TUKATIANE"