Nimekutana na moja ya CV nzito sana ya Mwanamke msomi.

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
4,538
11,868
ANGALIZO:
bandiko hili liwe chachu kwa watu wote hasahasa wanawake wanaopenda maendeleo ya kielimu.

nimeileta mada hii MMU kwasababu naamini hili ndio jukwaa linalotembelewa sana na wanawake hapa jamiiforum.

huwa navutiwa sana na maendeleo ya wanawake katika masuala ya kitaaluma. navutiwa zaidi hasa pale mwanamke anapoenda hatua moja zaidi kusomea masuala ambayo jamii zetu za kiafrika, zinaamini ni sisi wanaume tu ndio tunaweza.

leo katika pitapita zangu, nimekutana na CV nzito sana ya Mwanamke msomi.
si mwingine, ni mwanaanga Dr. Jeanette Epps ambaye pia ni mhandisi katika shirika la NASA huko marekani.

kilichonivutia zaidi katika CV yake ni kuonyesha kuwa alishawahi kuwa jasusi (intelligence officer) katika shirika la ujasusi la marekani(CIA) akishiriki katika project nyeti mbalimbali za kisayansi za shirika hilo.

jambo lingine lililonivutia katika CV yake ni kuonyesha kuwa ameshiriki kuandika machapisho(publications) mbalimbali ya kisayansi yanayohusu taaluma yake ya uhandisi wa mitambo ya anga za juu.

yapo mengi sana yaliyonivutia katika CV yake, ila kwa uchache ni hayo tu. kwangu huyu ni mwanamke wa shoka.

wale dada zangu wa jf ambao kipaombele chao namba moja ni kuolewa na mwanaume mwenye fedha, nawakaribisha kwa dhati kabisa mpitie CV ya mwanadada huyu. kuna kitu positive mtajifunza.

IMG_20190520_183115.jpeg
IMG_20190520_183209.jpeg
IMG_20190520_183240.jpeg
IMG_20190520_183929.jpeg
IMG_20190520_183857.jpeg
d0e73db0b341c0d7c3ba6b3d69278858.jpeg
 
Ni kweli ila usitarajie kumwambia kitu mwanamke wa hivyo kama ni mkeo

Akiamua siku ufue utafua
Akiamua ukune nazi utakuna nazi!

Kiufupi kila jambo lina uzuri na ubaya wake...mwanamke akisoma ni nzuri ila akisoma sana ni tatizo
 
Back
Top Bottom