Nimekunywa Mo Extra moyo unapiga sana

October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,635
4,995
Wakuu leo nimekunywa Mo Extra ila nashangaa mapigo ya moyo yanapiga sana mpaka sasa hivi, nimekunywa kama masaa 4 yaliyopita. Ila mpaka sasa yanapiga sio full time, ni kwamba moyo unapiga normal inakuja inapiga kama x5 (pupupupupu) nakuwa normal tena inakaa inakuja tena.

Hii inakuwaje maana nishawahi kunywa hichi kinywaji haikuwa hivi.

UPDATE:

Nashukuru wakuu wote, nimechukua ushauri wa kufanya mazoezi nikafanya mazoezi kama nusu saa nilivyomaliza haukupiga tena mpaka leo sasa hivi safi tu.

Sigusi tena hiki kinywaji sio kwa neno kifo lilivyotajwa mara nyingi humu. Nitakirudia kinywaji changu, Apple Punch.

NINI HUTOKEA TUNAPOKUNYWA "ENERGY DRINKS"?
"ENERGY DRINKS" ni vinywaji vinavyotajwa kukuongezea nguvu utakapotumia,na matumizi yake yameongezeka kipindi hiki.

Mwaka 2014 shirika la afya duniani lilivitaja vinywaji vya "ENERGY DRINKS" kuwa ni hatari kwa afya za watumiaji baada ya kutambua ongezeko la watumiaji wa vinywaji hivyo.

Kibiashara vinywaji hivi huuzwa kama vinywaji baridi vyenye uwezo wa ku'boost' utendaji kazi wa akili na mwili, kiungo cha CAFFEINE ni kiungo chenye chachu kubwa sana kwenye vinywaji hivi, lakini kuna watengenezaji wengine wa vinywaji hivi wao huweka viungo kama GINSENG na GUARANA kama mbadala wa CAFFEINE.



MUST-READ: KAMA BADO HUJA'LIKE' PAGE YETU YA FACEBOOK IITWAYO "CLYZ MOOD" LIKE HIVI SASA KUPATA FACTS NYINGI KAMA HIZI,PIA WAALIKE MARAFIKI WA'LIKE' PAGE YETU NA USISITE KUTUACHIA MAONI YAKO HAPA CHINI TAFADHALI.
upload_2017-8-27_23-52-54.png

Kulingana na maelezo ya SAMHSA (SUBSTANCE ABUSE AND MENTAL HEALTH SERVICES ADMINISTRATION) ambayo ni tawi la idara ya afya na huduma za kibinadamu ya MAREKANI yanaeleza kuwa kiasi cha CAFFEINE kilichopo kwenye chupa moja ya "ENERGY DRINK" ni kati ya miligram 80 mpaka miligram 500.Huku kikombe cha kahawa chenye ujazo wa mililita 150 kinatajwa kuwa na CAFFEINE kiasi cha miligram 100 (100mg).

Tafiti kadhaa zinaonesha wazi athari hasi za matumizi ya "ENERGY DRINKS" mfano; Tafiti ya mwaka 2013 ilioripotiwa na mtandao wa MEDICAL NEWS TODAY ilieleza ni kwa namna gani "ENERGY DRINKS" inavyoweza kuongeza uwiano wa kusinyaa na kutanuka kwa moyo (mapigo ya moyo)baada ya lisaa limoja la matumizi la vinywaji vya aina hiyo.

LAKINI NI ATHARI GANI HASA TUNAZIPATA KUTOKANA NA MATUMIZI YA V"ENERGY DRINKS"?

Mara tu baada ya kunywa ,ndani ya dakika kumi za mwanzo CAFFEINE huingia kwenye mirija ya damu hivyo kupelekeakuongezeka kwa mapigo ya moyo na presha ya damu.

Dakika 15 mpaka 45 baadae,kiasi cha CAFFEINE kilichoingia kwenye mirija ya damu kinakuwa kimeshaenea mwilini kote tayari, matokeo ya hili ni kuwa mtumiaji hujihisi yuko fresh sana ma umakini wa akili huongezeka, kiufupi anakuwa na kujihisi mchangamfu.

'CAFFEINE huzuia (kwa muda) njia za kemikali aina ya ADENOSINE (kemikali ambayo huhusika na maswala ya wewe kujiskia umechoka na uchovu) kufika kwenye ubongo na kuruhusu uzalishaji kirahisi wa kemikali ya DOPAMINE
(hii kemikali hutoa signal au taarifa za kujiskia vizuri kenda kwenye ubongo), hivyo kupelekea ubongo kupokea taarifa za kujiskia mchangamfu pekee, ubongo hufanya kazi yake ikiwemo kuzitafsiri zile taarifa na matokeo yake ni mtumiaji kujiskia mchangamfu na kuongezeka umakini wa akili.

Ndani ya saa moja baada ya kunywa "ENERGY DRINK",athari za CAFFEINE huanza kutokea na mmeng'enyo wa sukari hutokea (ambapo matokeo yake ni kujiskia mchovu),ile hali ya kujiskia mchangamfu taratibu huanza kupungua na hali ya kujiskia kuchoka huzidi.

Huchukua masaa matano mpaka sita (5-6) kwa mwili kupunguza kiasi cha CAFFEINE kilichokuwepo kwenye mishipa ya damu kwa 50%,na huchukua wastani wa masaa kumi na mbili (12) kwa mwili kupunguza kiwangho chote cha CAFFEINE kutoka kwenye mishipa ya damu.

NOTE: Muda unaotumika kwa mwili kupunguza kiwango cha CAFFEINE hutegemea na kiwango cha CAFFEINE kilichopo ndani ya mwili na pia hutegemea aina ya mtumiaji aidha kijana au mtu mzima na aidha ni mtumiaji wa mara kwa mara au mtumiaji wa mara moja moja.

Akina mama wajawazito,watu wenye matatizo ya ini na utumiaji wa baadhi ya madawa hupunguza kasi ya kuondoa kiasi cha CAFFEINE mwilini. Hata hivyo watoto na vijana kwao CAFFEINE huweza kukaa kwa muda mrefu mwilini na kwa kiwango kikubwa kuliko watu wazima. Hivi ndio maana "ENERGY DRINKS" huweza sababisha matatizo kadhaa kwa watoto ikiwemo hali kujiskia wasiwasi (anxiety).

Pia inaelezwa kuwa watumiaji wa CAFFEINE (kinywaji chochote cha chenye kujumuisha caffeine ikiwemo kahawa na energy drinks) wa mara kwa mara,kwao kuondoka kwa CAFFEINE mwilini huchukua kati ya masaa 12-24 baada ya matumizi,moja ya dalili za kuondoka kwa kiwango cha CAFEEINE mwilini ni kuhisi maumivu ya kichwa.

JE, KUNA ATHARI ZOZOTE ZA KUTUMIA "ENERGY DRINKS"?
"ENERGY DRINKS" huweza kuwa na athari hasi endapo havitatumiwa kama inavyoelekezwa, Katika kuangalia athari za matumizi ya "ENERGY DRINKS",tuangalie athari ya kiungo kimoja kimoja (vinavyotumika kutengeneza "ENERGY DRINKS" kama vitazidishwa matumizi).

CAFFEINE


Hiki ni kiungo muhimu sana katika utengenezaji wa "ENERGY DRINKS" na ni moja ya vitu vinavyotumiwa zaidi duniani.

Kiwango mahususi cha matumizi zaidi ya CAFFEINE (OVERDOSE) hutofautiana na mtu mmoja mmoja, kwa watu wengi utumiaji wa CAFFEINE zaidi ya miligram 400 kwa siku huweza kusababisha baadhi ya dalili za athari za CAFFEINE,mfano kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kukosa usingizi (mara nyingi watumiaji hutumia CAFFEINE kwa lengo la kutolala).

MATUMIZI ZAIDI(OVERDOSE) HUPELEKEA:
>Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
>Wasi wasi au kupaniki (panic)
>Kizunguzungu
Kwa wenye aleji (allergy) na CAFFEINE kwao hupelekea:
>Kupumua kwa tabu,kukaza kwa kifua,kutetemeka,kutapika.

KUMBUKA:
CAFFEINE hupatikana kwenye vinywaji vingi ikiwemo GREEN TEA na KAHAWA,hivyo ni muhimu kusoma LABEL kwenye chupa ya kinywaji kabla ya kukitumia kujua kama kinywaji hiko kinajumuisha CAFFEINE au la.

SUKARI (SUGAR)


"ENERGY DRINKS" hujumuisha sukari pia,lakini mfumo wa "FRUCTOSE CORN SYRUP" ambapo seli za mwili hubadilisha sukari hii kwenda kwenye mfumo wa GLUCOSE na kutumiwa kama nishati mwilini.

MATUMIZI ZAIDI (OVERDOSE) HUEPELEKEA:
>Kuongezeka uzito (obesity)
>Kuoza kwa meno
>Kiasi cha sukari kikizidi mwilini hupelekea kufeli kwa INSULIN(ambayo huhusika na kubalansi kiwango cha sukari mwilini.Moja ya matokeo ya kufeli kwa INSULIN ni mtu kupata kisukari,tunajua athari za kisukari!.

TAURINE


Kitaalamu bado hazijajulikana athari hasi za TAURINE,laikini huko siku za nyuma vinywaji vilvyokuwa vikijumuisha TAURINE vilipigwa marufuku katika nchi za UFARANSA,NORWAY na DENMARK,baada ya kugundulika kuwa TAURINE haina madhara kiafya vinywaji vilivyojumuisha kiungo cha TAURINE viliruhusiwa katika nchi hizo.

VITAMIN B


>Matumizi zaidi ya miligram 35 ya VITAMIN B yanatosha kabisha kukusababishia SKIN FLUSHING (kubadilika kwa rangi ya ngozi kama weupe huwa nyekundu,kwa sehemu tu ya mwili)

>Matumizi zaidi ya miliogram 300 huweza sababisha sumu ndani ya INI (ini ndo huchuja kiwango cha sumu mwilini,kufeli kwa ini maana yake mwili hautakuwa na uwezo wa kuchuja sumu iingiayo mwilini).

Chapisho moja la maswala ya dawa la UINGEREZA (The british journal of medicine)lilichapisha taarifa kuhusu mtu mmoja aliekuwa akitumia "ENERGY DRINK"(jina la kampuni halikuweza tajwa) chupa 5 kwa siku kwa muda wa kipindi cha wiki zipatazo tatu (3), aliyepatwa na kujengeka kwa sumu mwilini.

>Matumizi zaidi ya milgram 100 (100mg) ya VITAMIN B6 huweza kusababisha matatizo ya neva za hisia hivyo kupunguza uwezo wa kuhisi vitu.
HAPO JUU NI BAADHI YA VIUNGO VYA ENERGY DRINK NA MADHARA YAKE.

KIPI SALAMA KWETU?
Kwa kujaribu kuepuka madhara ya matumizi ya "ENERGY DRINKS" tunashauri yafuatayo yafanyike na watumiaji wa CAFFEINE

<> Watu wenye aleji (allergy) na CAFFEINE wasitumie "ENERGY DRINKS" kwa kuwa vinywaji hivyo hujumuisha CAFEEINE kwa kiwango kikubwa.
<> Wanawake wajawazito,wakina mama wanaonyonyesha,wenye matatizo ya moyo na presha wasitumie vinywaji vyovyote vinavyojumuisha CAFFEINE.
<> Ni vyema kusoma LABEL ya chupa ya kinywaji kabla ya kukitumia.

#PROUDLY_SPONSORED_BY
JSRindustries
CLYZ MOOD FB PAGE
CO-SPONSORED BY
KENDRICK STUDIO
HAMIS KIMWAGA (BINGWA)

[/QUOTE
 
Amka hapo ulipo anza kufanya jogging hata kwa nusu saa mapigo ya moyo yatarudi normal
Badala ya kumwambia akamuone daktari we unajifanya daktari? akifa tukutafute?

Msiwe mnajifanya kutoa ushauri wa afya online kwa mambo msiyoyajua. Matatizo ya moyo yanaongoza kuua watu nchi nyingi sana watu hua hawajui tu, Matatizo ya moyo yameua mara tatu zaidi ya HIV, malaria na TB combined. Sio kitu cha kuchukulia lightly hata kidogo.
 
Fanya mazoezi ya kuruka kichurachura simama chuchumaa ruka ruka and staff like that la sivyo tutakukosa mkuu. Hizo energy drinks ni hatari sana. Kifo nje nje. Hali ikiwa mbaya wahi hospitali na ukae mbali na hizo energy drinks.
 
Graph,

Kwahiyo unataka mpaka suala la kumuona daktari wanajf tumkumbushe nalo, na vipi kama mimi ni daktari naongea kwa uzoefu wangu utajuaje? Au unadhani akienda hospitali akisema amekunywa Mo Energy mapigo yanaenda mbio kuna dawa atapewa? Kwahiyo ulitaka comments zote humu tumwambie nenda hospitali na mtu kauliza ili apate ufumbuzi kama umeona nimekosea kumpa ushauri niliompa haya basi hujachelewa mwambie wewe aende akamuone daktari sasa.

Halafu unajua kwanini nimemshauri jambo hilo baada ya kusema moyo wake unakwenda mbio baada ya kunywa Mo Energy? Unajua kazi ya Mo Energy na yeye unajua amekosea wapi? Laiti ungejua kazi ya hizi energy drinks usingedoubt ushauri niliompa.
 
Hiyo Extra sio energy drink. Ni just berry flavoured drink with low caffeine content ambayo haina madhara labda kama uko very sensitive na caffeine.

Jaribu kucheki blood sugar yako kuna uwezekano haiko sawa. Hiyo Extra kama zilivyo carbonated soft drinks zinakuwa na sukari nyingi ambayo inaweza kuwa kisababishi cha mabadiliko unayoyasikia.
 
TADPOLE, Sio lazima umkumbushe ila usimpe ushauri usiojua. Na nina uhakika 100% wewe sio daktari, huwezi fanya diagnosis kwa information aliyokupa alafu ukamwambia akakimbie, hivi hujui kukimbia inapandisha mapigo ya moyo? Mtu mwenye tatizo la moyo aende akapandishe mapigo ya moyo?
 
Mapigo ya moyo kwenda mbio kuna sababu nyingi na dawa sio kukimbia, labda tuseme kujishughulisha na matembezi ya hatua kidogo yawepo na huu ugonjwa huwapata binadamu kuanzia miaka 35 na hasa wanaume, mojawapo ni haya lakini Daktari ni muhimu akupime huenda una mengine maana wengine hizo energy tunatumia tuendeshapo gari na zisizidi 2.

Common causes of high blood pressure spikes
  • Caffeine. Mo energy
  • Certain medications (such as nonsteroidal anti-inflammatory drugs) or combinations of medications.
  • Chronic kidney disease.
  • Cocaine use.
  • Collagen vascular disorders.
  • Overactive adrenal glands.
  • Pregnancy-related high blood pressure.
  • Scleroderma.
Here are 17 effective ways to lower your blood pressure levels:
  1. Increase activity and exercise more
  2. Lose weight if you're overweight
  3. Cut back on sugar and refined carbohydrates
  4. Eat more potassium and less sodium
  5. Eat less processed food
  6. Stop smoking
  7. Reduce excess stress.
  8. Try meditation or yoga.
 
Back
Top Bottom