Nimekosa pa kuanzia.. ila Kweli hii ni haki!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimekosa pa kuanzia.. ila Kweli hii ni haki!?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Bob Lee Swagger, May 10, 2012.

 1. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nina mdogo wangu anayesoma katika jiji la Mwanza,shule moja ya kata, iitwayo Mtoni sekondari; amenieleza kitu kilichonisikitisha sana, kwa sasa wao kule wako katika mitihani ya mock..
  Kilichotokea ni hiki..

  Wakiwa wameanza tayari mitihani yao, walipoteza STEPLER MACHINE juzi labda j3 au j4, sielewi kama ilikuwa katika ofisi ya mwalimu ama katika chumba cha mtihani.
  Siku iliyofuatia asubuhi mwalimu mkuu wa shule akawambia kuwa walete hiyo stepler machine la si hivyo hawafanyi mitihani ya mock ya siku hiyo, katika mazingira kama hayo stepler haikupatikana siku hiyo na wao hawakufanya mitihani yao ya siku,kama sijakosea amenambia hawakufanya English na Civics, shule yao ina mikondo/vyumba vinne vya mitihani so chumba chao chenye takriban wanafunzi 50 ndio hawakuweza kufanya mitihani siku hiyo.
  Siku iliyofuatia ikabidi wachange na kununua stepler machine nyingine na kwenda kuikabidhi kwa mwalimu mkuu, ambaye aliikataa na kusema anaitaka ile ile ya kwake ama sivyo wachange shilingi 1000/= kila mmoja!!
  Naambiwa kuna mwenzao mmoja aliyekwenda kushtaki juu ya suala hili kwa Afisa Elimu, kilichotokea ni kwamba baadaye mwalimu mkuu aliwatangazia kuwa wao wanaenda kumwambia afisa elimu ambaye ni mpwa wake so hawez kufanywa kitu!
  Na alichofanya Afisa elimu ni kumwambia huyo mwalimu mkuu jina la mwanafunzi huyo na Mwalimu mkuu akaamua kumpa suspension, ambayo ni kuwa asikanyage shuleni hadi tarehe ya kufanya mitihani ya necta mwishoni mwa mwaka!!

  Kweli hii ni haki?! ile dhana ya mwalimu kuwa mzazi imeishia wap?! Busara (hii ndogo tu) imekwenda wap?!

  Wanafunzi wanafanya mitihani ili kujipima uwezo wao katika wakati husika na matokeo ya mitihani yao ndo changamoto kwao kujitahidi na maandalizi zaid kabla ya necta, Je katika hili la kufanya mitihani kwa hofu ya kufukuzwa chumba cha mitihani na tena kufanya mitihani nusu nusu ni nini? Tutegemee matokeo gani?
  Je kuna stepler ya shilingi 50,000/=?! sio kwamba kuinunua tu ingetosha kwa sababu ilishanunuliwa ila akaikataa kwa sababu kuwa anataka ile ya kwake?! Na hata akipewa hiyo fedha naye hataweza kununua ile ya kwake vile vile! atanunua nyingine kama hiyo aliyoikataa! Sio uonevu huu na jinsi ya kutafuta fedha kwa visingizio vingine!!?

  Naomba maoni na/au msaada katika hili wakuu..
   
 2. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  ni PM jina la shule ili tutatue hilo tatizo.
   
 3. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Asante sana mkuu...
  Nimefanya hivyo tayari..
   
 4. n

  ngarambe Senior Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hivi humu hamna viongozi wa juu walishughulikie hilo tatizo
   
 5. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  kwan kwa afsa elimu ndo mwsho wa malalamiko? Wazaz hawapo? Kama upo dar sogea wizara ya elimu wape hlo na ufuatilie. Msaada huo sio kwa mdogo wako bali kwa taifa kaka.
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Viongozi wa juu ni akina nani? Hawa watokanao na CCM? Kuna anayejali kwani? Labda tu tuwape hili wabunge wa CHADEMA huko Mwanza wajaribu kulivalia njuga. Otherwise, kwa hawa wa CCM tangu waziri hadi mkuu wa wilaya akili zao ni kama za huyo mkuu wa shule na afisa elimu.
   
 7. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mjulishe lwakatare
   
 8. s

  sugi JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  kosa la wizi shuleni adhabu yake ni kufukuzwa shule!
   
 9. s

  sugi JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Hivi huwa mnakimbilia wapi,mnaposoma thread?si ameshaitaja shule,soma vzr mkuu
   
 10. E

  EJL Member

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  Uonevu huu kwa wanafunzi imekuwa jambo la kawaida, hasa kwa kuwa wazazi hutuwasaidii vijana wetu. Walimu wengi wamefanya wanafunzi kuwa ATM zao. Kila wakati kudai malipo yasiyokuwapo. Mwaka 2010 kuna walimu wa Buswelu secondary -iko huko huko Mwanza walikuwa wanadai sh.2000/ kwa wanafunzi wa kidato cha nne kwa ajili ya kuwasainia "clearance form". Hata kama mwanafunzi hadaiwi kitu mwalimu aitaka malip hayo.
  Niseme ufisadi katika jamii yetu upo kila mahali; na kwa wapambanaji ni vema tukaanza na huku chini tuliko maana tunaponyamazia unyama huu ndio unaoendeleza kuzalisha na kulea mafisadi. Kama mwalimu leo anadai 50,000 kwa stapler machine ya 4500/ atashindwa nini kudai kanunua mfuko wa cement kwa 100,000/ siku akipewa ukuu wa shule? Au kuziba pancha ya gari kwa 5mil pindi aipewa u-DEO?  EJL
   
 11. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Naelewa afisa elimu sio wa mwisho kwenye utatuzi wa hili.
  Wazazi wa wanafunzi pia wapo! lakini kuna kitu amenambia kuwa eti mwalimu mkuu 'huwatukana' wazazi wanapoenda kuhoji juu ya mambo kama haya. (note: nimeweka kwenye hizo alama hadi nitakapomuuliza vizuri kupata maana halisi ya kutukana ndipo ntakuja kuweka neno sahihi, kama lipo)
  Ni kweli kabisa msaada hapa sio kwa mdogo wangu pekee bali kwa taifa kwa kuwa uonevu wa aina hii haupaswi kufumbiwa macho! Mtu mmoja kufifisha matumaini na ndoto za vijana wadogo ni hatari kwa sababu inawafanya watumwa hata kama sio leo basi hapo baadae!
   
 12. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi umesoma hiyo thread vizuri mkuu?!
  Nani anatakiwa kufukuzwa shule linapotokea kosa la wizi darasani?!
  Je, ni busara wanafunzi 50 wanyimwe nafasi pekee waliyonayo ya kufanya mitihani ya majaribio ya mock kwa kosa la mtu mmoja?!
  Na nilivyoambiwa ni kwamba walijitolea kuchanga kununua hiyo stepler na wakanunua mpya kwa shilingi 8500/= lakini mwalimu akaikataa kwa kigezo kuwa anataka ile ile iliyopotea na ndo yeye akaamua kuwachangisha 1,000/= kila mmoja kwa ajili ya kuinunua! (kumbuka ni wanafunzi takriban 50 nilivyoambiwa so ni 50,000/= na obviously hawez kununua ile ile)!!
   
 13. Mjanga

  Mjanga JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 1,246
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  wadau tusikimbilie tu kusema uonevu, dhamira ya mwl Mkuu ni njema sana!
  lengo ni kukomesha vijitabia vya udokozi miongoni mwa watoto wenu!
  wazazi/walezi muwajibike!
  hiyo shule iko pale mabatini MZ kama sikosei, watoto wale ni bangi na wamejaa
  upumbavu mwingi sana!
  Mkuu huyo akaze kamba, tukianza kuwatetea wanafunzi kwa ujinga, kesho
  hao hao wanaingi ndani ya magamba tunaanza kulalamika!
   
 14. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu, naona kuna kitu hujanielewa! sijajaribu kutetea wizi hapa, Ni kweli labda stepler iliibiwa na mmoja wao lakini sidhani kama darasa zima lilishiriki ili basi kustahii adhabu hiyo kwao wote!? Na hichi ndicho ninachokitetea!
  Umesema wanafunzi pale wamejaa bangi na upuuzi mwingi, lakini cha kujiuliza ni kwamba je inawezekana kweli darasa zima likawa hivyo!?
  Ukisoma vizuri huo uzi, hapa najaribu kuelezea scenario ilivyokuwa na anayeniambia hajafukuzwa na anaendelea vizuri na mitihani isipokuwa ile miwili ambayo kama darasa, walizuiwa kufanya!? sasa kweli hapa kuna kitu kiovu ninachotetea!?
  kama hakipo basi ni uonevu kusema vijana 50 waliokuwa kwenye hicho chumba cha darasa wasifanye mitihani kwa sababu mmoja/wachache wao wameiba stepler!
  Kingine cha kujiuliza hapa ni kwamba hilo la mwalimu kuwachangisha 1000/= wanafunzi say 50 ili kununua stepler ambayo walijaribu kuinunua na kumpatia akaikataa ni haki?!
   
 15. s

  sugi JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Mkuu kosa la wizi,haliwi solved kwa kurudisha 2 kilichoibwa!wangapi tunawaona kila siku wanafungwa kwa kuiba?si wangetakiwa kurudisha tu kilichoibwa,mwalimu alitaka kukomesha spirit ya wizi,na alitaka wote wa feel hilo tatizo ili kila 1 awe mlinzi wa mwenzake,maana"samaki 1 akioza...."
   
 16. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,472
  Trophy Points: 280
  mimi nimewai kufundisha watoto wa mwanza, yaani watoto wa pale shida tupu..wanaunda mikundi ya ajabu ajabu mara mavampire,machekinolisi n.k kutwa nzima kuchora chora chata na mipicha,dharau kwa kwenda mbele..
  Uwenda wamezoea kudokoa vitu vya walimu sasa huyo mwalimu amemua kuwakomesha.
  Kama ni wilaya magu naomba uni pm jina la shule na mimi nijaribu kusaidia
   
Loading...