mahmood,mara nyingi ukizungumzia kitu cha mwenzako kana kwamba wewe unakijua zaidi kuliko mhusika unajizuia wewe mwenyewe kupata maarifa!anyway ngoja nijaribu kukuweka sawa
kwa ufupi ni kwamba-ukristo umesimama ktk agano jipya!na agano jipya linazungumzia mambo ya zamani ktk misingi inayopaswa kuwa baada ya kristo kuja!na huo ndio ukristo!
ndio maana sisi RC ktk misa au ibada yetu kuna somo la kwanza na somo la pili,yote yanaendana lakini mwisho wa siku tunasimama ktk somo la pili ambalo hutoka agano jipya!na huo ndio ukristo
Rafiki Mc Tilly Chizenga,
Soma hapo chini kisha tufafanulie.
Yesu Mwenyewe anasema katika mathayo 5:17-19.
17``Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike.
19 Kwa hiyo ye yote atakayelegeza hata mojawapo ya amri ndogo kuliko amri zote na akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni. Sikuja kuzifuta bali kuzitimiza.
18 Kwa maana ninawaambia hakika Lakini atakayetii amri hizi na kuwafundisha wengine kuzitii ataitwa mkuu katika Ufalme wa mbinguni.
Luka 24:44
44 Akawaambia, ``Haya ndiyo mambo niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi; kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika sheria ya Musa, katika Maandiko ya manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.
na Yesu alishasema kiingiacho si najisi bali kitokacho!labda nikuulize-kipi ni bora kwako-huwa unakunywa soda,lakini ukirudi nyumbani unapiga mkeo na watoto na kila aina ya fujo,au unakunywa pombe lakini ukirudi nyumbani umtulivu na kila aina ya upendo kwa wanao na mkeo?unadhani mkeo na watoto wakikuona ktk hali hizo mbili wakaulizwa baba anywe kinywaji gani watachagua soda?
Hakuifahamu aya hiyo, maana ya aya hiyo ni hii
kula chakula bila kunawa mikono hakumtii mtu najisi. (si kula nguruwe ni halali, kula nguruwe ni haramu kabisa, Biblia inasema hivyo kwa lugha safi kabisa Mambo ya Walawi 11:07-08)
Soma aya hizo za Biblia vizuri (Matayo 15:1-20)
1 Kisha Mafarisayo na walimu wa Sheria wakafika kutoka Yerusalemu, wakamwendea Yesu, wakamwuliza,
2 Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kutoka kwa wazee wetu? Hawanawi mikono yao kama ipasavyo kabla ya kula!
3 Yesu akawajibu, "Kwa nini nanyi mnapendelea mapokeo yenu wenyewe na hamuijali Sheria ya Mungu?
4 Mungu amesema: Waheshimu baba yako na mama yako, na Anayemkashifu baba yake au mama yake, lazima auawe.
5 Lakini ninyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema: Kitu hiki nimemtolea Mungu,
6 basi, hapaswi tena kumheshimu baba yake! Ndivyo mnavyodharau neno la Mungu kwa kufuata mafundisho yenu wenyewe.
7 Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu:
8 Watu hawa, asema Mungu, huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
9 Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu."
10 Yesu aliuita ule umati wa watu, akawaambia, "Sikilizeni na muelewe!
11 Kitu kinachomtia mtu najisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu najisi."
12 Kisha wanafunzi wakamwendea, wakamwambia, "Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa waliposikia maneno yako?"
13 Lakini yeye akawajibu, "Kila mmea ambao Baba yangu aliye mbinguni hakuupanda, utang'olewa.
14 Waacheni wenyewe! Wao ni vipofu, viongozi wa vipofu; na kipofu akimwongoza kipofu, wote wawili hutumbukia shimoni."
15 Petro akadakia, "Tufafanulie huo mfano."
16 Yesu akasema, "Hata nyinyi hamwelewi?
17 Je, hamwelewi kwamba kila kinachoingia kinywani huenda tumboni na baadaye hutupwa nje chooni?
18 Lakini yale yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi.
19 Maana moyoni hutoka mawazo maovu yanayosababisha uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na kashfa.
20 Hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi.
Lakini kula chakula bila kunawa mikono hakumtii mtu najisi." (Matayo 15:1-20)
kula nguruwe ni haramu , Biblia inasema hivyo kwa lugha safi kabisa,
Biblia inasema (katika Mambo ya Walawi 11:07-08)
Naye nguruwe ingawa anazo kwato zilizogawanyika sehemu mbili, lakini hacheui, ni najisi kwenu. Kamwe msile nyama yao wala kugusa mizoga yao, wao ni najisi kwenu.