Nimekumbuka zamani!!

Hii thread imenifanya nikumbuke mengi sana enzi za utoto!!
Nakumbuka nilikamatwa na Barua nimemwandikia Monitress nilipokuwa darasa la kwanza.
Nakumbuka nilikuwa nacheza michezo yote ya kike ingawa mimi wa kiume.
Nakumbuka enzi za KOMBOLELA lazima nikajifiche sehemu 1 na mrembo inapita michezo 3 hamjaonekana!!
Nakumbuka.............................!!!!!!!!
huyu ndo smasha clearing injinia!.................Anakumbuka kuwa faraha na wasichana tu!!
 
Kuna mwalimu wetu wakiume alikuaga mkali huyo, akitaka kukuchapa anakuuliza, unataka sita kali au nne moto, eti mtu anachagua sita kali hahaaa.

Hahahaha!Umenifanya nicheke kama mwehu!Eti sita kali au nne moto!
 
Hehehe ngoja nipotezee kabla watu hawajaanza kuchunguza!Alafu kuna kitu ntakupm!

duuhh
ilikuwa niende kulala
lakini sasa usingizi umeisha macho yametoka
ka samaki
nasubiria kwa hamu sana hiyo PM hahahahah lol
 
Hahahaha!Umenifanya nicheke kama mwehu!Eti sita kali au nne moto!
hi Lizzy! hivi natamani nikuonage manake sijui ulikuwa unawaza wapi mpaka ukaja na hii sredi? i real like it, it seems maisha yako yametawaliwa na furaha dats why you make us happy. nikisoma page za memba nabaki hoi.
Nakumbuka mkaka shuleni alipoanza kuvuta sigara mwalimu akamfuma akaiingiza yote mdomoni akajikausha kama hamna kitu mdomoni, akawa anakohoakohoa mpaka ticha akaondoka.

Nakumbuka vikalmati vya mama salama. Na watoto waliokuwa wananunua ice cream wanapokwa ile icecream yote ya juu na watoto wajanja wanabaki na biscuit tu
 
duuhh
ilikuwa niende kulala
lakini sasa usingizi umeisha macho yametoka
ka samaki
nasubiria kwa hamu sana hiyo PM hahahahah lol

Hope hujaogopa kama kibaka aliyekamatwa na wananchi wenye hasira!
 
Nakumbuka vikalmati vya mama salama. Na watoto waliokuwa wananunua ice cream wanapokwa ile icecream yote ya juu na watoto wajanja wanabaki na biscuit tu

Dah...kwenye kula kula sidhani kama kuna mtu alikua nyuma!Nikikumbuka..unakuta mtu anakung'atia embe unafuta mate alafu unabugia!
 
Nakumbuka nilipokuwa O-level tulikuwa na mchezo wa kutoa majina ya utani kwa walimu,kuna mwalimu mmoja alikuwa na nyusi nyingi karibu zinaungana tukawa tunamwitw MANYUSI na mwingine aliingia class siku ya kwanza amevaa suruali ina mifuko miwili nyuma tukaanza kumwita DABO POKETI,mwingine alikuwa na Garden Luv la kitosha linachomoza hadi shingoni tukawa tunamwita MWAKIPESILE kwa kuwa tu kuna gazeti fulani lilikuwa linatoa katuni ya jamaa mwenye jina hilo aliyekuwa na garden kama ufagio.

Primary napo nakumbuka niliwahi kucheza kamari nikaliwa hadi nauli ya daladala ikatokea lifti nikaikimbilia na kusahau begi la shule,kesho yake nikakuta madaftari tu tena yamechanwa begi likaenda, begi lenyewe lilikuwa ni la mgongoni limeangikwa OASIS.
 
Hahahahaah.....sasa hao madaftari yaliwashinda ama???Utoto bwana...nautamani kweli!!!
 
Uchangiaji niliouona katika thread hii unanifanya niunge mkono wimbo wa Lady Jaydee wa "Natamani kuwa kama Malaika".

Wengi maisha ya utotoni yana kumbukumbu nzuri sana.
 
Kijijini hapo Shitimbi!

attachment.php
 
Attachments

  • Kijijini.jpg
    Kijijini.jpg
    48.2 KB · Views: 103

Hi thread nimeipenda sana,
Kweli name imenikumbusha mbali sana….nakumbuka tukiwa shule ya msingi kabla ya kuingia darasani lazima tukimbie mchakamchaka…nakumbuka somo la sayansi kimu….mihogo ya kukaanga ilikuwa juu sana wakati wa mapumziko na bakora ukichelewa namba…
Nakumbuka tukiwa wadogo bado siku za sikukuu ilikuwa ndio swaga kwenda kutembea mjini maeneo ya feli na pale chini pembeni ya bahari siku hizi kumewekwa fensi….
Nakumbuka enzi tukiwa tunakwenda sinema kwenye theatres kama vile “Avalon,Empire,Empress,Odeon,New Chox na kule msasani Drive Inn” na sinema za kihindi kina Mithun na wengine…
Nakumbuka tulikuwa tunakwenda kuruka ukuta ili kuona mpira uwanja wa Taifa (ule wa zamani)…
Nakumbuka Corn Ice Cream za Bakhressa zilivyokuwa juu enzi hizo….
 
Back
Top Bottom