Mimi kuna siku moja nilikuwa nimepanda DCM za kutoka Mwanza Kwenda Igombe
Kuna mdada fulani hivi alikuwa na jamaa fulani hivi walikuwa wamekaa siti ya nyuma/mwisho kabisa.
Sasa yule mdada akawa anamusimulia kuhusu ubora na uzuri wa mtandao Jamiiforums.
Yule mdada alikuwa mweupe mrefu fulani hivi na alikuwa amevaa gauni refu.
Yule mdada alienda zaidi kumusimulia yule jamaa mambo ya Pm na kumushawishi ajiunge Jamiiforums.
Kisura yule mdada ni mzuri sababu nilimuona ila sikubahatika kupata/kuiona/kumuuliza kuwa anatumia ID ipi huku Jamiiforums.
Kama upo humu wewe mdada uliyepanda siku ile DCM za Mwanza To Igombe Jua kuwa nilikuona sana tu na ulivyoshuka alipitia ile njia ya kwenda ziwani na huyo jamaa.
Mimi nilikuwa naenda Kayenze kule kwa mwarabu wetu MAJID WA DIGIDIGI BUS
Mkuu Evalyn Salt anamjua sana tu huyo mwarabu