Nimekua, natamani kujitegemea

Nimekua, natamani kujitegemea

Kaza ujitegemee...mimi nilianza kujitegemea nikiwa na miaka 20
Wakuu habari za mwaka 2020 sina budi kumshukuru Mungu kwa kuuona tena mwaka mwingine na nawatakia maisha mema na maendeleo.

Niingie moja kwa moja kunako maada yangu wapendwa

Kwa sasa nina miaka 24 sijaoa bado toka 2018 mwezi wa 09 nimetoka nyumbani maeneo ya Sengerema nimekuja Mwanza.

Nilipofika nilifikia kwa ndugu yangu ambaye ni kama mdogo wangu maana namzidi umri kati ya miaka 2.

Nimekaa pale kama miezi 3 baada ya hapo nilienda kwa mjomba wangu ambaye nae yupo huku Mwanza. Nimeishi kuanzia mwezi wa 11-2018 na mpaka sasa hii 2020 nipo kwake.

Napiga harakati ndogo ndogo kujipatia hela ya matumizi na kuna wakati napiga naye ishu za kazi.

CHANGAMOTO YANGU KUBWA

Natamani na mimi nijitegemee; maana yake nipange geto langu nianzishe maisha yangu kama kijana. Hadi nahisi aibu muda wote kuishi bila wazo lolote ambalo litasababisha changamoto ya kujikwamua katika maisha.

Na kama mnavyojua changamoto ya kuishi kwa mtu yapasa uvumilivu, na kingine ambacho naogopa ni kuhusu hofu ya kwamba maisha ya geto ntayaweza nikiwa mwenyewe? Labda siku nikikosa ramani ya pesa itakiwaje?

Lakini wazo la kutoka hapa kwa mjomba bado sijamshirikisha nimepanga nikipata pesa ya kununua godoro na pesa ya pango la miezi mitatu ya kianzio ndiyo namtaarifu kuhusu hili.

Nimepanga mwezi wa tano niwe nishatoka hap kwa uncle na sitaki kurudi sahizi kijijini nataka nipambane kama kijana kabla sijaoa.

NATAMANI SANA USHAURI WENU WAKUU. JE, NIPO SAHIHI KWA MAAMUZI NINAYO TAKA KUCHUKUA MWAKA HUU 2020?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Big up bro,tusiogope changamoto za kuishi wenyewe bila ya wazazi kuwa karibu na nilichogundua kuishi hom huwezi panuka akili

Sent using Jamii Forums mobile app
ComfortZone.jpg
 
kuwa last born shida sana Nalazimishwa kurudi nyuumbani Dead line mwisho wa mwezi huu wote waeondoka mimi natakiwa nkakae na Mom Napiga hesabu za kutokwenda 😡😡
 
Box La kulalia 3000 au unaweza pita madukani usiku kuokota
Bakuli Moja 500
Sahani Moja 500
Kikombe kimoja 500
Jiko 3000 hadi 5000
Sufuria mbili 8500
Kijiko 150
Mwiko 500
kisu 1000
Mkaa 1000
Unga Nusu Debe bei ina. vary
Dagaa 1000
Mafuta 1000
Chumvi 400
Kodi 30000 inavary
Ndoo 2 ndogo na kubwa 8000
Si lazima ununue vyote kwa mkupuo
Wengine wataongeza au Kupunguza
 
Back
Top Bottom