TAARIFA FUPI YA WANAFUNZI WA DIPLOMA MAALUMU CHUO KIKUU CHA DODOMA KWA WATANZANIA NA SEREKALI
UTANGULIZI
Katika kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika shule za sekondari nchini Wizara ya elimu na Mafunzo ya ufundi kushirikiana na chuo Kikuu Cha Dodoma pamoja na baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) Iliandaa mafunzo ya stashahada maalumu ya ualimu katika sayansi,technolojia, na hisabati kwa wahitimu wa kidato cha nne.
Katika kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika shule za sekondari nchini Wizara ya elimu na Mafunzo ya ufundi kushirikiana na chuo Kikuu Cha Dodoma pamoja na baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) Iliandaa mafunzo ya stashahada maalumu ya ualimu katika sayansi,technolojia, na hisabati kwa wahitimu wa kidato cha nne na wenye sifa mbadala.
Mafunzo haya yanatolewa na Chuo kikuu cha Dodoma ,chuo cha elimu.Mafunzo haya yanafuata mfumo wa Tuzo za elimu ya Ufundi(NTA) unaoratibiwa na NACTE ikilenga kumuwezesha muhitimu wa kidato cha nne kupata mafunzo maalumu.Katika miaka hiyo mitatu chuoni mwanafunzi anasoma masomo yake mawili ya kufundishia katika kiwango cha kidato cha tano na sita.
Wakati Magufuli akiwa Mbunge na Waziri na Kikwete akiwa Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2014 Serekali ili wasilisha Bungeni mswada wa Sheria Na 14 ya mwaka 2014 ilikuruhusu wanafunzi hao wadahiliwe .Mswada wa sheria hiyo ulisainiwa Novemba 2014 na aliyekuwa Rais Jakaya Mrisho KIkwete
UDAHILI
Katika kudahili wanafunzi waliodahiliwa palikuwa na makundi mawili .
1;Waliokuwa wametoka kidato cha nne kwa mwaka huo 2014.(fresh from school)ambao wao hawakuomba kujiunga na program hii walipangiwa moja kwa moja Chuoni wakiwa na ufaulu wakuanzia Divition 3 lakini wakiwa na ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi .Katika hawa wenye div 3 wapo wengi waliokuwa na sifa ya kwenda kidato cha tano lakini serekali kwa kujua na kwa makusudi waliamua kutowapangia kidato cha tano ili kuwaleta kwenye ualimu.
2;Walikuwa ni wale waliomba kupitia NACTE au Wizara ya elimu wakiwa na sifa mbalimbali,mfano waliomaliza kidato cha nne miaka ya nyuma kwasababu moja au nyingine walishindwa kuendelea lakini walikuwa na sifa kama hao waliotoka shule moja kwa moja,kuna waliofeli kidato cha sita lakini kidato cha nne walifaulu vizuri kwa Div 1 na 2.Mbali na hilo wapo pia waliokuwa wamedahiliwa na kuanza kidato cha tano lakini kwakujua hii ni fursa nzuri waliomba nakuachana na kidato cha tano wakaja kujiunga na program hii.
Sasa katika hizi sifa mbadala wapo waliokuwa na ufaulu wa kiwango cha Div 4 wakiwa na D nne au zaidi au na credit ikizingatiwa kuwepo katika masomo ya sayansi kama hesabu,biology,kemia na physics lakini watakiwa kuwa na sifa ya ziada katika fani mbali mbali za sayansi kama Kompyuta,umeme,ubaharia,kilimo,nursing,misitu,maabara,uzoefu wa ualimu katika masomo ya sayansi(in service) n.k
Pale ambapo muombaji hakukidhi haja au sifa ya kusomea ualimu wa sekondari alipangiwa kujiunga na program hii lakini katika Diploma ya ualimu wa shule za msingi ambayo ni moja wapo ya program hii ya kuongeza walimu wa sayansi na ambayo ilikuwa ikienda sambamba na hii ya walimu wa sekondari na wakipata mkopo kutoka bodi ya mikopo sawa na wengine.Kwa hiyo watu wanapozungumzia waliorudishwa nyumbani wasiwasahau hawa wanaosomea ualimu wa Primary na wao walidahiliwa kwakuzingatia uafaulu kidato cha nne kwa masomo ya sayansi.Wao jumla yao walikuwa kama mitano hivi.
Kwa waliodahiliwa Kusomea ualimu wa sekondari walipangiwa kozi kulingana na ufaulu wao katika masomo yake mawili na hayo ndio yangekuwa masomo yake yakwenda kufundishia mfano aliyefaulu vizuri Physics na Hesabu alipangiwa kusoma kozi ya PME(Physics,Mathematics and education) wakati wengine walipangiwa CME,CBE,PCE,MIE(C=CHEMISTRY,M=MATH,PHYSICS,I=INFORMATION AND COMUNICATION TECHNOLOGY,B=BIOLOGY)Na masomo haya yote wanasoma katika kiwango cha Advance au kidato cha tano na sita.Wale wanaosoma ualimu wa Primary wao wanasoma masomo yote ya sayansi ya shule za msingi.
HISTORIA FUPI YA KURUDISHWA NYUMBANI KWA WANAFUNZI WA SPECIAL DIPLOMA
Hili suala limeanza muda mrefu na haya yaliyotokea ni matokeo ya muda mrefu wa madai ya walimu.Kuanzia kwa semester ya kwanza mwezi wa 11 mwaka jana lilionekana kuwepo na kamgomo ambacho hakikuwa rasmi ambacho dalili yake ni maudhurio mabaya kwa baadhi ya walimu madarasani.Lakini katika semester hii ya pili wiki za mwanzoni walimu baadhi waliingia madarasani huku wengi wao wakitoa visingizio mbali mbali bilakueleza ukweli kuwa wapo katika mgomo.Mpaka kuondolewa kwa wanafunzi hawa wa Diploma kuna kozi hawakuwa wamesoma
Kufikia wiki ya 6 ambayo ndio wiki ya mwisho katika kuanza kujiandaa na Test za mwisho ndipo wanafunzi tuliposhituka kuona hakuna mwalimu anayeingia kufundisha na baada ya kufuatili ikagundulika wapo katika mgomo wakudai malipo yao na stahiki zao mbalimbali.
Katika madai ya walimu moja ni chuo kutaka kuwalipa kwa lectures badala ya stream au mkondo.Ina maana kwa maelezo yao walimu ni kuwa hii program wanafundisha kama kazi ya ziada mbali na ile walioajiriwa nayo katika kuwafundisha wa degree,kwahiyo katika mapatano yao kama wanavyodai wao nikuwa lecture inalipwa kwa mkondo mmoja ambao kwa wastani unakuwa na wanafunzi wapatao 80 lakini matokeo yake kulingana na VENUE au madarasa mpanga ratiba baadhi ya lecture aliunganisha madarasa au mikondo zaidi ya mmoja na ndio malipo walitaka kuwalipa kwa lecture moja pamoja nakuwa amefundisha mikondo zaidi ya mmoja ambacho ni tofauti na mapatano yao.
Lakini ukiacha hilo wanamadai ya vitendea kazi vichache kama projector,maker pen,duster na kemikali kwaajili ya majaribio ya kisayansi jambo ambalo linasababisha ufundishaji wao hasa practicle kutofanyika kama inavyotakiwa.Na hili wanafunzi wanalielewa vizuri kwasababu wale wanaosoma biology semester iliyopita ya kwanza walitakiwa kufanya particle 6 wakafanya moja na wengine 2 tu.Ila chakusikitisha ni pale walimu walipokuwa wakiingia madarasani hawana duster wala makerpen wanafunzi wakiwasaidia ili waweze kufundishwa na wakati mwingine wanafunzi viongozi wa madarasa iliwabidi kuwa na duster na makerpen kwa tahadhari hiyo.
Lakini kubwa kuliko yote ni hili la wanafunzi wa mwaka wa pili kutoenda field au Teaching Practice au mazoezi kivitendo kama inavyoelekezwa kuwa walipaswa kwenda field mwaka wa kwanza na wapili.
Jumamosi tar 28/5 ndipo yalipobandikwa matangazo yakiwataka wanafunzi wote tuondoka maeneo ya chuo mwisho saa 12 jion ya siku ya jumapili tar 29/5,Katika Tangazo hilo hapakuwa na maelezo ya sababu yakufanya hivyo wala muda wakurudi chuoni huku likionyesha kuwa limetolewa na mkuu wa chuo..Kwa namna na utaratibu wakuwaondoa wanafunzi chuoni haukuwa mzuri na kwamaana hiyo hili limetafisiriwa kama KUFUKUZWA KWA WANAFUNZI WA DIPLOMA YA UALIMU kwasababu hawakupewa muda wa kujiandaa kwa nauli kwasababu wengi wanatoka katika familia maskini lakini pia wengi wanaumri mdogo ambao hilo lingeweza kuwa jambo la hatari kwao.
MAELEZO YA WAZIRI NGALICHAKO NA RAIS MAGUFULI
Kwa maelezo ya waziri Ngalichako Bungeni na Maelezo ya Rais Magufuli alipokuwa akihutubia wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam yanapingana sana.Kwa mujibu wa Waziri wa Elimu ni kwamba mwanafunzi wa special Diploma waliofukuzwa udom hawakuwa na makosa ispokuwa wameondolewa chuoni baada ya kukaa muda mrefu bila kusoma kutokana na mgomo wa walimu wao ambao wameshindwa kuafikiana baadhi ya madai yao na serekali haiwezi kumuingilia mkaguzi wa ndani wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
Rais Magufuli yeye anasema hao wengi vilaza na walidahiliwa bila sifa na wengine ni watoto wa wakubwa.Akaongeza kuwa wapo waliodahiliwa kuendelea na masomo ya Chuo kikuu wakati wana alama D nne na wanapata mkopo wa serekali wakati wengine wenye sifa wakikosa mkopo,na kama hao waliofukuzwa wangegoma angewafukuza wote.Na akadai wenyesifa yakuendelea ni wale tu wenye Div 1 na 2
Wazazi na wanafunzi wamebaki dailema (dilemma) baada ya hizi kauli mbili za waziri na Rais kupingana
.KInachoonekana hapa huenda ni kama ifuatavyo;
1;Huenda Rais alikuwa hana taarifa sahihi za sakata la hawa Diploma kwa hiyo alishindwa kutofautisha na kuwa specific kuchanganua maelezo yake kwamba wakati huu anazungumzia Special Diploma au wanafunzi wa Saint Joseph kilichofungwa na serekali..
2;HUenda alidanganywa au hakuambiwa ukweli kwasababu Fulani Fulani za wahusika wakiogopa kutumbuliwa.
3;Au alibeba vichwa vya magazeti yetu waliropoka kuwa hawa Diploma wamefukuzwa kwakukosa sifa wakichanganya kati ya hawa Diploma na Wanafunzi wa Saint Joseph.Special diploma wao udahili wao haukufanywa na TCU,udahili wao ulifanywa na NACTE kuzingatia vigezo vilivyoainishwa na katika vigezo hivyo pia palikuwa na kigezo cha ufaulu wa Div 4 kwa wale wenye sifa za ziada kama fani za Ufundi.
Tunaweza kusema bado hakuna kauli inayojitosheleza na yenye kuakisi ukweli katika hili sakata.Natarajia kama patakuwepo na utumbuaji wa wanafunzi wasiokuwa na sifa basi waanze na waliowadahili (NACTE).
TAFAKARI NA MAONI
1;Tumekuwa mashabiki sana wa utumbuaji tunasahau kufikiri na kujiuliza,Ni muhimu kuwa tunatafakari na kuhoji kwakina kwamba sio kila kitu nichakutumbua tu vingine kabla ya kutumbua lazima usikilize pande zote kwanza na kuruhusu busara itumike.Kama leo hii mtu muhimu au mwanao unayemtegemea anatumbuliwa ikiwa hana kazi au kukosa masomo bila kusikilizwa na kupewa kujitetea utajisikiaje?
2;Mfano unaposema wanaoenda Chuo Kikuu lazima wawe na Div 1 au 2 kwa kidato cha sita basi ujue kwa wanafunzi wanaosoma sayansi kwenye mchipuo kama PCB,PCM, PGM nk wengi watakwama na hawa ni watoto wa maskini ambao shule wanazosoma za serekali hazina walimu wakutosha kwa masomo hayo lakini haina maana kuwa ni vilaza.Na hili linajitokeza hata kwa wanafunzi hawa wa Diploma wengi wao watoto wa maskini na wametoka shule zetu za kata zisizo kuwa na walimu wa kutosha nazingine hazina kabisa lakini vijana hawa wa maskini kwakupenda sayansi hawakusita kujitahidi wakapata Div 3 na wengine 4.Pekee nihawa watoto wa maskini wanaopenda ualimu na hata serekali ilipowachagua bila wao kuomba bado walikubali.Ni vigumu kumpata mtu wa sayansi mwenye Div 1 au 2 akakubali kusomea ualimu wa sayansi.
Katika hili tunaomba serekali kwa umakini ingalie pia GPA za wanafunzi hawa walipokuwa chuoni kwasababu wengine pamoja na ufaulu wao kuwa chini kidato cha nne chuoni wameonyesha uwezo mkubwa.AU kama patakuwa na wasiokuwa na sifa kuwa wanafunzi waualimu wa sekondari basi isiwapoteze kwakuwaacha iwapeleke kwenye Diploma ya ualimuwa shule za Msingi.
3;Rais alizungumzia juu ya vyuo vingine vya ualimu kukosa wanafunzi kama vyuo vya Kwimba na vinginevyo.tahadhari hapa ni kwamba sababu kubwa kuletwa chuo kikuu Dodoma ni pamoja na kuzingatia hostel zakutosha ,walimu wakutosha,na miundo mizuri yakufundishia hasa kwa wanao soma masoma ya kompyuta kwa hiyo ayatazame na haya pia.
4;Rais Magufuli alikuwa Bungeni na kikwete ndio aliyesaini huo mswada uliopitishwa na Bunge kwa nini leo wanatugeuka?
HITIMISHO
Tunaunga mkono jitihada za Rais Magufuli kusafisha nchi hii ili tupige hatua kimaendeleo lakini wakati mwingine busara na hekima na ufuatiliaji wa karibu unahitajika kabla ya kuchukua hatua mbali mbali hasa katika sakata hili linalogusa watoto wa maskini WALIOHITIKIA WITO.
Mwisho serekali ituombe radhi kutudhalilisha na kutuita vilaza wakati yenyewe ndio ilitupeleka UDOM tena wengine hata bila kuomba walipangiwa kusoma hii diploma ya ualimu bila ridhaa yao lakini walikubali kwasababu ni watoto wa maskini hawakuwa na jinsi.
TUNAOMBA WATANZANIA KATIKA HILI WASIWE MASHABIKI WAJIHOJI KWANZA KABLA YA KUSHABIKIA