Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,806
- 59,286
- Thread starter
- #101
Hi thread nimeipenda sana,
Kweli name imenikumbusha mbali sana….nakumbuka tukiwa shule ya msingi kabla ya kuingia darasani lazima tukimbie mchakamchaka…nakumbuka somo la sayansi kimu….mihogo ya kukaanga ilikuwa juu sana wakati wa mapumziko na bakora ukichelewa namba…
Nakumbuka tukiwa wadogo bado siku za sikukuu ilikuwa ndio swaga kwenda kutembea mjini maeneo ya feli na pale chini pembeni ya bahari siku hizi kumewekwa fensi….
Nakumbuka enzi tukiwa tunakwenda sinema kwenye theatres kama vile "Avalon,Empire,Empress,Odeon,New Chox na kule msasani Drive Inn" na sinema za kihindi kina Mithun na wengine…
Nakumbuka tulikuwa tunakwenda kuruka ukuta ili kuona mpira uwanja wa Taifa (ule wa zamani)…
Nakumbuka Corn Ice Cream za Bakhressa zilivyokuwa juu enzi hizo….
Mchakamchaka ....Chinjaaaa
Mchaka mchaka ...Chinjaaaaa
Nimesahau mwendelezo...alafu kulikua na mwingine unasema tungeweza tungemrudisha SOKOINE duniani!!!
Ehhh bila kusahau ngonjera na mashairi,.....