Wakuu habari za mwaka 2020 sina budi kumshukuru MUNGU kwa kuuona tena mwaka mwingine na nawatakia maisha mema na maendeleo.
Niingie moja kwa moja kunako maada yangu wapendwa
Kwa sasa nina miaka 24 sijaoa bado toka 2018 mwezi wa 09 nimetoka nyumbani maeneo ya Sengerema nimekuja mwanza
Nilipo fika nilifikia kwa ndugu yangu ambaye ni kama mdogo wangu maana namzidi umri kati ya miaka 2
Nimekaa pale kama miezi 3 baada ya hapo nilienda kwa mjomba wangu ambaye nae yupo huku Mwanza nimeishi kuanzia mwezi wa 11-2018
Mpaka sasa hii 2020 nipo kwake
Napiga harakati ndogo ndogo kujipatia hela ya matumizi na kuna wakati napiga nae ishu za kazi
CHANGAMOTO YANGU KUBWA
Natamani na mimi nijitegemee maana yake nipange geto langu nianzishe maisha yangu kama kijana hadi nahisi aibu muda wote kuishi bila wazo lolote ambalo litasababisha changamoto ya kujikwamua katka maisha
Nakama mnavyojua changamoto ya kuishi kwa mtu yapasa uvumilivu, na kingine ambacho naogopa ni kuhusu hofu ya kwamba maisha ya geto ntayaweza nikiwa mwenyewe?,
Labda siku nikikosa ramani ya pesa itakiwaje ?
Lakini wazo la kutoka hapa kwa mjomba bado sijamshirikisha nimepanga nikipata pesa ya kununua godoro na pesa ya pango la miezi mitatu ya kianzio ndo namtaarifu kuhusu hili.
Nimepanga mwezi wa tano niwe nishatoka hap kwa uncle na sitaki kurudi sahizi kijijini nataka nipambane kama kijana kabla sijaoa.
NATAMANI SANA USHAURI WENU WAKUU JE NIPO SAHIHI KWA MAAMUZI NINAYO TAKA KUCHUKUA MWAKA HUU 2020?
Sent using
Jamii Forums mobile app