Bob Lee Swagger
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 1,362
- 515
Nina mdogo wangu anayesoma katika jiji la Mwanza,shule moja ya kata, iitwayo Mtoni sekondari; amenieleza kitu kilichonisikitisha sana, kwa sasa wao kule wako katika mitihani ya mock..
Kilichotokea ni hiki..
Wakiwa wameanza tayari mitihani yao, walipoteza STEPLER MACHINE juzi labda j3 au j4, sielewi kama ilikuwa katika ofisi ya mwalimu ama katika chumba cha mtihani.
Siku iliyofuatia asubuhi mwalimu mkuu wa shule akawambia kuwa walete hiyo stepler machine la si hivyo hawafanyi mitihani ya mock ya siku hiyo, katika mazingira kama hayo stepler haikupatikana siku hiyo na wao hawakufanya mitihani yao ya siku,kama sijakosea amenambia hawakufanya English na Civics, shule yao ina mikondo/vyumba vinne vya mitihani so chumba chao chenye takriban wanafunzi 50 ndio hawakuweza kufanya mitihani siku hiyo.
Siku iliyofuatia ikabidi wachange na kununua stepler machine nyingine na kwenda kuikabidhi kwa mwalimu mkuu, ambaye aliikataa na kusema anaitaka ile ile ya kwake ama sivyo wachange shilingi 1000/= kila mmoja!!
Naambiwa kuna mwenzao mmoja aliyekwenda kushtaki juu ya suala hili kwa Afisa Elimu, kilichotokea ni kwamba baadaye mwalimu mkuu aliwatangazia kuwa wao wanaenda kumwambia afisa elimu ambaye ni mpwa wake so hawez kufanywa kitu!
Na alichofanya Afisa elimu ni kumwambia huyo mwalimu mkuu jina la mwanafunzi huyo na Mwalimu mkuu akaamua kumpa suspension, ambayo ni kuwa asikanyage shuleni hadi tarehe ya kufanya mitihani ya necta mwishoni mwa mwaka!!
Kweli hii ni haki?! ile dhana ya mwalimu kuwa mzazi imeishia wap?! Busara (hii ndogo tu) imekwenda wap?!
Wanafunzi wanafanya mitihani ili kujipima uwezo wao katika wakati husika na matokeo ya mitihani yao ndo changamoto kwao kujitahidi na maandalizi zaid kabla ya necta, Je katika hili la kufanya mitihani kwa hofu ya kufukuzwa chumba cha mitihani na tena kufanya mitihani nusu nusu ni nini? Tutegemee matokeo gani?
Je kuna stepler ya shilingi 50,000/=?! sio kwamba kuinunua tu ingetosha kwa sababu ilishanunuliwa ila akaikataa kwa sababu kuwa anataka ile ya kwake?! Na hata akipewa hiyo fedha naye hataweza kununua ile ya kwake vile vile! atanunua nyingine kama hiyo aliyoikataa! Sio uonevu huu na jinsi ya kutafuta fedha kwa visingizio vingine!!?
Naomba maoni na/au msaada katika hili wakuu..