Nimekutana uso kwa uso na jirani akichungulia nyumbani kwetu 😒

Nimekutana uso kwa uso na jirani akichungulia nyumbani kwetu 😒

Binti wa zamani

Platinum Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
11,763
Reaction score
27,149
Huyu jirani yetu ni baba ni mtu mzima, tumepakana naye, na mara nyingi mida ya jioni anapenda kukaa kibarazani kwake juu ghorofani, na tushamzoea hivyo.

Usiku wa leo niko narudishia mapazia, ghafla namuona na binoculars (zile za kuonea mbali) ameelekeza huku kwangu anatuangalia na baada ya kuniona wala hajashtuka ameendelea tu kuangalia.

Sasa sijaelewa alikua anafanya vile kwa lengo gani, tumeongea na mtoto wake kwa simu ili amuulize maana niko mwenyewe na vijana wadogo tu na sikutaka kwenda hapo kwake usiku.

  1. Ingekua wewe kwenye hii situation ungefanyaje?
  2. Na vipi ushawahi kua na jirani ambaye ni kipengele? ilikuwaje ?
 
Kwa asiyejua binoculars ni hivyo vidude

Screenshot 2025-12-29 at 21.50.07.png
 
Anhaaa jirani pole bhana, nilikuwa natazama mandhari ya mazingira hapo kwako kiukweli unajua sana kupamba nyumba na nimefurahi kuona pia wewe umeniona

Kwa maana niliona haina haja ya kujificha tayari ushaniona au unadhani nitakuibia jirani??
 
Huyu jirani yetu ni baba ni mtu mzima, tumepakana naye, na mara nyingi mida ya jioni anapenda kukaa kibarazani kwake juu ghorofani, na tushamzoea hivyo.

Usiku wa leo niko narudishia mapazia, ghafla namuona na binoculars (zile za kuonea mbali) ameelekeza huku kwangu anatuangalia na baada ya kuniona wala hajashtuka ameendelea tu kuangalia.

Sasa sijaelewa alikua anafanya vile kwa lengo gani, tumeongea na mtoto wake kwa simu ili amuulize maana niko mwenyewe na vijana wadogo tu na sikutaka kwenda hapo kwake usiku.

  1. Ingekua wewe kwenye hii situation ungefanyaje?
  2. Na vipi ushawahi kua na jirani ambaye ni kipengele? ilikuwaje ?

Kupata stimu😎

1. Namumkaribisha kabisa
2. Mie ndio jirani kipengele, ninepiga sana chabo
 
Anhaaa jirani pole bhana, nilikuwa natazama mandhari ya mazingira hapo kwako kiukweli unajua sana kupamba nyumba na
Wewe mzee una shida mahali
nimefurahi kuona pia wewe umeniona, Kwa maana niliona haina haja ya kujificha tayari ushaniona au unadhani nitakuibia jirani??
Kwanza leo nilikua na siku ya hovyo, halafu nakutana na huu ujinga wako umenikera sana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom