Nimekosea wapi

Nimekosea wapi

Kwenye ile orodha ya wanaume wako wa zamani uliomtajia, Jay Mo kwa nini hukumtaja?
 
Niliwahi kuandika uzi wangu wa kutafuta mwenza humu ndani, katika wengi waliokuja nikabahatika kupata kijana mmoja aliyeukuna moyo wangu,nikaona nijaribu mahusiano naye sikutaka kujiachia mazima tangu nimemkubali ni wiki tatu zimepita na bado hajaweka fedha zake kwenye pochi yangu (sex) amekuwa akinionesha upendo wa hali ya juu, hana elimu kabisa ila ni mfanyabiashara aliyefanikiwa, imekuwa ni kawaida kunifuata kazini kila ambapo nikimwambia aje na kunipeleka nyumbani,neno langu limekuwa sheria kwake, sasa tatizo ni hili wiki iliyopita akaniomba anifundishe kuendesha gari ili nikiweza anipe moja nitumie kati ya machache anayomiliki. Mwanafunzi Mimi nimekuwa muoga kuingia barabarani kibaya zaidi niliparamia ukuta na gari ikabonyea akanifokea sana kiukweli iliniuma kufokewa naye kwani mpaka alinitolea tusi, ndani ya gari ukapigwa wimbo wa sisi tunakula bata wa Jay mo, nikamuomba autoe akataka kujua kwanini nikamwambia simpendi Jay mo tumegombana, akataka kujua sababu sikumwambia basi hapo ndipo tatizo likaanza amenuna hataki kuongea na mimi Sasa Wakuu sielewi nimekosea wapi kwenye kugonga gari au kukataa kumwambia ugomvi wangu na Jay moo ni nini!!! Nakosa raha yaani mahusiano yangu mapya yavunjike ndani ya wiki tatu sina rahaa kabisa


Sent using Jamii Forums mobile app
Yakivunjika kwa ajili ya sababu kama hizo, trust me; even u, don't want that kind of relationship! Kwanza kakosea kukufundisha gari badala akupeleke driving school kwene magari ambayo huenzi gonga ukuta hovyo. Ukizoea ndo aje akupe hayo yake. Yeye mwenyewe hakuanza kirahisi. Na huo wimbo alipaswa kukuvumilia, sababu angekuja kuijua tu. Literally, speaking ni utoto tu ndo unaendelea hapo
 
Hapo hajarasimisha tayari unafokewa na kutukanwa😳😳 Read between the lines.
 
Kwa mbalii nakuona unaandaliwa kuwa single mother.Kugongeza gari anakuzingua unadhani ataweza kukukabidhi ulitumie ?? Shirikisha akili achana na miteremko.
 
Hii tabia ya wapenzi kufundishana kuendesha magari sio kabisa, kwa nini asikupeleke driving school ukajifunze huko?
 
Yakivunjika kwa ajili ya sababu kama hizo, trust me; even u, don't want that kind of relationship! Kwanza kakosea kukufundisha gari badala akupeleke driving school kwene magari ambayo huenzi gonga ukuta hovyo. Ukizoea ndo aje akupe hayo yake. Yeye mwenyewe hakuanza kirahisi. Na huo wimbo alipaswa kukuvumilia, sababu angekuja kuijua tu. Literally, speaking ni utoto tu ndo unaendelea hapo

Nimekuelewa sana kiukweli


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Jamaa yako atakuwa na shida kwani ni lazima kupenda nyimbo za kila wasanii?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom