GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,824
- 6,562
Kama utamaduni ni utajiri, Tanzania inao mwingi sana.
Nilikuwa nafahamu kuwa ni sehemu ya utamaduni wa Kimasai wanaume kutoboa masikio. Ndiyo maana nilishangaa nilipokutana na vijana wa Kisukuma wanaovaa hereni.
Hata mahali nilikokutana nao ni mshangao pia. Ni mkoa ambao unaojulikana kuwa wenyeji wake ni Waha. Namaanisha Kigoma.
Hao vijana wa Kisukuma, ambao kwa makadirio ya umri walionekana kuwa walizaliwa miaka ya elfu mbili hivi, walikuwa wamevaa hereni na mibangili mingi.
Nulipowauliza watu wanaoishi karibu nao (majirani zao ni Waha na Wasumbwa, wote wapo Kakonko Kigoma), nilielimishwa kuwa kwa Wasukuma kuvaa hereni na mibangili mkononi, ni ishara ya utajiri wa ng'ombe.
Si kila kijana wa Kisukuma anaruhusiwa kuvaa hivyo. Ni yule tu ambaye kwao kuna utajiri wa ng'ombe. Namna ya uvaaji wa mibangili mkononi na miguuni huonesha kiwango cha utajiri wao. Kwa uvaaji tu wa mibangili, unaweza ukajua idadi ya ng'ombe waliyo nayo kama ni maelfu ya ng'ombe n.k.
Labda, wakati mwingine, wasanii wa Tanzania wanaovaa hereni hawajaiga Wazungu bali wanadumisha utamaduni wao wa asili.
Kwani kuna mtu aliyekuwa anajua kuwa kuna vijana wa kabila la Wasukuma wanaovaa hereni masikioni?