Nimekataliwa kwenye maombi ya kazi kisa Ulemavu wangu

Hivi Tanzania kuna sheria ya kukataza ubaguzi wa walemavu kwenye mambo kama ya ajira?

Nchi kama Marekani kuna sheria kali dhidi ya ubaguzi wa rangi, jinsia, na ubaguzi dhidi ya walemavu katika ajira.

Inaitwa "The Equal Employment Opportunity Act of 1972"

Nilijaribu kutafuta kama hiyo sheria ipo ila sijaiona.

Kilichopo ni muongozo wa uwiano wa kuajiri kati ya wasio walemavu na walemavu, lakini kama tunavyojua bongo sheria au miongozo haifuatwi ndio athari zake ndio hizi
 
Tunaishi kwenye Dunia ya ushindani Mkuu.

Kwa nchi ya ulimwengu wa tatu dhana ya kufata sheria na taratibu kwa ukamilifu haipo. Sheria inayohusu walemavu kwenye ajira inawalinda.

Mimi ni ww kabisa,nina usikivu hafifu sema mm haya mapungufu huwa siyapi nafasi.

Wakati mwingine ulemavu ni vile unavyojichukulia ww,naamini kwa namna mmoja au nyingine kila mtu ni mlemavu kwa tafsiri yake.

Ukweli ni kwamba matangazo mengi ya kazi ya taasisi za serikali hutaka kujua endapo ww ni mlemavu uoanishe hali yako ili wakuhudumie inavyotakiwa.

Nilimaliza chuo 2015, na 2016 nikapata kazi. Muhimu ni kujiamini tu,kama ww ni bora kuliko wengine utachaguliwa tu haijalishi hali yako mkuu.

Naomba ni PM.
Siogopi hii hali ndio maana naendelea kutuma maombi kila ninapoona nafasi ambayo ipo kwenye taaluma yangu.

Ningefanyiwa Interview halafu nikaambiwa sijafaulu Interview hapo angalau ingeleta picha nzuri, kuliko na kuambiwa kuwa hatukupi kazi kisa ni ulemavu, wangeangalia kwanza uwezo wangu halafu wajumlishe na huu ulemavu ndio wangetoa maamuzi yaliyo mazuri.
 
Guys hivi kwa wenye vigugumizi sana huwa wanakua na favor zao katika usaili?maana nina mdau wngu ana akili sana..tatzo lake ni hlo tu..Akiitwa katika usaili kigugumizi hasa akiwa at STP..Panelists wawe na huruma aisee
Kati ya interview alizowahi kufanya aliambiwaje kuhusu hicho kigugumizi
 
Mkuu upo ktk kile chama cha walemavu, nafikiri kuna kipaumbele chenu ktk ajira za serikalini ,kikubwa jaribu kutafuta connection ya kuonana ana kwa ana ,uso kwa uso na afisa muajiri serikalini hii italeta matokeo chanya nafikiri.
 
Huwa hajionyeshi kama ana kigugumizi,Panelists humhisi FEAR IS WHAT MAKES HIM STUTTERING..Sometimes akiitwa sehemu interview hua hatokei kwa kuogopa atashindwa kuongea..Huruma sana aisee.
Mshauri asiwe anaogopa kwenda akiitwa ili akapate uzoefu wa interview
 
Mkuu upo ktk kile chama cha walemavu, nafikiri kuna kipaumbele chenu ktk ajira za serikalini ,kikubwa jaribu kutafuta connection ya kuonana ana kwa ana ,uso kwa uso na afisa muajiri serikalini hii italeta matokeo chanya nafikiri.
Niliwahi kufuatilia ili niweze kujiunga ila nilibaini kuna miyeyusho kama tunavyojua vyama vingi vya makundi mbalimbali vina msaada mdogo kwa wahusika. Niliamua kupambana kivingine.

Nilijaribu kuwasilisha taarifa zangu pale CCBRT Hospital, kuna kitengo cha kushughulikia watu wenye ulemavu katika masuala ya kazi/ajira ila hadi sasa sijapata mrejesho wowote ingawa najua mambo huwa hayaendi haraka
 
Alifanya utafiti ili kubaini ni aina gani hii ya ndoano iliyotegwa kama itakuwa na manufaa chanya au hasi kidimbwini. Mara ghafla notification ikaibuka ikisomeka "Kazi uliyoomba na usikivu hafifu sidhani".
Umejaribu kutafuta hearing aids ? (kwa teknolojia ya sasa huenda hilo lisiwe tatizo wala ulemavu); unaweza ukaperform na kuwa na usikivu mahili kushinda hata paka...

Kila kazi ina requirements zake...

Hata mimi nikiomba kazi pale Barcelona ili nikawe playmaker nikinyimwa sio kwamba ni wabaguzi huenda kuna mtu kama Messi na kwa jinsi wanavyocheza huenda mimi nisikizi vigezo...
 
Umejaribu kutafuta hearing aids ? (kwa teknolojia ya sasa huenda hilo lisiwe tatizo wala ulemavu); unaweza ukaperform na kuwa na usikivu mahili kushinda hata paka...

Kila kazi ina requirements zake...

Hata mimi nikiomba kazi pale Barcelona ili nikawe playmaker nikinyimwa sio kwamba ni wabaguzi huenda kuna mtu kama Messi na kwa jinsi wanavyocheza huenda mimi nisikizi vigezo...
Hearing Aids nishawahi kutumia bila mafanikio yoyote, nimetumia hivyo vifaa vya aina tatu tofauti.

Hospital nishaenda mara nyingi sana, Muhimbili nimeenda mara 3, TMJ mara 1, Ekenywa mara 1, Hear Well mara 1(hii ni Clinic ya masikio ipo Upanga, Diamond Tower)

Kote huko walisema nitumie vifaa lakini hivyo vifaa havikusaidia chochote
 
Back
Top Bottom