Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,820
- 59,406
Nimejikuta nakumbuka enzi zangu za utoto..utundu...ukorofi na uchokozi kwa sana nikaona nishee na kakaz pamoja na dadaz zangu wa JeiEff....bila kukosa zenu!!!
Nakumbuka darasa la tano rafiki yangu L alianza kuandikiana barua za kimapenzi na mvulana mpya shuleni...tena alikua mkubwa kuliko sisi.Tulikua tuna kundi letu sasa ghafla mwenzetu akapunguza kusoma na sisi...kucheza na sisi....kila saa anajifanya kuna kitu anatakiwa kufanya!Siku moja tukiwa darasani tunamsubiria mwl. wa eng. aje mwenzetu akawa kainama kwenye daftari yuko bize kweli....si tulikua dawati la mbele na yeye la pili kwahiyo tukageuka kumuuliza anasoma nini akakataa kutwambia!Tukapanga wawili wabaki pale kumsumbua alafu mimi nimzunguke ili nimnyang'anye lile daftari!Ikawa vuta nikuvute nikatoka na kipande cha karatasi na yeye akabaki na kipande....tukakimbia nje kuongalia tunaona mambo ya nakupenda...sijui nini na nini tukabaki tunacheka!Bahati mbaya mwl akatukuta pale nje akaitaka ile karatasi kwahiyo besti yetu akawa in trouble.Akamaind seme baadae akaja kutuambia asante!!!
Nakumbuka tulikua tunapikiwa uji wa sukari na chumvi ...tunaweka malimao au kupindi cha maembe tunachukua mabichi tunayakataka alafu tunaweka kwenye uji!Makande na ugali wa maharage vilikua vinasindikizwa na maparachichi!!Siku za sherehe wali wa maharage...pilau au ndizi nyama!!
Nakumbuka niliwahi kulipiza kisasi kwa kumsingizia mshkaji mmoja hivi kanipiga baada ya kunichokozoga mpaka nikaogopa kwenda shule kwa siku kadhaa...nikajificha chaka..lolzz....then nilivyorudi mi ndo niliadhibiwa yeye hata hakuguswa!!Basi alicharazwa na adhabu ya kuotesha na kunyeshea maua akapewa!!!
Nakumbuka kuna kipindi iliazuka kwamba baadhi ya wanafunzi wana majini....sijui kama ilikua kweli au walikua wanajifanya tu ila walikua wanazimia....wanaongea mambo ya ajabu ajabu..bila kusahau wakawa wakorofi kweli maana wakiona fimbo tu wanazimia kwahiyo wakawa hawachapwi.
Nakumbuka wavulana walikua wanatuchungulia na vioo tukiwa mstarini....waliotangulia kukua wakawa wanashikwa maziwa...wengine wanachekelea wengine wanamaind.
Nakumbuka tulikua tunashika namba saa 1...usafi mpaka saa 2....break saa 4..lunch saa 6 mpaka 7....alafu class tena mpaka saa 9 alafu tunamalizia kwa usafi.
Nakumbuka tulikua tunatumwa kuni....watu wanakuja na vifagio vyao.
Nakumbuka kuna mtoto mmoja mkorofi kweli alikua anaitwa Gody alirushaga baruti wakati wa mapumziko chuma ikamdondokea mwenzake kichwani akapasuka kidogo.Akakimbia hakuwahi kuja tena shule..mama yake alikua mwalimu wa shule nyingine kwahiyo akampeleka mtoto wake huko.Huko nako akaendelea na uchokozi kama kawa....siku moja wakiwa wanatoka shule akawa anamtoboa toboa msichana mmoja na penseli...yule msichana akampokonya ile penseli akajikuta amemtoboa jicho!Gody akawa chongo kwa uchokozi wake.
Nakumbuka kipindi cha majini mvulana mmoja alichaniwaga kaptula yake na mmoja wa wasichana akiwa amepandisha yake.Hahahaha....mshkaji alibaki wazi nyuma ikabidi aazimwe sweta ajifunike alafu akaruhusiwa kwenda nyumbani.
Nakumbuka nilikua tukitoka shule naingia tuition mpaka saa 12 ndo niende nyumbani.
Nakumbuka siku moja nilipitia kwa rafiki yangu kuangalia tv ....nilivyorudi nyumbani nikasema nilikua nimetumwa na mwl.Ile nimeingia ndani kubadilisha nguo rafiki yangu huyo kaniletea begi langu nlikua nimesahau kwao.....akaulizwa na wewe ulikua umetumwa akajibu hapana,...sasa begi la Lizzy umelipata wapi...akajibu tulikua kwetu tunaangalia tv akasahau.
Nakumbuka kuna rafiki yangu baba yake alijinyonga!Nampitia asubuhi tuongozane nakuta kwao kumejaa watu.....kumbe baba wa watu kajinyonga...tena kisa mapenzi!!
Nakumbuka nilimvunja kaka yangu jino mpaka sasa hivi yuko kama ana mwanya!!!LOLZZZ!
Nakumbuka siku ya mtihani wa darasa la nne mvua ilinyesha radi ikachana mti uliokuwepo nyuma ya darasa letu kwanzia juu mpaka chini!!Bila kusahau picha zetu za kushikilia makompasi.....swagga za enzi hizo.
Ahhhh so many memories..nyingine ngoja niwawekee wajukuu zangu!!!!