Nahisi itakuwa Bagamoyo roadInteresting
hukusema hiyo mitaa ni wapi
Nahisi itakuwa Bagamoyo road
Kawaida tu kwenye dunia yenye Mungu na mashetani yapo tunashukuru hukudhurika poł sana punguza muda wa kurudi uciku km saa10Ndugu zangu mimi sio muumini wa haya mambo, sijui majini wanga siamini kama yapo. Ila leo kuna kitu kimenitokea kinaweza kubadili maoni yangu juu ya hivi viumbe.
Kama mjuavyo mwisho wa wiki huu unapilika nyingi za usiku na mimi leo nilikuwa kwenye misele ya usiku. Sasa wakati narudi mida ya saa kumi na robo hivi alfajiri hii nimeona vitu naona si vya kawaida.
Wakati narudi nyumbani niko peke yangu kwenye gari na barabarani ghafla akatokea paka mweupe anakatiza barabara . Kwa kawaida usiku huwa nakimbiza gari kidogo na ninaendesha katikati ya barabara, basi yule paka katokea upande wa kushoto anakatiza kueleke kulia.
Kwa instict za udereva nikanyunyiza breki kidooogo, nikahamia kushoto alipotoka nikamkwepa bila kashkashi. Kuangalia nyuma kwa kutumia vioo sikumuona yule paka! Kwenda mbele kama mita kumi nikamuona mwanamke wa kizungu 'blonde' kavaa gauni jeusi refu limefunika hadi viatu kasimama upande wa kulia wa barabara!
Nikamwangalia na yeye akaniangalia wakati napta macho yalipogongana mwili wote ukanisisimka! Kwa mazingira yale niliomkuta na muda huu si kawaida kukuta mwanamke kasimama peke yake awe wa kizungu au mswahili, ndugu zanguni huyu ni jini? Nimeandika hii habari kabla sijalala mkiona nipo kimya sana mjue ni athari za huyo 'jini'.
cc: mshana jr
Ha ha haaaa.. Unaijua nauli ya kutoka dar hadi katavi? Half Katavi ni mlisha mifugo nyumbani kwa Pinda kule Mpanda so ticket ya ndege kwa duu kama wewe haezi gharamikia. Unless ujitolee kwa kila kitu
Ukiwa mitaa ya Kigoma na Shinyanga unaweza ukadata ukitembea usiku na gari! Unaweza kukutana na debe ktkt ya barabara linabingirika lenyewe ukilikwepa unalo
Kaa huamini sema "siamini kama majini yapo" period......... usielezee hapa kama wewe ndo msemaji wa mwisho! Majini yapo na yanafanya Yao kama kawaida, Mimi Ni mkristu nilikua siamini hizi mambo, but nilikutana na jini la kike Ana Ana, mpaka Leo linasumbua! Imani kama yako imepelekea shida kwangu coz ilichukua miaka 6 Kuja kuamini na hiyo Ni baada ya uaribifu mkubwa kutokea.....usipotoshe watu hapa, Leo watu wengi wanaishi na majini bila kujua yanaleta shida kubwa but vile wana Mawazo kama yako inawachukua muda kupambana nayo!Hakuna bidhaa ya aina hii katika ulimwengu halisi no something like that exist in the real world
Hofu. woga, paniki na simulizi za uwepo wa majini zilizojazwa ufahamu wako , zilizuia udadisi halisi juu ya ulichokiona.
Ukakimbilia kwenye suluhisho batili.
Katika ulimwengu wa fikra pevu, akili kubwa, great thinkers,
Ambao ndio ulimwengu wa kweli hatuna kitu kama hicho.
Kumbuka 'mawazo' huumba hivyo vitu yaelekea uliviumba au kuvibadili mambo kwa hofu Na yoga
Think twice.
Ukiwa mitaa ya Kigoma na Shinyanga unaweza ukadata ukitembea usiku na gari! Unaweza kukutana na debe ktkt ya barabara linabingirika lenyewe ukilikwepa unalo
Mh hii kitu ilishawahi mtokea mama yangu kipindi nikiwa mdogo, alikutana na nguruwe kama 80 hivi usiku na vimuri muri akapotea njiaUmenikumbusha kuna siku nimetoka bar saa tisa usiku na nilikuwa sijalewa kivile, ile nakaribia nyumbani nikaona watu ambao naweza kusema sio wa kawaida kutokana mwonekano wao.
Na ili nifike nyumbani iliuwa ni lazima nipite pale walipo. Sasa kutokana na pombe zangu na kujiamini nikaendelea kuwasogelea na nilipowakaribia nikawaambia kabisa sasa mi napita hapo hapo kati kati yenu ili mjue mi ni nani, na wenyewe wakasogea pembeni wawili upande wa kushoto na wawili upande wa kulia, nikapita.
Baada ya kupita nikawa najihisi tofauti, kama niko ndotoni hivi! Nikageuka ili niwatukane sikuwaona, nikasema ngoja nitukane hivyo hivyo hata kama siwaoni, sikuweza (ulimi uling'ang'ania juu)
Nikaendelea na safari, ikaanza kunyesha mvua na cha ajabu ile njia nimeizoea lakini nilitafuta njia ya kuchepukia nyumbani sikuiona, nilikuwa nazunguka maeneo yale yale hadi asubuhi saa kumi na mbili kasoro ndio nikafanikiwa.
Ile nafika nyumbani wanashangaa eti kwanini nimeloana, Kumbe ile mvua ilininyeshea mm tu!
Mkuu nimewahi kuisikia hiyo 'kanuni' mara nyingi sana, kwamba unapokuta kitu cha ajabu (au mtu) katikati ya barabara usiku mwingi, USIKWEPE! Nyosha tu ata kama unaenda kukigonga. Eti ukikikwepa tu ni kosa kubwa, inakula kwako, lazima upate bonge la ajari ama ufe.
Kumbe ina ukweli eeh?
Nasikia jini huwa haonekani kwa reflected light eg mirror hata ukimpiga picha haitoki.1. ... "Kuangalia nyuma kwa kutumia vioo sikumuona yule paka!"
Mida ya SAA 10 usiku, sidhani kama inawezekana uone kitu kilichopo nyuma eti kwa kutumia site-mirror or driver-mirror, it is never easy kwenye barabara ya giza! Unless barabara ina mataa au kuna gari lingine nyuma yako linakufuata.
2. Majini ni viumbe. Kama unaamini kuwa SHETANI yupo, basi amini pia kwamba majini yapo.
Haijawahi kunitokea, ila binafsi naamini mambo hayo yapo.
Mkuu nadhania ungekuwa ushapiga 'vyombo' + akili za usiku, walahi huyo blonde ungempa lift. Teh teh
-Kaveli-