Tetra
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 1,526
- 771
ILIKUWA NUSURA IWE KESI KUBWA KWA WAPANGAJI,,BAADA YA MPANGAJI (MWANAUME) KUJIFUNGIA NDANI PASIPO KULA KWA SIKU TATU MFULULIZO ,HATA HIVYO HALI HII ILIPOBAINIKA ALITOLEWA NJE NA KUPEWA HUDUMA STAHILI NA WAPANGAJI WENZAKE,MWANAUME HUYU ALIJIKUTA AKITOKWA MACHOZI YA HUZUNI NA KUONGEA MBELE YA WAPANGAJI WENZAKE UTADHANI ANAONGEA NA MKEWE !!
::
Ulitelekezwa na mumeo ukiwa na mtoto wa miezi mitatu.Ulikuwa ukiteseka na kuumia.Uzuri wako uliniingia moyoni, na tulikubaliana kuoana ili tuwe mke na mume
Kumbuka nilikokutoa mke wangu!
::
Upendo wangu kwako ulikuwa hauna mfano,
Nilimhudumia mtoto mpaka amekua msichana mkubwa,
Nakushukuru pia umenizalia watoto wawili wa kiume ninaowapenda.
Kwa nini umeniacha mke wangu!
::
Ulianza kubadilika ndani ukiwa ni jeuri
Mwanzo nilijua labda ni kwa sababu biashara niliyokuanzishia ndio inakupa kiburi
Lakini kumbe ni zaidi ya hivyo.
Kwa nini unanifanyia hivyo mke wangu.
::
Sasa umetoroka na kuniacha peke yangu,
Umemrudia bwana wako aliyekuacha zamani,
Linaloniuma ni wewe kuondoka na wanangu,
Unaishi nao kwa mume mwenzangu,
Nimekosa nini kustahili hili mke wangu?
::
Nawapenda wanangu
Nakupenda mke wangu
Ulipoamua kuondoka ungeniachia wanangu
Au nao si wangu
Niambie kweli mke wangu!
Nimekosa nini kustahili hili mke wangu!!
=
NDIVYO ALIVYOWASIMULIA WAPANGAJI WENZAKE KWA MAJONZI,NI HAPA IGUNGA TABORA.