Nimekosa mke wa kuoa mpaka leo hii

Nimekosa mke wa kuoa mpaka leo hii

Habarini Wadau,

Sijajua tatizo ni nini. Mpaka leo hii kila mdada ninaekua nae in relationship kwa lengo la kuja kuoana nae basi nakuja gundua mapungufu mengi tu ambayo yananipelekea kuto kumwamini kama atakua mwema katika maisha ya ndoa.

Nimejaribu so many girls lakini la hawajafanania tu na vile mke anavyotakiwa kuwa. Sasa miaka inasonga now na utu uzima waja.

Nahisi nina mkosi kwa kukosa mke mpaka sasa.Wadau hebu nisaidieni njia gani mlizitumia ili kumpata umpendae?

Msaada tafadhali.

Kaka huyo unaemtaka HAYUPO HAPA CHINI YA JUA. Labda umtengeneze mwenyewe ndo atakuwa hivyo utakavyo
 
Tatizo vijana wengi wakiwa wanaomba kupata mwenzi wa maisha wanakuwa tayari na watu wao, unakuwa umeshamweka fulani kichwani so ukilala ukiota unasema umejibiwa kumbe mawazo; hatuachi Mungu afanye ila tunamlazimisha kufanya tunavyotaka
 
Usiwe desperate kuingia kwenye mahusiano let alone kukimbilia kuoa.
Inawezekana umeweka vigezo vya juu sana kwa huyo mwenzi unayemtaka au Inawezekana pia una vigezo vya kawaida tu, ila hujampata wa kwako sahihi. Ni kawaida sana, wala usijione kuwa una mkosi, relax kila kitu kitakuwa mwaaaaaah kwa wakati wake

Lingine umesema "Nimejaribu so many girls lakini hawajafanania. ...". Ukiwa desperate sana utajikuta kila siku una mahusiano mapya afu ukikaa naye after few days/months unagundua kuwa huyo sio mtu sahihi kwako na hii pia inachangiwa na wewe kuingia kwenye mahusiano with so much expectations. Na usiwe Unaingia kwenye mahusiano na negativities, utashindwa kuona positive side ya huyo mtu wako as wewe upo busy kuangalia flaws zake. Kila mtu ana mazuri na mapungufu yake, so angalia kama unaweza kuyahimili mapungufu ya mwenzi wako. Kwa muda huu wewe relax tu kwanza, kaa tu single kwa muda na wala usiwaze sana kuhusu mahusiano. Kila kitu kitakuwa poa tu, let things happen naturally, usiforce mahusiano

Unatumia kinywaji gani nikuagizie bibiee??? hapa mleta mada asipoelewa basi tena.
 
Mmmh ukute wewe ndio una shida alafu unawaona hao unaowapata ndio wenye shida, hakuna mwanamke perfect ndugu labda umuumbe, ila napo akiingia kwenye hii dunia tafrani bado utamuona ana mapungufu.
 
mkuu ankol mbona watoto wapo kibao.Nahisi unatatizo dogo tu wala sio mkosi,
*Hauko vizuri kwenye kufanya uchaguzi/selections.
Ushauri wangu,
1.Acha kutongoza wanawake bila kufatilia mienendo yao kwanza yani usiokote okote wapenzi tu.Hutajua yupi ni sahihi.Binafsi kufanya kile ninachokiita "smart moves" ni bora maana utapunguza list ya kufahamiana na watu wa hovyo.

2.Jenga uhusiano na mtu ambae anaelekea kuwa na chemistry na wewe,napendekeza pia awe mtu mwenye akili ya maisha zaidi mwenye mawazo ya kukujenga kuliko anaefikiria vitu vya kipuuzi puuzi tu kama starehe.Hili utalijua kwenye mazungumzo yenu ya mara kwa mara.

3.Sio lazma wote tuoe wasichana kama akina Kim Kardashian,Amber Rose,kama kipaumbele chako ni muonekano mzuri sana ili usifiwe una mke mzuri ila kichwani awe bogus ni shida na utauweka sana kwa bongo hii iliojaa wasanii wa mapenzi.

4.Hakunaga mwanamke mmbaya kaka. Ma wife material hawanaga muonekano mzuri sana(Wapo kawaida sana)hapo awali maana hawajawekaga urembo kama kipaumbele sana maishani zaidi ya mipango yao kimaisha isipokuwa wanauweza wakipata fursa yani matunzo mda ukiwadia.Ndio maana wakishaolewa wanazidi kuwaga wazuri mpaka tunashangaa!

Ukizingatia haya nina imani itakuweka karibu zaidi na kumpata mwanamke sahihi zaidi mkuu atakaekufaa sio wababaishaji.
 
Last edited by a moderator:
hakuna mtu anayefikiri kwa umakin kuhusu mwanamke na bado akamwoa. kaka kama inawezekana pata tu mtoto mtunze vizur na kama nalo gumu acha tu ilimrad jiwekee mazingira mazuri ya namna utapata huduma ukiwa mzee au mgonjwa. Sijui kwann Tanzania tusiwe na mfumo mzuri wa kutunza wazee maana binafs hofu ya kutooa iko hapo tu kuwa nani atakuangalia kiundan uzeeni?!!! kama kukuosha. kukuvalisha. kukulisha. kukugusa popote. kutuma na kuamini (trust). kitu kingne oa ukiwa na umri mkubwa kama 50 hivi iwe rahis kudharau mambo ya kike ya ovyo na busara na hekima zimeshakomaa.
 
Usiwe desperate kuingia kwenye mahusiano let alone kukimbilia kuoa.
Inawezekana umeweka vigezo vya juu sana kwa huyo mwenzi unayemtaka au Inawezekana pia una vigezo vya kawaida tu, ila hujampata wa kwako sahihi. Ni kawaida sana, wala usijione kuwa una mkosi, relax kila kitu kitakuwa mwaaaaaah kwa wakati wake

Lingine umesema "Nimejaribu so many girls lakini hawajafanania. ...". Ukiwa desperate sana utajikuta kila siku una mahusiano mapya afu ukikaa naye after few days/months unagundua kuwa huyo sio mtu sahihi kwako na hii pia inachangiwa na wewe kuingia kwenye mahusiano with so much expectations. Na usiwe Unaingia kwenye mahusiano na negativities, utashindwa kuona positive side ya huyo mtu wako as wewe upo busy kuangalia flaws zake. Kila mtu ana mazuri na mapungufu yake, so angalia kama unaweza kuyahimili mapungufu ya mwenzi wako. Kwa muda huu wewe relax tu kwanza, kaa tu single kwa muda na wala usiwaze sana kuhusu mahusiano. Kila kitu kitakuwa poa tu, let things happen naturally, usiforce mahusiano

Ushaurii mzuri saana huu...
 
Back
Top Bottom