Nimekutana na wahitimu 2 wa chuo kikuu wakifanya ujasiriamali Kariakoo mtaa wa Kongo kwa mtaji usiozidi elfu hamsini. Aibu kwa taifa

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
1,947
2,000
Huku Tanzania ikipaa kiuchumi na sasa tuko kwenye uchumi wa kati.

Mwaka jana mwezi nimeusahau ila nikicheki kwenye kumbukumbu zangu ninaweza kujua mwezi,tarehe na hata saa nikiwa na wife tulipokuwa tunazuguka Kariakoo, nikasikia sauti nikiitwa kwa jina langu. Nikamwona kijana akinichangamkia.

Kumbe ni school mate kashikia mikanda 3 ronyaronya akiwarubuni watu kuwa ni ya ngozi. Ile mikanda inauzwa elfu 2 mmoja wao huuza elfu 3-5. Imagine mikanda 3 huo ni mtaji wa elfu 6.

Nilishindwa kuamini kuwa ni yeye maana nilipochati naye about 3 or 2 yrs back aliniambia yuko Chuo kikuu huko Iringa, nilishangaa kuwa ni yeye!

Nikamuuliza swali la mtego huku nikimuonea huruma. "Vipi Iringa umeondoka lini"? Akaniambia tangu mwaka juzi nilipomaliza Chuo. Nikajisikia hudhuni sana, nilimpa namba anitafute nimpige tafu hajanitafuta mpaka leo mwaka umepita.

Jana tena nimekutana na graduate mwingine niliyesoma naye O -level huku akiwa na kibegi chenye bidhaa chache na zisizo na thamani kubwa akielekea kazini Kariakoo, huyu anaonyesha utayari. Nitamsaidia kadri ya uwezo wangu.

Serikali mnatesa vijana, mtu asome Chuo Kikuu miaka 3 akauze mikanda barabarani Kariakoo?
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
7,683
2,000
Huku Tanzania ikipaa kiuchumi na sasa tuko kwenye uchumi wa kati.

Mwaka jana mwezi nimeusahau ila nikicheki kwenye kumbukumbu zangu ninaweza kujua mwezi,tarehe na hata saa nikiwa na wife tulipokuwa tunazuguka Kariakoo, nikasikia sauti nikiitwa kwa jina langu. Nikamwona kijana akinichangamkia...
Mpongeze kwa uthubutu, kupata wazo la biashara hiyo, ni ngumu sana kwa wengi wetu kuthubutu na ku come up na idea hata kama una mtaji wa Mil.10!!
 

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
983
1,000
Graduates wana shida aisee kila anachofanya anakosea akienda kuajiriwa motivation speakers wanamuambia huko siko hakuna utajiri, akitulia home ataambiwa dogo hajielewi anashindwa kujiongeza, akiingia mtaani kutafuta chochote kitu anaonekana kama kashapotea huyu.

Muhimu : Wengi wanaodiss harakati za graduates hawajawahi kuingia hata UE moja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom